Mzee Faraj Katalambula Amefariki Dunia

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062

Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini Tanzania
marehemu Mzee Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho
Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.

Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili.
Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata
kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu
kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula ambaye ni Mtoto wa Marehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.
From: g sengo

NB: Nimeambiwa kuwa atazikwa leo huko Isevya, TABORA. R.I.P. Faraj Katalambula.
 
I believe Pili Pilipili was and to me is the best Play, yaani ukiisoma ile kitu huwezi weka chini hadi last page, tumepoteza shujaa wengi wa waliobakia ni wale wa kukopi na kupesti hadithi toka kwenye mtandao..... sorry kwa wanaomfahamu vizuri hivi ndie huy huyu alieandika na ile riwaya ya SIRI ya SIFURI???
 
Hapana SIRI YA SIFURI mwandishi alikuwa Mzanzibari jina limenitoka (sio Shafi).......character alikuwa INSPECTOR NAJUUM
 
FARAJ KATALAMBULA KUZIKWA MKOANI TABORA

Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini marehemu Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.

Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili. Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula mwanae marehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.
From: g sengo

NB: Nimeambiwa kuwa atazikwa leo huko Isevya, TABORA. R.I.P. Faraj Katalambula.

Poleni sana wafiwa, wana Tabora, pamoja na watanzania wenzangu walio ktk tasnia ya uandishi wa vitabu na riwaya!

Nakumbuka sana kitabu cha Faraji H. Katalambula: "Simu ya Kifo" pia Filamu ya "simu ya kifo" iliyotokana na Kitabu husika.
Ktk filamu hiyo Mzee Kipara alicheza kama Inspecta Wingo.

RIP Faraji H. Katalambula
 
Pumzika kwa amani F. H. H. Katalambula, nakumbuka sana Riwaya zako; "Simu ya Kifo" and "Buriani" pia na Jarida la Picha "Film Tanzania" na wahusika wake Lawalawa na Mzee Frijala.

Nukumbuka wakina Marehemu Mzee Kipara "walitoka" kwenye hizo filamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom