Mzee afariki kwa kumwagiwa upupu

dropingcoco

Senior Member
Jun 21, 2008
124
11
Wazee wanaodai mafao yao ya kustaafu, jana walifukuzwa mahakamani kwa kumwagiwa upupu, habari ya kusikitisha ni kwamba mzee mmoja amefariki kutokana na adha ile, watanzania tujiulize......ilishindikana nini kwa polisi kuwaondoa wale wazee pale katika hali ya kiustarabu na kulazimika kutumia maji ya upupu, kama vile walikuwa ni magaidi walioshindikana, hivi wale wazee walikuwa na nguvu gani kuwazidi polisi? hii ndio tunaita amani katika nchi pale unapodai haki yako?....TUTAFAKARI

SOURCE: ITV
 
Hivi kupata haki ni lazima wengine wawe kafara? mwaka huu sijui, tutafika wapi. Na polisi wetu ndio hao wameshazoea kuwatendea raia unyama namna hii, badala ya kuwa "usalama wa raia"!
 
JK alisema wiki hii hakuna atakaye mwaga damu, CCM ni chama cha amani kulikoni sasa kuanza kuua wazee?
 
tanzania kudai haki yako ni kosa la jinai

nashangaa sana na naumia sana

ni wakati wetu kufanya mabadiliko watanzania

chagua slaa
 
Nimeona hiyo taarifa ITV nimependa walivyoripoti! Ila KOVA kakataa kwamba hakuna aliekufa! nahisi tuandamane
 
Wazee wanaodai mafao yao ya kustaafu, jana walifukuzwa mahakamani kwa kumwagiwa upupu, habari ya kusikitisha ni kwamba mzee mmoja amefariki kutokana na adha ile, watanzania tujiulize......ilishindikana nini kwa polisi kuwaondoa wale wazee pale katika hali ya kiustarabu na kulazimika kutumia maji ya upupu, kama vile walikuwa ni magaidi walioshindikana, hivi wale wazee walikuwa na nguvu gani kuwazidi polisi? hii ndio tunaita amani katika nchi pale unapodai haki yako?....TUTAFAKARI

Jana jioni nilikuwa Kawe Police Station, nikifuatilia masuala fulaniya mai waifu wangu. Nikawaona vijana wa Kova wakivaa combat zao nyeupe. Kumbe ndio wale - tena wengine wadogo sana, hao wazee wanaweza kuwa BABU na BIBI zao - waliokuwa wakiandaliwa kwenda kuwatimua?

JK anasema kwamba kuna wanasiasa wanawashawishi wananchi kumwaga damu. Je, huku kwa Jeshi la Polisi, tena kwa wazee wanaodai haki yao WALIOSHINDA MAHAKAMANI, ndio nini?

Hii sasa si aibu. Ni fedheha na jekeli. Fedheha kwa kuwa damu imemwagika pasi na sababu. Kejeli kwa kuwa hatuna uwezo wa kuwachukulia Polisi hatua za kisheria, kwani wao wameshika mpini sisi tumeshika makali.

2010 TUBADILIKE, TUSIDANGANYIKE TENA!
 
Wazee wanaodai mafao yao ya kustaafu, jana walifukuzwa mahakamani kwa kumwagiwa upupu, habari ya kusikitisha ni kwamba mzee mmoja amefariki kutokana na adha ile, watanzania tujiulize......ilishindikana nini kwa polisi kuwaondoa wale wazee pale katika hali ya kiustarabu na kulazimika kutumia maji ya upupu, kama vile walikuwa ni magaidi walioshindikana, hivi wale wazee walikuwa na nguvu gani kuwazidi polisi? hii ndio tunaita amani katika nchi pale unapodai haki yako?....TUTAFAKARI

Lakini tunaomba SOURCE yako!
 
Hivi kupata haki ni lazima wengine wawe kafara? mwaka huu sijui, tutafika wapi. Na polisi wetu ndio hao wameshazoea kuwatendea raia unyama namna hii, badala ya kuwa "usalama wa raia"!

Hivi huko bongo kwanini mpaka leo bado tunafanya mambo ya kutumia nguvu wakati watu wanapodemonstrate kupinga kitu kwa amani, manake mie na mifano ya huku RSA watu wanapoandamana huwa ni basic right n auwa wanakuwa escorted na polisi na ku present petions to concern authorities safi kabisa lakini mambo ya kupiga watu bila sabau huwa siyaoni au kutumia unnecessary force for peaceful demonstration hakuna huku, na mfano mwezi uliopita wafanyakazi waligoma mwezi mzima lakini sikuona demontrator wanapigwa au kuzuiwa kuandamana, manake hata polisi wanafahamu haki za raia ama sivyo serikali inaweza kuwa sued kwa uzembe wa kuumiza mtu bila sababu ya kisheria! Inabidi hata polisi nao waelewe haki hizi za msingi!! Inabidi vyombo vya usalama vieleweshwe haya yote na kujua constitutional rights za raia. This is unfortunate for a country like ours which is still wants to build strong democratic institutions!
 
Ndio utawala wa sheria! Jeshi la polisi na ulinzi wa raia. HONESTLY THE SO CALLED VYOMBO VYA USALAMA VINGEKUWA VINAWAJIBIKA KWA WANANCHI NA SIO WATAWALA KUSINGEKUWA NA UPUUZI KAMA TUNAOUONA. THEY CAN KILL, MAIM AND DO WHATEVER BUT NOTHING WILL HAPPEN TO THEM EXCEPT BE PRAISED/PROMOTED. MNAKUMBUKA MISTAKEN IDENTITY YA KOMBE, VIJANA WALIOUAWA ARUSHA!! dereva TAXI DAR ETC.
 
JK alisema wiki hii hakuna atakaye mwaga damu, CCM ni chama cha amani kulikoni sasa kuanza kuua wazee?

ndo nanyie mjipange, atakaye thubutu kutaka kuvuruga amani atakiona cha mtema kuwasha.
 
Ndio utawala wa sheria! Jeshi la polisi na ulinzi wa raia. HONESTLY THE SO CALLED VYOMBO VYA USALAMA VINGEKUWA VINAWAJIBIKA KWA WANANCHI NA SIO WATAWALA KUSINGEKUWA NA UPUUZI KAMA TUNAOUONA. THEY CAN KILL, MAIM AND DO WHATEVER BUT NOTHING WILL HAPPEN TO THEM EXCEPT BE PRAISED/PROMOTED. MNAKUMBUKA MISTAKEN IDENTITY YA KOMBE, VIJANA WALIOUAWA ARUSHA!! dereva TAXI DAR ETC.

kwani raia ni hao tu waliokuwa wanafanya fujo nje ya mahakama kuu na kutishia amani wafanya kazi wa mahakama, kuzuia shughuli za kiuchumi za raia wema, kufunga barabara, kuendelea kuchafua mazingira.
 
wanajikaanga kwa mafuta yao....naomba wajulisheni ndugu,jamaa hasa mababu/mabibi zetu maana yajua CCM watapindisha ukweli hasa wale wanaoiona CCM ndiyo Mkombozi wao...Malaria Sugu uko wapi njooo uwatetee Mafisadi...
 
Back
Top Bottom