Mzanzibari aliyekamatwa na FBI kwa ugaidi arejeshwa

Unajua Mods na Invisible,

Mfike mahali muwe serious, maana huyu mtu mmoja mwisho ataishia kuiua hii forum, tunajaribu kumheshimu lakini naona anafikiri na sisi wote humu forum ni kama kamati za UV-CCM na Nchimbi,

Wewe mkuu unayeleta maneno ya udini, unajifanya kutukana wa-Islam wakati wewe mwenyewe ni Mu-Islam, tena una maneno mengi sana machafu against wa-Kristo kule kwenye section ya dini, nakuomba uelewe kuwa unafahamika sana, inaonekana nia yako ni kuhakikisha either umekuwa kinara wa hii forum, au unaivuruga, na tayari umepata wafuasi flani ambao hawakuelewi vizuri, I know you now stop this nonesense!

FMES. Kukata mzizi wa fitina naona umtaje tu huyu jamaa. Ninavyokumbuka mimi, mantra ya humu ni; haogopwi mtu humu!
 
sasa huyu kijana akiwa gaidi kweli mtamlaumu. Aanze kukaba wamarekani nae huko tanzania maisha ni tit for tat. Violence will be treated with violence by any means necesary.
Ajaribu aome cha mtema kuni. Asijaribu maana kifo kitakuwa karibu naye nakwambia. Acheni kumdanganya
Ashukuru tu kwamba karudi nyumbani salama.
Mmarekani anayo haki ya kufanya hayo maana aliyeumwa na nyoka akiona hata mjusi........
Habari ndio hiyo.
 
FMES. Kukata mzizi wa fitina naona umtaje tu huyu jamaa. Ninavyokumbuka mimi, mantra ya humu ni; haogopwi mtu humu!

Ninayemlenga ananielewa, that is what counts unless you have a problem too, au? maana sina uhakika haya yamekukutaje bro au ni wewe?

Kwa sababu swali langu liko very clear kuuwana kwa wakristo na waisilamu duniani kunahusiana nini na kushikwa huyu mbongo huko kwenye declared unfriendly zone na US, katika vita vyao na wanaowaita magaidi?
 
Hapana FMES. Kwa sababu umemtuhumu huyo jamaa kwenye public forum ingekuwa vyema vilevile kumtajaili jamii iamue kama anafaa kutengwa au la. Ungetaka kumpelekea ujumbe yeye, ungemtumia PM. Kwa kufanya hivi unafanya watu waanze ku'speculate' na hii si vyema. Mtaje tuu. Unamuoneaje haya muovu huyo?

Kwa bahati mbaya wamarekani (sio wote) wameunganisha ugaidi na uislamu. Huyu bwana alikamatwa si kwa sababu tu alikuwa katika eneo la vita bali kwa sababu alikuwa ni muislamu. Angekuwa mchungaji asingekamatwa. Kutokana na hili kuna wenzetu wanaona kuwa ni haki alivyofanyiwa kwa vile nao wanataka kutoa hukumu ya jumla kwa watu wa dini ile. Hiyo mifano ya wakristu kuuana na waislamu (niliwataja pia wafuasi wa buddha, wahindu , wayahudi na wakommunisti) ilikuwa ni kuonyesha kuwa hakuna dini yenye monopoly na uovu, ugaidi ukiwa mmojawapo.

Ingawa ni very tempting kuhukumu jamii kwa makosa ya wachache wa jamii hiyo ina hatari zake. Kudai kuwa solution ya ugaidi, ni waislamu wote waokoke, ni mawazo potofu na ni kuwatukana waislamu, maana kuna magaidi wametoka hata katika hao wanaojiita wameokoka (KKK kiliongozwa na watu wa kanisa n.k., anti-abortion activists, wakina Timothy McVeigh etc etc)! Moja ya sababu iliyomfanya huyu bwana akamatwe na kuteswa ni imani yake. Hilo halikwepeki.

Tusiopenda collective punishment tunaona hiyo sio haki ndiyo maana tunapiga kelele.
 
SMZ yafuatilia kuachiwa kwa mtuhumiwa...

2008-09-03 10:27:02
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema itafuatilia suala la Mtanzania, Suleiman Abdallah Salim (Morris) wa Zanzibar, ambaye ameshikiliwa katika magereza mbalimbali na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema SMZ itahitaji kufahamu jinsi haki za binaadamu zilivyozingatiwa kipindi chote cha miaka mitano alichowekwa kizuizini.

Hatua hiyo, inachukuliwa baada ya Mtanzania huyo kuachiwa kutoka gerezani nchini Afghanistan na kulalamika kwamba, aliteswa na kupata madhara makubwa ya afya na sasa anadai amekuwa akipoteza kumbukumbu.

``Tutafuatilia kupitia njia za kidiplomasia katika Ubalozi wa Marekani ili kujua jinsi haki za binadamu zilivyozingatiwa, kwa vile huyo ni raia wetu,`` alisema Waziri Hamza.

Alisema serikali imeshtushwa na taarifa za kuteswa raia wake na baadaye kuachiwa bila kuzingatia athari alizopata.

``Kama hayo malalamiko ni ya kweli, basi ni uvunjaji wahaki za binadamu na sisi kama serikali tutaanza kufanya uchunguzi,`` alisema Waziri Hamza.

Akizungumza nyumbani kwao Mtaa wa Mwanakwerekwe, Suleiman alisema hivi sasa amekuwa akipoteza kumbukumbu na kusikia maumivu makali mwilini.

``Sijisikii vizuri kuzungumza kwa sababu nimekuwa nikipoteza kumbukumbu kwa muda mfupi na ninahitaji matibabu,`` alisema.

Alieleza hivi sasa anawasiliana na Shirika la Msalaba Mwekundu kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kuzorota afya yake, hali iliyosababishwa na mateso aliyopata kwa nyakati tofauti kwenye magereza ya nchini Kenya, Somalia na Afghanistan.

``Natamani kuzungumza na vyombo vya habari, lakini afya yangu sio nzuri napoteza kumbukumbu nahitaji matibabu,`` alisema Salim kwa shida.

Awali, akisimulia chimbuko la kukamatwa kwake, alisema alikamatwa eneo la Abusasu mjini Mogadishu mwaka 2003, akiwa kwenye shughuli zake za biashara na kuingizwa katika gari bila kufahamu anakopelekwa.

``Waliniambia mimi ni Msomali, nilikataa nikiwaambia ni Mtanzania, kisha wakasema ni Muyemeni nikasema ni Mtanzania na walipoona nasema Kiswahili wanakiambia nimlete ndugu yangu aniwekee dhamana nikawaambia sina jamaa Nairobi na kwetu ni Tanzania,`` alisema.

Baadaye alisafirishwa kutoka Nairobi hadi Afghanistan na kuwekwa gereza la Marekani ambalo alidai limeghubikwa na giza.

Alisema kwenye gereza hilo na wenzake, huku wakiishi maisha magumu bila kuruhusiwa kuzungumza, walipewa mateso kila mara.

Salim alisema baadaye alihamishia kambi ya jeshi huko Bagram akiwa amefungwa kwa minyororo na kuvalishwa vifaa kwenye macho ili asitambue anakopelekwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakar Khatib Shaaban, alisema Mtanzania huyo ana haki ya kufungua kesi ya madai dhidi ya serikali ya Marekani.

``Kwa sababu hili ni jambo binafsi, mhusika kama anahisi haki zake za kibinaadamu zimevunjwa ana haki ya kufungua kesi ya madai, lakini polisi haina nafasi ya kuingilia uhuru wake,`` alisema Kamanda Shaaban.

Suleiman maarufu Morris ni kijana aliyekulia Mtaa wa Malindi Unguja na shughuli zake kubwa zilikuwa ni uvuvi, ambazo zilimfanya kufika Somalia ambako alikamatwa na kuhusishwa na kundi la Al Qaeda linaloongozwa na Osama Bin Laden.

Wakati huo huo, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haihusiki na kuachiwa huru kwa mtuhumiwa huyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema serikali haikuhusika kwenye mazungumzo ya kidiplomasia wala msaada wa kisheria.

Suleiman alirejeshwa Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kwa msaada wa Chama cha Msalaba Mwekundu baada ya kuishi kwenye magereza kadhaa ya Afghanistan kwa miaka mitano.
 
Kibunango,
Huyo waziri ni muongo tu hamna lolote anataka kumweka sawa huyo Suleiman. Kwani miaka yote hiyo walikuwa hawajui kwamba kuna mzanzibara amewekwa kolokoloni nje?
Kaa mkidanganyika kama kawaida yenu.
Wote hao wanajua kuwa huyu bwana kakamatwa nchi ya watu tena kulikokuwa na hatari ya ughaidi. Unasikia mwenyewe kuwa hata watu waliokuwa katika orodha ya FBI aliwaambia anawafahamu. Huwezi kuelewa hapo?
Nyie wazanzibari msipokuwa macho katika kutumiwa na extimists, shauri yenu. Mtaishia kulalamika tu kila siku huku mnasota jela za Marekani. Msicheze na wamarekani maana hawana huruma kwa maghaidi.
Yule aliyekamatwa Pakstani mbona hiyo serikali yenu ya zanzibar wanajua aliko lakini hakuna wanalofanya?. Wanajua nyie mnapenda kuchezea danger zone. Na hayo ndio matokeo yake.
Habari ndio hiyo.
 
Kibunango,
Huyo waziri ni muongo tu hamna lolote anataka kumweka sawa huyo Suleiman. Kwani miaka yote hiyo walikuwa hawajui kwamba kuna mzanzibara amewekwa kolokoloni nje?

Ndio hapo na mimi napigwa na butwaa....
Unasikia mwenyewe kuwa hata watu waliokuwa katika orodha ya FBI aliwaambia anawafahamu. Huwezi kuelewa hapo?
Kweli hata mimi nilimsikia anasema wanafahamiana na wale watuhumiwa wa ugaidi akina khalfan.......
Nyie wazanzibari msipokuwa macho katika kutumiwa na extimists, shauri yenu
??????? ina maana wanatumiwa? na wakina nani?
Yule aliyekamatwa Pakstani mbona hiyo serikali yenu ya zanzibar wanajua aliko lakini hakuna wanalofanya?.
Khalfani Ghailan alikamatwa katika battle na majeshi ya pakistan akiwa katika kambi ya Al qaida.....mama yake alilia sana na kusema haamini kaama mwanae ni gaidi.Alisema anasingiziwa!
 
nashangaa huyu mtanzania.....membe kazi yako si kwenda kutanua tu marekani, kazi yako ni kama hii pia

Membe atalalamika wapi huyo kibaraka tu wa wamerakani kazi kujikomba komba tu kwa wamerakani kisha tunakuja kuumia sisi raia wa kawaida.....ni bora na mara mia kuunga ushirika na China na sio hawa wapuuzi wamarekani..
 
Kwa bahati mbaya wamarekani (sio wote) wameunganisha ugaidi na uislamu. Huyu bwana alikamatwa si kwa sababu tu alikuwa katika eneo la vita bali kwa sababu alikuwa ni muislamu. Angekuwa mchungaji asingekamatwa. Kutokana na hili kuna wenzetu wanaona kuwa ni haki alivyofanyiwa kwa vile nao wanataka kutoa hukumu ya jumla kwa watu wa dini ile. Hiyo mifano ya wakristu kuuana na waislamu (niliwataja pia wafuasi wa buddha, wahindu , wayahudi na wakommunisti) ilikuwa ni kuonyesha kuwa hakuna dini yenye monopoly na uovu, ugaidi ukiwa mmojawapo.

Ingawa ni very tempting kuhukumu jamii kwa makosa ya wachache wa jamii hiyo ina hatari zake. Kudai kuwa solution ya ugaidi, ni waislamu wote waokoke, ni mawazo potofu na ni kuwatukana waislamu, maana kuna magaidi wametoka hata katika hao wanaojiita wameokoka (KKK kiliongozwa na watu wa kanisa n.k., anti-abortion activists, wakina Timothy McVeigh etc etc)! Moja ya sababu iliyomfanya huyu bwana akamatwe na kuteswa ni imani yake. Hilo halikwepeki.

Mkuu naomba tena kukuuliza, maneno ya quote ya juu ndio hasa hoja ya msingi ya mtoa mada, sasa ninajaribu kuyaoanisha na yako hapa chini sioni yanapokutana,

FBI wamemshika jamaa kwa sababu walidhani kuwa ni gaidi, na sio kwamba ni mara ya kwanza wamefanya hivyo na record iko very clear kwenye hilo, sasa maneno yako yanahusiana vipi na sisi Tanzania, na wa-Kristo au Wa-Isialmu wa Tanzania?

Mbona sioni connection zaidi tu ya kujaribu kupanda mbegu ambazo haziwezi kutusiadia sisi wananchi tunaokuja hapa kuelimishwa kuhusu matatizo ya taifa letu? I mean watu wangapi wasio na makosa wameshiwka wapo Guantanamo tena wa mataifa mabli mbali? Hata sisi tulipokwenda Kampala kumuondoa Amin, tulishika watu wengi wasiohusika kabisa na vita, US iko kwenye vita na magaidi sasa wakikushika kwenye ameneo ambayo wao wamesha-declare kuwa ni ya vita, sisi Tanzania tutakusaidia vipi?

Na what that has to do na dini yako au ya US? au Tanzania? I just do not get it!

FMes,
Nimeongeza maneno ya Fundi Mchundo. Naona yeye kanielewa ninasema nini. Ninachosema ntarudia kwa kifupi. Tanzania si KISIWA. Haya mambo ya dini, ubagudhi wa rangi, abortion, ushoga, madawa ya kulevya, ujambazi, sex business, siasa, samaki wakubwa kuwala wadogo nk yapo dunia nzima na yapo Tanzania. Ninavyojua mie ili kusolve problem, lazima uende kwenye mizizi na huko ndiko utauona MZIZI wa FITINA na kuung'owa. Kukaa chini na kusema "mie Tanzania simo" kwa karne hii HAIWEZEKANI. Sasa basi hizi dini zote sisi tuliletewa. Kama waleta dini wanapigana na ugomvi wao wanauleta hadi kwetu (Morris and USA Ambas. bombing etc) si kuwa tayari tumo ndani? Au wataka nini kitokee ujuwe Tanzania haya machafuko ya dini yanaweza siku moja yakawa makubwa?
Nimeandika ili kuonyesha huu ugomvi wao ulianza wapi. Kutoka hapo ndiyo sasa cha kujiuliza kama VIPORO vya ugomvi wa Wazungu na Waarabu huko Jerusalem miaka hiyo na sasa wajukuu wao, kuna haja kweli ya sisi Watanzania KUUINGILIA? Kumbuka kuna Watanzania walisaidia kutengeneza bomu lililolipua ubalozi wa USA Tanzania na Watanzania wengi wakafa kuliko hata Wamarekani. Laiti wangelijua wanasaidia ugomvi wa watu wasingelifanya hivyo. Kama kuelezea KIINI cha ugomvi wa dini ni KUPANDA MBENGU, inawezekana. Ila mie naona napanda mbengu nzuri tu. Kama Watz walikamata watu wasiohusika huko Uganda, nakubaliana na wewe. Na ukitaka kulaumu usilaumu VITA au Wanajeshi. Tafuta Mzizi wa fitina ulioanzisha hii vita na huo ndiyo UULAUMU. Sijui ni JKN aliyeanzisha vita au Idd Amini. Ukiupata na KUUONYESHA huo mzizi, utaweza kusolve ili mara nyingine lisitokee tena. Ukiujadili huo mzizi "SIDHANI KAMA UNAPANDA MBENGU MBAYA TANZANIA" kwa sababu tu vita na kukamatwa kulitokea Uganda.
 
Sikonge hajakosea. Mbengu zipo. Wako wakristu wanaoamini kuwa haya yote yaliyomkuta ni haki yake maana si wanadini wenzake ndiyo wanaojilipua huko ulaya na marekani? Na kuna waislamu watakaomtetea Morris kwa sababu tu wanaona hii ni ishara nyingine ya chuki ambayo wakristu waliyokuwa nayo dhidi ya waislamu. Ninachojaribu kufanya ni kuwakumbusha kuwa badala ya kuhukumu dini, tuwahukumu watendaji.

Kama tulipoenda Uganda tuliwashika watu kwa vile tu walitokea kabila moja na Idi Amin basi nasi tunastahili lawama. Na hasa kama tuliwatesa na kuendelea kuwashika hata pale tulipogundua kuwa wao hawakushiriki katika maovu ya Idi Amin. Ninavyojua mimi ni kuwa ingawa kweli walikuwepo wakorofi wachache waliofanya tofauti ( kama ninavyosikia walivyo mapolisi wachache Oistabei na kwingineko) lakini hii haikuwa policy yetu kule Uganda. Waganda wangeisha tuanika.

Katika demokrasia ya magharibi kumshika mtu bila kumueleza makosa yake, kumuonyesha ushahidi uliopo dhidi yake na kumpa nafasi ya kujitetea katika mahakama ni ukiukwaji wa haki ya binadamu. Kosa si kumkamata tu Morris bali ni kumtesa na kumshikilia bila kumpa nafasi kujitetea katika mahakama ya wazi! Ndiyo maana wengi wanawalaumu wamarekani maana mwishoni hakuta kuwa na tofauti kati yao na huyo wanayemwita gaidi, ambaye nae anawahukumu watu kwa kutoka tu katika jamii fulani.

Amandla!
 
William Bennett, aliwahi kusema, hypothetically, kuwa kama mtu anataka kupunguza crime marekani moja ya njia ni ku'abort' watoto wote weusi! Kwa vile sehemu kubwa ya waliojela ni weusi basi hii hupothesis ina make sense. Hakikisha watu weusi wanapungua basi uhalifu utapungua. Ni mtazamo kama huo ndiyo unaochangia mtazamo wa baadhi ya wamarekani dhidi ya ugaidi unaowahusu wao. Ukiwafunga waislamu wakutosha (hasa wale wenye imani kali) basi ugaidi utapungua! Ndiyo maana collateral damage kama huyu Morris haziwasumbui maana si hata Fupi nae alitokea unguja! Na yeye alikuwa mtu simple, hajui hata kuendesha gari! Mawazo kama haya, yasipokemewa ndiyo yatakayotufikisha pabaya. Kukataa kuyazungumzia si solution.
 
1.
Hapana FMES. Kwa sababu umemtuhumu huyo jamaa kwenye public forum ingekuwa vyema vilevile kumtajaili jamii iamue kama anafaa kutengwa au la. Ungetaka kumpelekea ujumbe yeye, ungemtumia PM. Kwa kufanya hivi unafanya watu waanze ku'speculate' na hii si vyema. Mtaje tuu. Unamuoneaje haya muovu huyo?

Nimeweka ukweli na anayehusika anaujua, sasa vipi mbona umekuuma sana unahusika na huyo jaamaa au vipi? Maana personal sihitaji lectures zako kuhusu namna ya kufuata sheria za hii forum katika kutoa maoni yangu, una haki ya kujibu maneno yangu lakini other than that huna haki ya kunishurutisha anything hapa, au? Ninarudia kuwa wale wote wanaotaka kutuletea udini hapa waende kwenye section ya dini au watoke maana tunachoishwa na hizi confusions, na mimi siwaogopi ndio imetoka hiyo vipi na wewe ni mmoja wao nini?

2.
Kwa bahati mbaya wamarekani (sio wote) wameunganisha ugaidi na uislamu. Huyu bwana alikamatwa si kwa sababu tu alikuwa katika eneo la vita bali kwa sababu alikuwa ni muislamu. Angekuwa mchungaji asingekamatwa. Kutokana na hili kuna wenzetu wanaona kuwa ni haki alivyofanyiwa kwa vile nao wanataka kutoa hukumu ya jumla kwa watu wa dini ile. Hiyo mifano ya wakristu kuuana na waislamu (niliwataja pia wafuasi wa buddha, wahindu , wayahudi na wakommunisti) ilikuwa ni kuonyesha kuwa hakuna dini yenye monopoly na uovu, ugaidi ukiwa mmojawapo.

1. Kama ni kweli basi Wa-Islam wote USA wameshikwa? Ni hao hao wa-Marekani, walioniomba nimtafutie Q'uraani, mbongo mmoja aaliyeshikwa na askari wetu bongo na kumkabidhi kwa FBI, sasa na sisi bongo tulimshika yule bwana kwa sababu ni Mu-Isilam?

2. Siku bomu lilipopigwa ubalozi wa Nairobi, FBI waleinda pale unajua askari wa Kenya, walifanya nini bro? Walisubiri siku ya Ijumaaa na kwenda na kukusanya wa-Isialm wote kwenye msikitki ya Nairobi na kuwapeleka kwenye uwanja ambako kwa kushirikiana na FBI, walipwapitia wote na mwisho kuwapata waliokuwa wakiwatafuta, sasa una maana na Kenya nao ni anti-wa-Isilamu?

Hayo maneno yako mengine nia yake ni kupanda mbegu za chuki katika hii jamii, kwa sababu mimi ni Mkrtisto, lakini nilipoombwa kumtafutia Q"ruani huyu kijana mbongo waliyemfunga maisha I never even thought twice kwamba mimi sio Mu-Islam, wazo langu la kwanza lilkuwa ni huyu ni mbongo mwenzangu nikaenda kumtafutia, 75% ya wahsikaji wangu ni Wa-Isilamu sijawahi kuwa na any problem nao, besides, Wa-Marekani wakiamua kuwashika Wa-Isilamu kwa sababu zao binafsi sisi wa-Tanzania inatuhusu nini hasa?

3.
Ingawa ni very tempting kuhukumu jamii kwa makosa ya wachache wa jamii hiyo ina hatari zake. Kudai kuwa solution ya ugaidi, ni waislamu wote waokoke, ni mawazo potofu na ni kuwatukana waislamu, maana kuna magaidi wametoka hata katika hao wanaojiita wameokoka (KKK kiliongozwa na watu wa kanisa n.k., anti-abortion activists, wakina Timothy McVeigh etc etc)! Moja ya sababu iliyomfanya huyu bwana akamatwe na kuteswa ni imani yake. Hilo halikwepeki.

Tusiopenda collective punishment tunaona hiyo sio haki ndiyo maana tunapiga kelele.

Hayo maneno yanaweza kusemwa na watu wenye matatizo ya udini, ndio ninaowasema na wanajulikana na niamini one thing hii ni kwa mara ya kwanza nimeweza kuhtibitisha point yangu ambayo nimekuwa nikiisema kwa muda mrefu sana hapa kuwa kuan watu wanajaribu kutuvuruga na wana sababu moja inayowaunganisha nayo ni udini! Sasa ni zamu ya wananchi wajionee wazii kwa macho yao nilichokuwa nikikisema!

Waswahili walisema siku zote njia ya muongo na mnafiki huwa ni fupi sana, kwa sababu huwa hakumbuki jana alisema nini au alifanya nini, mwishowe hujiweka wazi wenyewe, lakini wa-Tanzania tunazo akili sana za kujua kuwa matatizo ya udini ya USA, sisi bongo hayatuhusu kabisaaa!

Ahsnate Mkuu!
 
1.
Kama waleta dini wanapigana na ugomvi wao wanauleta hadi kwetu (Morris and USA Ambas. bombing etc) si kuwa tayari tumo ndani? Au wataka nini kitokee ujuwe Tanzania haya machafuko ya dini yanaweza siku moja yakawa makubwa?

Wageni wametuletea mambo mengi sana, dini ni moja wapo lakini hatuwezi kutimiza uovu wetu kwa kusingizia kuwa ni dini tulizoletewa na wageni, kwa sababu kama ni kweli dini imetuingia kiasi hicho unachosema kiasi cha kufikia kuhukumiana 'kwa kutmia udini, then how come tuna mafisadi? Ni dini gani tuliyoletewa inayruhusu ufisadi? Au nao ni kwa sababu ya Ukristo na U-Isilamu?

Matatizo ya kupigwa kwa ubalozi wa US bongo, sijui kwa upande wa US, lakini kwetu bongo ilikuwa ni Osama kuu exploit u-umasikini wetu, kwa sababu hakuna mbongo hata mmoja aliyehusika aliyepewa kitabu cha Q'uruani na mabomu tu! Ninajua kwua waliohusika wote walipewa pesa, sasa what dini has to do na this?

Nimeandika ili kuonyesha huu ugomvi wao ulianza wapi. Kutoka hapo ndiyo sasa cha kujiuliza kama VIPORO vya ugomvi wa Wazungu na Waarabu huko Jerusalem miaka hiyo na sasa wajukuu wao, kuna haja kweli ya sisi Watanzania KUUINGILIA? Kumbuka kuna Watanzania walisaidia kutengeneza bomu lililolipua ubalozi wa USA Tanzania na Watanzania wengi wakafa kuliko hata Wamarekani. Laiti wangelijua wanasaidia ugomvi wa watu wasingelifanya hivyo. Kama kuelezea KIINI cha ugomvi wa dini ni KUPANDA MBENGU, inawezekana. Ila mie naona napanda mbengu nzuri tu. Kama Watz walikamata watu wasiohusika huko Uganda, nakubaliana na wewe. Na ukitaka kulaumu usilaumu VITA au Wanajeshi. Tafuta Mzizi wa fitina ulioanzisha hii vita na huo ndiyo UULAUMU. Sijui ni JKN aliyeanzisha vita au Idd Amini. Ukiupata na KUUONYESHA huo mzizi, utaweza kusolve ili mara nyingine lisitokee tena. Ukiujadili huo mzizi "SIDHANI KAMA UNAPANDA MBENGU MBAYA TANZANIA" kwa sababu tu vita na kukamatwa kulitokea Uganda.

Again siioni a point, vita vya kidini vya wazungu na waarabu sisi bongo vinatuhusu nini hasa? Sisi siku zote tunatumika kwa sababu ya umasikini na ujinga wetu, lakini hata siku moja dini haijawahi kuwa sababu ya msingi ya sisi kutumiwa na wageni, unelss kuna something I' missing hapa!
 
Nimesikitika sana, Pole Morris. I am sorry to say that Tz is interested with foregn politics na masifa yasiyo na tija kumbe ni watu wanakuweka sawa ili waje kula kwa mrija kwa visingizio vya foreign investors. Nakuambia miaka ijayo Marekani itakuja kuchimba mafuta hapa Tz na tutalipa fadhila ya mafyeza ya ukimwi, malaria, n.k. Thubutu basi kumwambia Kikwete kupitia mamlaka zake atoe statement kuhusu huyu Morris, atapiga chenga na ikilazimika atoe statement ataitoa kwa Kikwere ili Serikali ya Bush isiielewe. Huku Tanzania serikali yetu haijali wananchi wake na si ya JK tu hata zilizopita, na ndiyo maana tuewapa wahindi nafasi ya ku dominate na kutuona watz mafala tu. Wana JF tuanzie kwanza na tabaka la wahindi, tusiende mbali. Samahani siwachukii wahindi bali ni namna ambavyo wameshatudharau na kwa kuwa wamelelewa na system. Nimeshakuwa India kwa muda kiasi na sikuweza kuona namna ambavyo mtu kama tz atapewa nafasi kule India, hata kama umeoa au kuolewa kule wewe ni outcast tuu. Sasa nako huku TZ wahindi wameshatufanya outcast ndani ya nchi yetu.
 
Sikonge hajakosea. Mbengu zipo. Wako wakristu wanaoamini kuwa haya yote yaliyomkuta ni haki yake maana si wanadini wenzake ndiyo wanaojilipua huko ulaya na marekani? Na kuna waislamu watakaomtetea Morris kwa sababu tu wanaona hii ni ishara nyingine ya chuki ambayo wakristu waliyokuwa nayo dhidi ya waislamu. Ninachojaribu kufanya ni kuwakumbusha kuwa badala ya kuhukumu dini, tuwahukumu watendaji.

Kama tulipoenda Uganda tuliwashika watu kwa vile tu walitokea kabila moja na Idi Amin basi nasi tunastahili lawama. Na hasa kama tuliwatesa na kuendelea kuwashika hata pale tulipogundua kuwa wao hawakushiriki katika maovu ya Idi Amin. Ninavyojua mimi ni kuwa ingawa kweli walikuwepo wakorofi wachache waliofanya tofauti ( kama ninavyosikia walivyo mapolisi wachache Oistabei na kwingineko) lakini hii haikuwa policy yetu kule Uganda. Waganda wangeisha tuanika.

Katika demokrasia ya magharibi kumshika mtu bila kumueleza makosa yake, kumuonyesha ushahidi uliopo dhidi yake na kumpa nafasi ya kujitetea katika mahakama ni ukiukwaji wa haki ya binadamu. Kosa si kumkamata tu Morris bali ni kumtesa na kumshikilia bila kumpa nafasi kujitetea katika mahakama ya wazi! Ndiyo maana wengi wanawalaumu wamarekani maana mwishoni hakuta kuwa na tofauti kati yao na huyo wanayemwita gaidi, ambaye nae anawahukumu watu kwa kutoka tu katika jamii fulani.

Amandla!
Pamoja na maelezo yako yote mazuri. Hapa hata mbali na suala la dini,utagundua hiyo stori ya huyo unaemuita Morris ingawa yeye ni Suleiman, kasimulia yeye tu na hatuna stori ya wamarekani. Je mmepata wapi sababu ya kutoa hukumu kwa wamarekani kwa sababu Huyu Mzanzibari kasimulia?
Tungepata habari za upande wa pili si ajabu hata hii thread ingefungwa.
Nashangaa wengi wametoa hukumu kwa wamarekani wakati katika maelezo yake huyo Morris/Suleiman unaweza kugundua kuna kitu alikuwa akihusika kwa jinsi fulani hata kama anasema hakuwahi kuhusika. Kuna uongo pia ili aonewe huruma.
Mbona hawajakukamata wewe Fundi mchundo? mbona watu wengi hawajakamatwa na wako nje na tena wengine wako Marekani ndani na ni waislamu?
Acheni kuchezea usalama wa nchi za watu kwa kutaka kuleta stori za kuonewa huruma hapa. Kwanza nahisi wamemuachia huru tu kwamba ameshajifunza shida za dunia jinsi zilivyo. Na asidhani ni mwisho, ninaamini yuko under strict watch na may be yeye hajui.
Acheni kutoa hukumu za haraka haraka kwa kutegemea maelezo ya upande mmoja.
Habari ndio hiyo!
 
Nimesikitika sana, Pole Morris. I am sorry to say that Tz is interested with foregn politics na masifa yasiyo na tija kumbe ni watu wanakuweka sawa ili waje kula kwa mrija kwa visingizio vya foreign investors. Nakuambia miaka ijayo Marekani itakuja kuchimba mafuta hapa Tz na tutalipa fadhila ya mafyeza ya ukimwi, malaria, n.k. Thubutu basi kumwambia Kikwete kupitia mamlaka zake atoe statement kuhusu huyu Morris, atapiga chenga na ikilazimika atoe statement ataitoa kwa Kikwere ili Serikali ya Bush isiielewe. Huku Tanzania serikali yetu haijali wananchi wake na si ya JK tu hata zilizopita, na ndiyo maana tuewapa wahindi nafasi ya ku dominate na kutuona watz mafala tu. Wana JF tuanzie kwanza na tabaka la wahindi, tusiende mbali. Samahani siwachukii wahindi bali ni namna ambavyo wameshatudharau na kwa kuwa wamelelewa na system. Nimeshakuwa India kwa muda kiasi na sikuweza kuona namna ambavyo mtu kama tz atapewa nafasi kule India, hata kama umeoa au kuolewa kule wewe ni outcast tuu. Sasa nako huku TZ wahindi wameshatufanya outcast ndani ya nchi yetu.

Mkuu shukrani sana kwa post yako, kwa sababu inagusa exactly where the problem is yaani matatizo yetu ya kisasa, ubinafsi, ujinga kama sio umasikini, yaliyomkuta Morris sio mazuri, lakini mabaharia wamekutana nayo sana toka kwa miaka mingi sana iliyopita,

Mabaharia wengi sana wamekufa kwenye ardhi ya Sudan, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko, ambavyo pia dini was involved, sasa eti serikali itasikia leo, wakati haijawahi hata siku moja kujali haya ya wananchi w ake nje wasiokuwa huko rasmi kiserikali? Kwamba eti victims wa matatizo ya huko nje ni victim wa udini wa huko nje na bongo?

Wakuu kuna wabongo wengi sana wamekufa nje na mpaka leo habari zao haizjulikani, na kuna cases ambazo balozi zetu zilifahamishwa mapema, lakini hakukuwa na response, lakini bado ninasema kuwa dini has nothing to do na haya matatizo!
 
Mi nadhani hapa JF kuna members ambao ni wanasheria nadhani wanaweza kuangalia jinsi gani ya kumshauri huyu Morris atakavyoweza kufugua kesi ili hatimaye alipwe fidia. Kwa kweli licha ya mateso ya kimwili nadhanii hata kisaikolojia atakuwa amepata athari sana ukizingatia kuwa sehemu zote alizopitishwa alipata mateso....Hey!!! Lawyers where are you? Saidia huyu mtu na wanaharakati wa haki za binadamu huu ndio wakati wa kuonyesha uwepo wenu...
 
FMES ! You never cease to amaze me! Uamuzi wa kumtaja au kutomtaja huyo mbaya wako ni wako. Kwangu mimi lilikuwa ni ombi tu kwa vile nilidhani hapa tumesimamia uwazi. Hizi insinuations na innuendos ndizo zinazobomoa badala ya kujenga. Lakini huo ni mtizamo wangu binafsi na sitegemei kuungwa mkono na wote.

Haya, Mkuu! Hao FBI hawakujua wapi pa kuipata Quran hadi wakakutafuta wewe? Au ilihitajika Quran ya kiswahili? Nayo hao mabwana au mabibi kweli hawakuweza kuipata mpaka wakakutafuta wewe? Au kuna jambo unataka kutufahamisha? Excuse my ignorance lakini mimi nilidhani FBI mandate yao inaishia kwenye mipaka ya marekani? Nje ni CIA? Sijasikia FBI wakituhumiwa kuwa na jela au kukamata watu nje ya marekani bali CIA. Lakini, tena, lazima nikiri, huo utaalam sina maana simjui hata mmoja FBI wala CIA. Una ushahidi gani kuwa huyo unayemuita mbongo alikamatwa na serikali ya Tanzania? Halafu unanishutumu mimi kwa kuwa mchonganishi? Nijuavyo mimi wengi wa raia wa Tanzania walikamatwa nje ya Tanzania. Wale waliokuwa Tanzania taratibu zilifuatwa kwa kuomba mahakamani na kama sikosei kuna baadhi ya watuhumiwa walishinda. Mbona kuna mmarekani mweusi mmoja aliyekuwa mwanachama wa Black Panther nae alirudishwa baada ya taratibu kufuatwa? Sasa hayo ya serikali yetu kukamata wanaoshukiwa kwa ugaidi na kuwakabidhi unayasema wewe.

Mimi sichagui. Ninazungumzia dini, ukabila, imani ya uchawi, ubaguzi wa kijinsia, ubaguzi wa rangi kwa vile najua vyote hivi vina nafasi katika jamii yetu. Kuvizungumzia si kupachika mbegu za chuki bali ni kuvitoa vile vinavyozungumziwa gizani na kuvileta kwenye mwanga. Sasa kama wewe unaamini wakina fupi walifanya waliyoyafanya kwa sababu ya pesa tu, hiyo ni imani yako. Kama mambo yote ni pesa tu, huyo Osama anafanya nini huko kwenye mapango wakati anatoka katika ukoo tajiri kupindukia?

Wamarekani wenyewe wanapelekana mahakamani kupinga yale yanayotendeka Guatanamo. Ni wamarekani wenyewe walioijia juu serikali yao waliposema kuwa hakuna Habeas Corpus kwa wale wanaowaita magaidi. Ni wamarekani wenyewe wanaosema kuwa jinsi vita dhidi ya ugaidi ilivyoendeshwa awali imechangia kwa kiasi kikubwa katika kujenga chuki kati ya hizi dini mbili. Hakuna mtu anayewakatalia wamarekani kuchukua hatua dhidi ya wale wenye nia mbaya nao. Kama nilivyosema awali. Tatizo si kukamata. Tatizo ni kutowafikisha mahakamani ambapo wataweza kuhumiwa kufuatana na ushahidi utakaopelekwa.

Kwa vile wengine wakiona Fundi Mchundo mapovu yanawatoka, posting zangu zilikuwa zinaelekezwa kwa watu wenye mawazo kama ya huyu hapa chini.

Bwana mdogo, nakupa pole sana kwa yote yaliyokukuta. najua imekuathiri sana, ila ichukulie kama ni somo/challenge kwako kuhusu namna ya kuishi. kwamba unatakiwa kuishi kwa utaratibu, usiwe unaenda nchi za watu bila utaratibu, kama nchi hizo hazina utaratibu wa visa kama somalia, basi usiende kama ukienda ukubaliane na yote yatakayokupata huko.

kwa upande wangu, najua wamarekani wengine wanaweza kuwa wabaya kama walivyo hata watu wengine, walikutesa/walikuinterrogate ili wapate jibu. sio walikuwa wanakutesa. mazingira waliyokukuta nayo ndiyo yaliyokupelekea kuyapata hayo. kufuga ndevu kama osama si vizuri. kuamini dini anayoamini osama sio vizuri. ndo maana yanawapata hayo. ulishawai kuona wapi mkristo hata mmoja amekamata kwenye huo ugaidi wenu? pateni somo basi, acheni hiyo dini yenu ya ajabu, ndo maana yanawapata hayo. ndo maana watu wanadanganywa vihela hata wakakubali kulipua ubalozo Dar wawauwe hata watz wenzao kwasababu tu ya wamarekani. hii dini ni mbaya, ikimbieni. kama hamkimbii, mnaona yanayowapata?na bado. nashukuru umerudi, wewe kama mtz mwenzangu. lakini kwa wale ambao bado wako kule, naomba Mungu kama hawana makosa warudishwe haraka, ila kama wana makosa, wawanyonge tu, ndo sheria ya kule inavyosema. ugaidi ndo matunda yake.

siamini unachokisema kuhusu nyimbo humo kwenye mashimo, unaonekana unaongea ili watu wawaone wamarekani kwasababu ni wakristo basi dini ya kikristo sio sahihi, inakiri kuwa hakuna mungu kama unavyosema ulisikia. ni shetani tu alikuwa anakutia moyo kumbe anaenda kukunyonga, shukuru Mungu umerudi. ibilisi sio rafiki yako, hayo masauti ulikuwa tu umechanganyikiwa na kifo au mapepo yalikuwa yanakuongelesha wewe rafiki yao, ili uone kama dini ya kikristo wanayomwabudu Mungu ktk kweli ni ya uongo. uislam sio dini sahihi na hawana Mungu kweli, hapo sehemu zingine walisema ukweli. natumaini utabadilisha tabia, ubakie hapa tz ulitumikie taifa, uache kwenda somalia na kushirikiana na magaidi wengine kule kwenye islamic court rebels. sikiaaa!3

Huyu mmisheni mwenzangu ndiye niliyekuwa nampinga. Haya nyinyi mashujaa wa kupinga udini mlikuwa wapi wakati anayasema yote haya? Mmemshupalia Fundi Mchundo kuwa anapandikiza chuki za udini lakini huyu mwenzenu mmemnyamazia! Nyinyi ambao marafiki zenu wengi ni waislamu!

Ignorance is never an excuse.

Nilikuwepo.
 
1.

Wageni wametuletea mambo mengi sana, dini ni moja wapo lakini hatuwezi kutimiza uovu wetu kwa kusingizia kuwa ni dini tulizoletewa na wageni, kwa sababu kama ni kweli dini imetuingia kiasi hicho unachosema kiasi cha kufikia kuhukumiana 'kwa kutmia udini, then how come tuna mafisadi? Ni dini gani tuliyoletewa inayruhusu ufisadi? Au nao ni kwa sababu ya Ukristo na U-Isilamu?

Matatizo ya kupigwa kwa ubalozi wa US bongo, sijui kwa upande wa US, lakini kwetu bongo ilikuwa ni Osama kuu exploit u-umasikini wetu, kwa sababu hakuna mbongo hata mmoja aliyehusika aliyepewa kitabu cha Q'uruani na mabomu tu! Ninajua kwua waliohusika wote walipewa pesa, sasa what dini has to do na this?

Again siioni a point, vita vya kidini vya wazungu na waarabu sisi bongo vinatuhusu nini hasa? Sisi siku zote tunatumika kwa sababu ya umasikini na ujinga wetu, lakini hata siku moja dini haijawahi kuwa sababu ya msingi ya sisi kutumiwa na wageni, unelss kuna something I' missing hapa!

Hayo maneno yako mengine nia yake ni kupanda mbegu za chuki katika hii jamii, kwa sababu mimi ni Mkrtisto, lakini nilipoombwa kumtafutia Q"ruani huyu kijana mbongo waliyemfunga maisha I never even thought twice kwamba mimi sio Mu-Islam, wazo langu la kwanza lilkuwa ni huyu ni mbongo mwenzangu nikaenda kumtafutia, 75% ya wahsikaji wangu ni Wa-Isilamu sijawahi kuwa na any problem nao, besides, Wa-Marekani wakiamua kuwashika Wa-Isilamu kwa sababu zao binafsi sisi wa-Tanzania inatuhusu nini hasa?
FMes,
Kuna jamaa alikuwa na matatizo ya macho. Wakamchukua hadi Space Station na huko akawa anaona watu na magari duniani kwa macho yake bila kutumia chombo chochote. Watu tunapishana. Unapoona wewe inawezekana mie sioni na ninapoona mie wewe huoni. Ni jambo la kawaida kabisa dunia hii.
 
MZANZIBAR ALIYEKAMATWA AU MTANZANIA! miye simo kikwete alisema ukiwa nje nchi ni tanzania lakini ukiwa ndani nchi ni tanganyika na zanzibar, huyu amekamatwa nje nyie mnasema ni mzanzibar badal ya mtanznia? angekamatwa pale kariakoo ni mzanzibar, ukikamatwa kule kibanda maiti unguja wewe ni mtanganyika

miye simo, kwi! kwi!
 
Back
Top Bottom