My opinion: Je serikali ya CCM iko serious kweli au ni kiini macho tu

Hivi SHERIA za nchi hii zinasimamiwa na ccm au Serikali kwa maana ya dola.Unaposema ccm imelishughulikia suala la Mbowe ipasavyo ni sahihi kweli!!?Kweli nimeamini nyoka hawezi kuzaa mjusi mawazo yako sawa sawa Kama ya magamba wenzio wote.

- Serikali ni ya CCM, so CCM is responsible 100% kwa maamuzi yote! Get that!

William @ NYC, USA.
 
William @ New York, kama una mapenzi ya kweli na chama chako basi wasiliana na Nape ili uchukuwe jukumu la kuwafunda vijana wao wanaowatuma kuja kwenye mitandao, badala ya kuja na kujenga hoja na kutetea hoja wao wamekuwa ni mfano mbaya kwa chama chako inaonekana kama ni chama cha misukule.
Wewe binafsi najuwa una uwezo wako binafsi aliokujalia mungu wa kujenga hoja na kuitete na kuleta topic za kichokonozi, ingawa watu wengi wanashindwa kuelewa hasa unasimamia lipi!
Members wengi humu naona huwa wanashindwa pointi of argument na wewe mwishowe ukimbilia kuattack Surname yako. Big up mkuu, kungekuwa na ccm 5 tu humu jamvini wenye uwezo wa midahalo kama wewe jukwaa lingenoga zaidi.

- Thaanks kwa sana mkuu!

William @ NYC, USA.
 
Je, mpango wako wakuanzisha tawi la CCM huko Marekani bado lipo? Au ulitaka kunogesha mjadala hapa jamvini?

- Mkuu hivi nilisema Tarehe mbona inakusumbua sana vipi si unaweza kuanzisha tawi la Chadema! ha! ha! mkuu this wekend tunakutana tena kuanzisha tawi majuu sio mchezo so soon linakuja usiwe na wasi wasi, na karibu sana!

William @ NYC, USA.
 
William,
Kudos for coming in open and expose your face for heavy punching...it is a sign of maturity! On the other hand, CCM bwana mpaka wawe serious, lazima kitu fulani kitokee...nawashukuru sana CCM kwa kuchagua uongozi huu maana weakness zake zimeifanya CCM ijitambue sasa kwa ina gonjwa baya kabisa ambalo ni lazima lipatiwe dawa haraka iwezekanavyo. Angelikuwa ni kiongozi mwingine, angelitumia nguvu na rasilimali nyingi kulinda maovu yaliyotokea na hivyo wananchi kutojua ukubwa wa tatizo la kiungozi ndani ya CCM.

- Heavy punching? Nimechukua nilipokuwa Primary School ile ya live nikishuka tu kwenye gari Shuleni saa za asubuhi, wananfunzi wanarusha abuse, watoto wa wakubwa bwana! mibaba yao mijizi! ha! ha! ha! hizi hapa is nothing! Lakini thaanks thou!

William @ NYC, USA.
 
- Serikali ya Tanzania kwa sasa inaongozwa na kutengenezwa na CCM, kama vile Serikali ya Democrats kule US ilivyomuuua Osama ndivyo wanavyojinadi kwenye kutafuta kura za uongozi na ndio ukweli wenyewe, unajua JF tuna kaazi sana ya kuelemisha jamii!, I mean hata haya mambo madogo hivi!

William @ NYC, USA.

William mbona kana kwamba uraia wako wa Tanzania uliupata kwa kuomba? Majibu ya maswali yote unayo na unayajua, sheria tunazo zipo vitabuni labda jaribu kuwakumbusha wawe wanazisoma kidogo, kama tungekuwa na utawala wa kisheria kashfa zote hizi zinazojitokeza zingekuwapo. CCM haina cha kujinadi kwa wananchi wanachotakiwa ni kujaribu kuondoa kero zinazowakabili watanzania. UTAJINADI VIPI WAKATI MWILI MZIMA UMEJIPAKA MAVI? Mwenyekiti analijua hili fika ndio maana hawezi kufanya mkutano wa hadhara, kimsingi alipaswa kufanya angalau mkutano mmoja wa hadhara si kushinda bali kuwashukuru wanaccm waliompigia kura. Kilichobaki ni kumtuma mtu punguani kama NAPE kufanya mikutano ya hadhara mwenye akili timamu hawezi kusimama mbele ya watanzania kuinadi CCM katika kipindi kama hiki. Kazi ni kubwa kinachotakiwa ni viongozi wetu kuwa wakwel ili kurudisha imani.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Watu wa ajabu kwelikweli

Willium kaongea ukweli ikifikiriwa ni mwanaCCM (UKWELI MWIKO) sasa sijui kwa nini wadau wanaanza kumkwaruza kwa hili na lile.






..................Hamna kitu kama AshaRose Migiro kuwa Rais 2015.......
Hamna lolote la maana alilowahi kulisimamia the same to JK kwa miaka yote
aliyokuwa waziri
 
..................Hamna kitu kama AshaRose Migiro kuwa Rais 2015.......
Hamna lolote la maana alilowahi kulisimamia the same to JK kwa miaka yote
aliyokuwa waziri
 
mkuu hiyo kauli ni mbofu mbofu ina maana unapiga mkwara kwa wewe unailinda sana hii forum bila wewe kusema sio ya CHADEMA basi inakuwa ya CHADEMA?
Kwani wanaopost hapa ndani ni kina nani?
na lini Jamii forum waliomba wanachama wake kuonyesha kadi ya chadema kama sharti la kujiunda na hii forum?
hacheni maneno mbovu mbovu bana, hizi dharahu ndizo zinazowaponza ccm kila kitu chadema, ina maana sisi wananchi hatuna akili za kufikiria mkuu? kama mtu ana amini ujinga ni juu yake hata kama forum ina milikiwa na chadema mbona kila siku tunasoma hapa pumba zako na wewe sio mwana CHADEMA,
AU chadema ni nchi gani? unaongea kama kikwete bana

- Some of us tutaendelea kama kawaida yetu kuihakikishia Dunia kwamba hii sio forums ya Chadema, so pole sana mkuu sio wote tunaofikirishwa kwa mafungu hapa pamoja na kuficha thread na maoni lakini tumetoka mbaali sana na this game, huwa tunasimama pale pale bila kuyumbishwa wala kuogopa, hatuogopi watu maana hoja hujibiwa kwa hoja!

- Sheria ninaijua sana mkuu, ndio maana hata umejitokeza kuja kunijibu! ha! ha! ha!, au? Halafu can you imagine ningewaambia waandishi wa habari kwamba ni kweli nii ni forums ya Chadema, ile siku waliponiuliza? Hapana huwa tunasimamia principle na in the process tunajifunza mengi sana kwamba kuna watu ambao tupo nao ni wa hatari sana kuliko hata hao watawala tunaowapigia kelele! ha! ha1 ha! tunawajua lakini!


William @ NYC, USA.

hao waliokufuata walikuwa influenced na post za hapa ndani, swali ni je hizi post ziko influence na chadema?
jibu liko wazi ni no?
hao wana akili za kimagamba kama walitaka kujua umiliki wa jamii forum walitakiwa kupata ushahidi wa umiliki? nimesikia una share kiasi hapa lakini sio kufikia hatua wewe kuongea pumba zako hapa kwenye forum, hacha mambo ya kitwana una ishusha hadhi forum yakwamba wewe ndiye unaweza kusema nini kina endelea hapa ndani na nani mmiliki wa hii forum?
ina maana wewe ulinunua share kwa ajili ya kufanya umagamba hapa ndani watu wakunyamazie kisa utawambia kwamba utawambia waandishi wa habari inamilikiwa na chadema.
zama za kutishana zimepitwa na wakati kama umefanya kitu kizuri katika jamii isiwe blackmail katika jamii.
sometime u need to shut up man
 
- Serikali ya Tanzania kwa sasa inaongozwa na kutengenezwa na CCM, kama vile Serikali ya Democrats kule US ilivyomuuua Osama ndivyo wanavyojinadi kwenye kutafuta kura za uongozi na ndio ukweli wenyewe, unajua JF tuna kaazi sana ya kuelemisha jamii!, I mean hata haya mambo madogo hivi!

William @ NYC, USA.

wacha bwana! ivi unajua kuwa Osama aliyekuwa kwenye sera ya Obama wakati anagombania urais? Pili, unajua ugaidi ni vita...aka 'war on terror'? Kwenye vita ni nani anachukua credit ya ushindi? Si jemedari mkuu. Kwenye ishu ya Osama, who gave the go ahead on the mission? Si jemedari mkuu aka Obama. Why should he not take credit? Tofautisha Jeshi katika vita na polisi katika kutunza sheria za nchi. Wewe umesoma shule gani mkuu? Mbona unaonekana kama vile huko shule ulikuwa unapitishwa tu? Jeshi na polisi ni vitu tofauti na havifanyi kazi moja. Jifunze hilo kwanza!!! Ndio maana mafunzo yao ni tofauti kabisa. Wewe leo Polisi Marekani wakimkamata Bush kwa wizi tuseme kwenye supermarket, Obama atasifiwa? embu fikiria hilo kwanza. Polisi ni CIVIL SERVANTS. They have/should not have political interest. Kauli yako inaonyesha jinsi gani nyie ccm mlivyoharibu hii nchi. Na inafanya kauli za viongozi wa Chadema waliosema kuwa Polisi wanaupendeleo wa chama kuwa kweli. Huoni kuwa hilo sio sahihi? Jifunze URAIA aise ndugu yangu. Unatia aibu sana!
 
Hivi SHERIA za nchi hii zinasimamiwa na ccm au Serikali kwa maana ya dola.Unaposema ccm imelishughulikia suala la Mbowe ipasavyo ni sahihi kweli!!?Kweli nimeamini nyoka hawezi kuzaa mjusi mawazo yako sawa sawa Kama ya magamba wenzio wote.

umeona jinsi kauli yake ilivyo finyu katika fikra ehhe?
 
halafu mkuu kinachonichosha ni jinsi anavyosifu magamba yao kuwa tangu uhuru wamelinda sheria mara tatu tu, duuh, hii kali kweli kweli.
Zumbemkuu....

Si kweli kwamba CCM wamelinda sheria mara tatu tu, ni ile ufupi wa kumbukumbu na uelewa wa William, na sometimes ni mtu wa kudandia mada nakuleta kama inititator, so expects lots of similar "shody" analyses from William

Nevertheless, CCM ya JK is the weakest CCM in history and unfortunately wanavuana nguo wenyewe kwa wenyewe kama wake wenza!!
 
- Serikali ni ya CCM, so CCM is responsible 100% kwa maamuzi yote! Get that!

William @ NYC, USA.

Duh!!nimekuelewa sasa,kwa hiyo ccm inaweza ikapindisha sheria halafu wananchi tukaishangilia?Tukiwapinga polisi wanaisaidia ccm kutunyamazisha sio?Kazi ipo kwa kweli,bungeni wabunge wa ccm wanapitisha jambo kwa maslahi yao na hatuwezi kupingana nao mfano ktk kikao cha Bunge kilichopita kuhusu MAHAKAMA zetu sote tulijionea yaani kila kitu ni kuburuzwa tu.
 
Zumbemkuu....

Si kweli kwamba CCM wamelinda sheria mara tatu tu, ni ile ufupi wa kumbukumbu na uelewa wa William, na sometimes ni mtu wa kudandia mada nakuleta kama inititator, so expects lots of similar "shody" analyses from William

Nevertheless, CCM ya JK is the weakest CCM in history and unfortunately wanavuana nguo wenyewe kwa wenyewe kama wake wenza!!

Niliogopa kuandika haya! Mtoa mada anazidi kuonyesha uelewa finyu alionao kwenye masuala ya taifa....mkuu unakumbuka wale akina Nalaila Kiula walivyohukumiwa? Mtikila alivyofungwa jela? Niliposoma nikachoka kabisa eti bila aibu mara 3 my footy....
 


- CCM ina alternatives nyingi sana za wagombea wa Urais, kuliko huko upande wa pili Magufuli, Mwandosya, Membe, Sitta, Mwakyembe, hawana wapinzani!

William @ NYC, USA.

CCM, kutokea TANU, ilijengwa na watanzania wote. sisi wote tumeijenga CCM tokea enzi ambapo huwezi kufanya cha maana bila kuwa na kadi ya CCM nchi hii. resource zote za taifa zilitumika kuijenga na kuiimarisha. rejea viwanja vya mpira nk. ambapo CCM imejirithisha baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi. hata hizo kesi ulizotaja ambazo CCM inapata kigugumizi kuzishughulikia "kwa mujibu wa sheria", nyingi zimeifaidia CCM moja kwa moja. vyama vingine vyote vimeanza mwanzo kabisa.

Kuwa CCM ni kama vile unateremka mlima: unaungwa mkono na system iliyopo, na hakuna mtu anakushangaa mtaani. kuwa chama cha upinzani inabidi uwe na uso uliotiwa zege, na baadhi ya watu mtaani mpaka sasa watashangaa kama una akili timamu. huyo Obama uliyemtaja kwamba amepewa support na wamarekani, aliwahi kusema kwamba bibi yake wa kizungu alikuwa bado na mashaka makubwa na watu weusi.

Kwa watu wazima wengi, ambao wamekulia CCM, ni ngumu kidogo kwenda vyama vingine tofauti na CCM. nadhani hii age ya vijana ndio inasaidia sana hivi vyama vingine. hawa hawana "hangover" ya CCM. na ni kutokana na kuwatumia vizuri hawa, inawezekana kuleta mabadiliko. watu kama wewe, baada ya kuishangaa CCM jinsi inavyokuona kama vile ni mwendawazimu, baadae kama na wewe uko serious kweli, utajiuliza hivi unaitendea haki conscience yako kwa kuendelea na chama kama hicho ambacho kina damu mikononi mwake, kina rekodi ya kuiba fedha za wananchi wake, kina baka demokrasia.

utajiuliza hivi ni kwa nini nisiwasaidie alternative party waipe likizo CCM ijirekebishe? that is, kama na wewe hutajali kupandisha mlima - maana ndio kazi utakayokuwa nayo, working with a party other than CCM for now.

So, ni rahisi kutaja majina ya hao unaowasikia katika power sasa hivi, kwamba wanauzika, lakini ambao kwa kweli wanafaidika tu na nafasi ya CCM. from the other parties, you have to earn everything
 
@ Facebook: by William Malecela on Tuesday, June 7, 2011 at 8:36pm

@ NEW YORK CITY-US: Hongera sana Serikali ya CCM kwamba kwa mara ya Tatu toka tupate Uhuru, imeonyesha kuwa ikiamua inaweza kusimamia Sheria bila kujali inamgusa mwananchi au kiongozi wa taifa. Ninasema kwa mara ya Tatu kwa sababu mara ya kwanza ilianza na Balozi Mahalu, halafu Mawaziri Wake Yona na Mramba, na safari hii Mwenyekiti wa Chadema. Kama kawaida siku zote the end of hizi National Legal dramas huwa ni open for debate, na hasa iwapo the end justifies the means, lakini angalau hata kidogo kuliko kutokuwepo kabisaa! Ninasema hivi, kusimamia Sheria za Jamhuri ni lazima kuwepo na gharama na sisi wananchi walipa kodi lazima tuwe tayari kulipia gharama za Serikali yetu kusimamia Katiba ya Jamhuri, ambayo Viongozi wetu wa taifa hukubali kwa kiapo cha vitabu vyetu vitakatifu kwamba bora wafe, kuliko kuona Sheria za Jamhuri zinavunjwa!

- HOWEVER: Serikali ya CCM ifike mahali sasa isituchukulie sisi wananchi kama ni wendawazimu au walevi walevi flani hivi, ambao tunaweza kudanganyika kirahisi sana na viini macho. I mean huu mwendo wa kasi sana uliotumika katika kusimamia Sheria kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwa nini isitumike na kwenye kesi zingine ambazo ushahidi wake wa maovu against sisi wananchi, na kwa Sheria za Jamhuri yetu upo wazi kabisa! I mean upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Ufisadi wa Radar na BAE, tunajua kwamba upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Richmonduli, tunajua sana kwamba upo ushahidi wa wazi kuhusu Dowans na Kagoda, sasa kwa nini huku upande wa pili unaowahusu Viongozi wa CCM Serikali inasua sua na kuwa na makengeza? Hivi ni kweli Serikali ya CCM inaweza kwa macho makavu sana na uso kwa uso kutuambia wananchi kwamba Farijala na Maranda tu ndio waliochota hela za EPA? Yaani kazi yote ile na gharama za kamati ya Mwakyembe na Richimonduli mpaka leo kwa nini hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikishwa kwenye Sheria? Kumbe Serikali ya CCM ikitaka kusimamia Sheria inaweza kutumia hata midege ya Jeshi ambayo tafsiri yake inaweza kuwa Amiri Mkuu Wa Majeshi yetu ndiye Chief Of Our Law Enforcement, kwa hiyo mkono wa kushoto kuusaidia wa kulia sio dhambi, Bravo for that lakini vipi wahalifu sugu huko ndani ya CCM?

- I mean we are taking Serikali ya CCM at its words kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwamba iko serious na kusimamia Sheria za Jamhuri, So! tunasema hivi Charity begins at home sasa ni wakati wa Serikali ya CCM kutuhakikishia wananchi kwamba katika kusimamia Sheria za Jamhuri, hakuna aliye juu yake kwa kuwafikisha kwenye Sheria Viongozi wake wengi wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ile ile iliyovunjwa na Mwenyekiti wa Chadema, mpaka kumbeba na Midege ya Jeshi letu ili akaridhie Sheria Arusha, sasa hii Midege iwabebe na wanaohusika na Radar & BAE, Richmonduli, IPTL, Dowans, Kagoda, EPA, Deep Green, Meremeta, Anabem, Kiwira, ATC na wao tuone wakibebwa na midege ya Jeshi kwenda kwenye Sheria za Jamhuri!: Tunasema hivi sisi wananchi wa Tanzania sio mabwege tena!

Well, People Good Night!

William Malecela @ New York City, USA.
I hope watakuelewa tho i doubt coz wanaimba majukwaani na hatuoni utekelezaji.
 
Ndugu William,

Tatizo kubwa la chama chako cha ccm ni kuona kwamba mtu akivuma ndie anafaa kuwa kiongozi, na hawana utaratibu wa kuandaa viongozi ambao watakuja kutumikia wanchi na sio kutumikia marafiki na historia ya viongozi, na tatizo jingine ni kwamba chama chako kinafikiri viongozi wa Tanzania wamepigwa mihuri usoni na nilazima watoke kwenye kundi lao, hiyo ni tabia mbovu sana, miongoni mwa watanzania wengi wenye upeo anaweza kutokea kiongozi bora kuliko hao unaowafikiria, na hao ndio wamekuwepo miaka nenda miaka rudi bila kuleta maendeleo ya maana kwa mtanzania.

Unachoweza kujivunia ni kwamba mtaji wa ccm ulikuwa ni uelewa mdogo wa watanzania wengi hasa wa vijijini na dar, sasa walio wengi hasa vijijini wameanza kuelewa kumbe kiongozi wa nchi sio lazima atoke ccm, kitu kingine ni kwamba watu wengi walikuwa hawaendi kupiga kura kwa kuwa hawakuamini kama chama kingine kinaweza kushinda hata kama wamekichagua sababu ya dhuruma ya ccm, sasa watakwenda kupiga kura na kulinda kura zao.

Vitu vingine unavyoweza kujivunia ni tume yenu ya uchaguzi, usalama wa taifa na vyombo vyenu vya ulinzi, kwa wenzetu hasa huko USA vyama vyote hupata fursa sawa kutoka hao niliowataja, ila kwa mwelekeo ninavyouona wananchi watakuwa tayari kufa lakini sio ccm kurudi madarakani tena, mimi natembea nchi yetu yote mijini na vijijini watu wanabadilika kwa kasi sana.

Utashuhudia chaguzi kuanzia 2014 na hutaamini utakacho kisikia, wewe kaa huko USA usiote ndoto ya kuja kukuta hatamu za ccm miaka yote, tunafanya babadiliko kwa kasi ya ajabu.
 
William, ni vigumu sana kuukata mkono unaokulisha au kukata mti uliokalia. Inahitaji ujasiri wa uwendawazimu kufanya hivyo. Ufisadi/mafisadi ndo wamemweka mkuu wa nchi kwa hiyo kujaribu kumshawishi awakatilie mbali ni sawa na kumshauri mtu akate mkono wake bila ganzi. JK hana moral authority ya ku-deal na mafisadi wakubwa ndo maana yuko busy na vidagaa
 
Back
Top Bottom