My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

Ndugu hizi ngonjera za mwenyekiti wako zitakusumbua bure ni bora uhame upande kama kweli una nia ya kupigania mabadiliko kama ulivyo mention mwenyewe. Huyu mwenyekiti wenu ni msanii wa hali ya juu kawateua tu vijana wakupiga kelele kama wendawaazimu mtaani kuficha uozo wake na weakness zake siku ziende (si kiongozi makini na ni coward huyu) hana huo ubavu wa kufukuza mtu.

kwanza elewa kuna katiba ya chama ambayo CCM ina ya kwake hapo sijui nguvu za mwenyekiti zinatumika vipi lakini huo huwezo wakuwatoa watu sijui CC or somen hapo ndipo janja yake inapoishia, hila huko mbele mjomba ni mtafaruku wa hali ya juu hata kama kweli anayo hiyo nia.

Kutimuliwa kwa Makamba Snr katika uongozi wa juu CCM usikutishe hile ilikuwa ni kazi ubwete. Raisi kama kiongozi wa chama hanao huwezo huo kichama lakini hana uwezo wa kuchezea katiba ya 'JMT' kiholela olela especially kwa vigogo wenzake waliomzidi maarifa.

Ukisha watoa huko CC bado wanabaki pale pale ni wabunge wa kuchaguliwa katiba inasemaje kuhusu viongozi wa kuchaguliwa na wananchi maana raisi hana haki ya kuvunja mkataba wa wananchi na viongozi wao waliemchagua wao hawawakilishe jimboni (sio enzi za nyerere hizi watu vilaza).

Kibaya zaidi hawa jamaa wanajeuri ya kusema mwenye kuwaona wana hatia hawashitaki mahakamani si ndipo hapo tunapoamua kama kweli kuna makosa, jiulize kwanini hili alifanyiki sasa sijui huyo mwenyekiti anatumia sababu zipi kusema watu wahame iwapo tuhuma zenyewe bado azija thibitishwa kisheria.

Kulalama kwa JF aina maana jamaa wapo guilty, maana hata muuaji hadharani sio guilty mpaka mahakama iamue hivyo. Kama kweli raisi anataka kuvua magamba akaze misuli hawashughulikie kupitia njia sahihi waende mahakamani, waonekane wanamakosa ndio uanze kelele baada ya hapo.

Na kama kweli hao triplets wataenda mahakamani ujue hii aitakuwa kama kesi hizi tulizozizoea za raisi akiamua jamaa wafungwe au wapatikane na hatia inakuwa. Hawa jamaa ni powerful matter of fact ndio waliomweka raisi madarakni and even if the president was to force the issue kuna hatakae baki kwenye ushahidi wa hawa watu si tutafunga mawaziri wote na serikali yenyewe kuko lapse.

Get real 'money' achana na hizi nyimbo za Chama Cha majambazi we hama kambi tu, hawa jamaa atleast wana moral authority ya kukemea lakini CCM ni uozo kuanzia juu mpaka chini na viongozi wote wanaoitumikia serikali ni yale yale tu. Hao jamaa (mapacha watatu) ni scape goats kwenye siasa za CCM ambazo viongozi wana uchu wa madaraka na wivu wa within the party; hila hali halisi CCM ni uozo mtupu huondio ukweli wenyewe.

Hivi we unaamini kabisa CCM itawafukuza wabunge wake kipindi hiki halafu waitishe uchaguzi au uoni momentum ya chadema waende poteza viti kwa upinzani. May be its about time 'slidingroof' explained the meaning of 'game theory' politically, apparently wajumbe wa raisi kwenye kuvua magamba hawalijui hili ndio maana watu wanakurupuka tu na kauli za kujichimbia makaburi.
 
- Ukitaka kumua nyoka unaanzia kichwani kwanza! hawa mapacha watatu ndio hasa kichwa cha nyoka na magambas!

William @ NYC, USA.
Kwa mantiki hiyo JK, Nape, Mukama na wanachama wengine wa CCM ni mwili wa nyoka ambaye anaweza kuotesha magamba. Tumuue nyoka ili asiendelee kutuuma ( utawala mbovu, uwizi wa maili ya umma)
 
Napinga ufisadi kwa nguvu zote! naomba niachie hapo
Sasa twende kazi.

Kuna watu wawili nimetokea kuwahusudu sana Tanzania:mmoja ni Dr Slaa na mwingine ni Lowassa.

Nianze na Dr. Slaa. Huyu ametuonesha kinagaubaga na bila kujali hatma ya maisha yake, mapungufu yaliyopo kwenye governance system yetu; rushwa kubwa (grand corruption), utawala usiozingatia sheria, madhara ya Taifa kutokuwa na miiko ya uongozi, kutowajibika pale kiongozi anapofanya kosa, athari za Taifa kutozingatia vipaumbele katika mipango na utendaji wake, urafiki katika maswala ya uongozi, na kubwa zaidi - viongozi kutoishi wanachokisema.

Nije kwa Lowassa; Huyu mheshimiwa ametuonesha kitu kimoja kikubwa nacho ni; as a nation we are facing a failed leadership, na sasa tuko kama a homeless centre, hakuna wazazi kwa hiyo yatima (watanzania) wanategemea wasamaria wema. Movie ya Lowassa inatuleza kwamba kwa nchi yenye stong leadership wahalifu au watuhimiwa wa uhalifu wanapelekwa mbele ya vyombo vya sheria na SIO mazungumzo. Tanzania tulishuhudia majadiliano na baadae 'grace period' kwa wakwepaji wa EPA. Sasa tunashuhudia tena mazungumzo ya RACHEL.

Assume for example Lowassa anakubali kuondoka kwenye chama baada ya haya mazungumzo, hivi ni kweli atakuwa ameondoka au watakuwa wamekubaliana mechanisms fulani za yeye kuendelea kuwa active ndani ya chama?! Na akiondoka does that mean alimefanya kosa au amevunja sheria ya nchi? Ni sheria gani hiyo atakayokuwa amekiuka? Na ni nani au ni chombo gani chenye mamlaka ya kumtia mtu hatiani? Hivi Lumumba ni sehemu ya kutafsiri sheria?

My wish kwa hawa heros wangu wawili ni haya: Kwamba Dr Slaa ataendelea kutupa mwanga juu ya mdodoro uliopo ndani ya mfumo wa utawala wetu (governance system). Pamoja na hayo nategemea atueleza vinara wakuu wanaodidimiza utawala/usimamizi wa rasilimali za nchi.

And my heor Lowassa asitunyime haki yetu kama raia wa Tanzania - nayo ni kusikia ni kwa jinsi gani amevunja sheria za nchi hii, alikuwa peke yake? na kama alikuwa na mtu/watu ni nani huyo/how? In otherwords, my wish kwa Lowassa ni kwamba atasisitiza sheria ifuate mkondo wake, na kama tujuavyo mbele ya sheria a person is innocent until proven guilty!
 
- baba yangu hahusiki na anything kama huna cha kuchangia kwenye mjadala wa taifa ni bora ukakaa pembeni ukaachia wanaotaka kuelimishana, kama una tatizo na baba yangu wewe ni kumfungulia topic yake! ha! ha! siku njema sana mkuu!

William @ NYC, USA.

William,
kuliwahi kuzuka tetesi kuwa Patel yule mmoja wa wachota hela za EPA alifinance haruc ya mzee wako na hapo ndipo anapohusishwa na yeye kuwa mmoja wa walionufaika na pesa za EPA, je hili unalisemaje, kama ulishawahi kulijibu sio vibaya ukirudia mkuu
 
Hii mbona ipo kwenye katiba ya Chama?....Sehemu ya kwanza,Ibara ya 5,kifungu cha 3.
Sasa kwanini tuwakumbushe kila siku hawa wazee na watoto wao?
Kwanini sisi wanachama wa CCM tusifungue mashtaka mahakama kuu kuhusu ukiukwaji wa katiba ya chama?
Mbona wazee wetu wa Yanga waliwafukuza viongozi wao mwaka 1987? Kwa kuenda kinyume na katiba ya Youg Africans?...na mahakama kuu ikaamuru uchaguzi ufanywe na kuuvunja uongozi?
Sasa mimi na wewe Wiliam tunasubiri nini? kama wamevunja katiba si wafukuzwe uanachama?...Kwanini tuwabembeleze?

Sitambui wala sitatambua AZIMIO LA ZANZIBAR....mwenye nalo anionyeshe hapa jamvini!!
 
William,
kuliwahi kuzuka tetesi kuwa Patel yule mmoja wa wachota hela za EPA alifinance haruc ya mzee wako na hapo ndipo anapohusishwa na yeye kuwa mmoja wa walionufaika na pesa za EPA, je hili unalisemaje, kama ulishawahi kulijibu sio vibaya ukirudia mkuu

Na-hope huko tunakokwenda hatutatakiwa kudhibitisha au kukanusha tuuma za wazazi/ndugu zetu ambao wako hai na wanaweza kujibu shutuma zao wenyewe. Kama tukifanya hivi tutakua tunanyamazisha independent voices. Na vile vile chochote atakachosema William ni wazi very few if not all of us will doubt because of conflict of interest. Naomba pia nitoe angalizo:tusije ku-assume watoto ambao wazazi wao wanaonekana walikua wazalendo wakweli ndio wenye haki yaku-voice their opinions. Uliyeuliza swali unaweza kuwa una-good intentions as I also believe in freedom of speech. Lakini I also believe we should judge people as individuals wanapotoa maoni yao otherwise tutaanza kupoteza mweleko wa thread ikaishia kuwa too personal ambayo haitusaidii kwenye mustakabali wa nchi yetu.
 
Kwa kuongezea Ndugu Unstoppable, nadhani William alitoa maelezo kwa ufahamu wake juu ya hizi tuhuma Mzee dhidi ya mtuhumiwa wa EPA. Na alileza kuwa wakati wa michango ya harusi mmoja wa watu walioleta mchango alikuwa Sophia Simba (correct me I am wrong), na Bi Sophia alileta kama group contribution ambamo ndani yake kulikuwa na mchango huyu mtuhumiwa wa EPA. Kwa hiyo technically Mzee anakuwa mbali kidogo. Hata hivyo ningependa kuamini in fact ninaamini William is his own man. Yes, loves his father and all that na achokisema hapa jamvini in fact kinaweza kutafsiriwa kama kuwa na mtazamo wa mbali kidogo na Mzee? but that goes to show the character of the man! Call a spade a spade!

I hope T.K utakuwa umeridhika walau kidogo na haya majibu na pia inatuonesha kuwa kupita hili jamvi tunaweza kutoa dukuduku zetu wakati huo huo tukapata mawazo kama si majibu ya dukuduku hizo. Tuzidi kushikamana maana taifa linatafunwa! chapa kazi William, chapa kazi T.K.
 
NN unapokuwa rais ni issue nyingine hasa kwa nchi zetu hizi.

Lakini hali imekuwa mbaya kiasi hata mawaziri, makatibu wakuu nao wanaiba zaidi ya alichoiba rais . Kwangu Binafsi bora fisadi awe mmoja tu rais wengine hawaruhusiwi.

Tukimaliza tatizo la ufisadi la mwaziri na watendaji ndo tunahamia kwa hicho cheo amabcho kiko above the law. Alkini hawa kina mkapa, Mwinyi na JK tuwaweke pmbeni tu.

Hakuna utawala wa sheria wa haki unaotaka hivi...FISADI ni fisadi tu awe rais awe mpiga debe na wote wanastahili kupikwa kwenye chombo kimoja..tunaposema hatuwataki mafisadi basi hakuna kuwatazama usoni wote hukumu moja...
 
Hakuna kitu chochote ambacho ni real katika huu upuuzi wa kujivua gamba. Hawa jamaa walitaka kutuuzia mbuzi kwenye gunia wakidhani watanzania bado ni mabwege.

Mikakati anayoipendekeza William ilishapendekezwa siku nyingu tofauti ni wigo tu...kwani walishasema kuwa yeyote aliye kwenye list of shame part I and II anatakiwa kuwa Segerea siku nyingi..

Sasa kati ya wana CCM nani yuko tayari kufungua pandora box ya hizo lists of shame?? Kama yupo basi naomba nitajiwe na akimudu kuifanya hio kazi basi nidaiwe kulipa faini yoyote ile (isipokuwa mke wangu na watoto)!!
 
Willy,
Mkuu wangu shukran sana kwa kuweka ukweli huu ambao hauna ushabiki labda tu mtu apende kushabikia..Sisi wote hapa tunaomba hawa mapacha watiwe ndani kama walivyotangulia kina Yona na Mramba kwani tuna ushahidi mkubwa zaidi dhidi yao na mahla pekee panapoweza kuthibitisha kwamba wao ni innocent/Guilty ni mahakamani na as long as they are presumed innocent hakuna sheria inayokataza kukamatwa kwao.Hatuwezi kukataa ukweli huu kwa sababu ati kuna Mafisadi wengi CCM ama nchini kwani kama ingekuwa hivyo tusinge wakamata hata wezi maanake wapo wengi.

Nakumbuka wakati JK anaingia madarakani alisafisha Polisi na kukamata majambazi kiasi kwamba tuliweza kusafiri, kulala na kutembea kwa amani ingawa sii majambazi wote walokamatwa isipokuwa ilitoa onyo kali kwa majambazi. Na katika majambazi hao wapo walioshinda kesi zao na wengine kupelekwa lupango ndivyo sheria inavyo operate.

Na hata walipokamatwa Yona na Mramba, mkuu wangu rushwa iliogopwa kama ukimwi na kwa mara ya kwanza ilikuwa ukienda ofisi za serikali utahudumiwa haraka na bila kutoa rushwa. Lakini pamoja na yote haya hivi vilikuwa vita vya Titans, kumbe ilikuwa kugombea nafasi za Kufisadi lakini toka Lowassa ameondolewa madarakani serikali ya JK imekwenda likizo, yaonyesha JK hawezi kuongoza pasipo Lowassa na mtandao. Serikali hii imekuwa sii ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo Ujambazi na Ufisadi umerudi tena kwa kasi baada ya serikali kwenda rikizo.
CCM na JK kama kweli mnataka kujuvua magamba kukomesha Ufisadi basi ile ile dawa ya Lowassa na Sokoine itumike kupambana na Ufisadi kwani inawezekana. Sumu ya nyoka pia ni snake venom antidote!
 
Ni kweli mkuu ila naamini kwamba mambo mazito kama tunayoyatamani yanafanywa ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye msimamo usioyumba. Pia ambaye si mhusika wa jinao inayoongelewa.

Kwa serikali ya sasa na CCM nzima tunaye kiongozi wa namna hiyo????
 
Mkuu Willy,
Nakupongeza kwa ujasiri wako wa kusema, ingawa sina uhakika kama sauti yako itasikilizwa. CCM imefika njia panda. Inabidi ifanye uamuzi wa kuchagua kusuka au kunyoa. Kuwafukuza mapacha watatu ni uamuzi mzito sana ambao unahitaji ujasiri kama wa kichaa kuutekeleza; ingawa ndo uamuzi wa mhimu kuuchukua ili kuanza kurejesha imani kwa wananchi.
Kutokuwafukuza ni mhimu kwa mshikamano wa chama, lakini ni uamuzi ambao utakigharimu sana chama. Kitaendelea kuchukiwa na wananchi, na matokeo yake ni km ulivyosema, come 2015 kitapigwa chini.
Uamuzi ni wao, kusuka au kunyoa. Thanks for daring to say it openly.
 
William,

..na ufisadi uliotumika kumuingiza JK madarakani unaushughulikia namna gani?

..JK,Lowassa,na Rostam, wameunda mtandao ambao ni chama ndani chama[ccm].

..katika kufanya hivyo wametumia fedha chafu, mbinu chafu na fitina dhidi ya wenzao ndani ya CCM, rushwa na hongo ktk uchaguzi n.k n.k.

..haya mambo mlitakiwa myashughulikie tangu mwaka 1995 lakini hamkufanya hivyo. kuyashughulikia sasa hivi wakati mtandao wameshashika chama ndiko kunakusababisha muwe na kigugumizi.

..UGUMU WA KUWAFUKUZA LOWASSA NA ROSTAM NI KWAMBA MWENYEKITI NAYE NI MDAU KTK UFISADI MWINGI WALIOUFANYA.

NB:

..na kile kitendo cha Mwenyekiti wa Chama kuwapigia kampeni za waziwazi hivi hakistahili hata kutolewa karipio?

..hivi kitendo kile siyo dalili za wazi kwamba Mwenyekiti anawaunga mkono mafisadi?

..let me explain: Takukuru iko chini ya Ofisi ya Raisi. Sophia alikuwa waziri wa nchi Utawala Bora. Kwa msingi kisheria Waziri wa Utawala Bora, and particularly Takukuru, ni Raisi. sasa Raisi alipokuwa anawapigia kampeni watu wanaoshitakiwa na Takukuru kweli mnamuelewa. Halafu Takukuru ni chombo cha ulinzi na usalama, na Raisi ndiye amiri jeshi mkuu.

..sasa JK siyo kama haelewi uzito wa Amiri Jeshi Mkuu kufanya kitendo kama kile dhidi ya askari wake walio ktk medani ya kupambana na Rushwa. JK amepitia mafunzo ya kijeshi, ni senior commander mstaafu mwenye cheo cha Luteni Kanali.

- Mkuu kuna hoja nzito umeztioa, lakini pia kuna hoja dhaifu sana kama ya pesa za kampeni kuwa chafu, no that is out of the line, Tanzania htuna sheria za ku-control pesa za kampeni, vyama vyote vimetumia pesa chafu if it is the case, Rais anapopiga kampeni anapangiwa na wasaidizi wake, pamoja na yote CCM haikuwa imejitayarisha kuyapoteza hayo majimbo, ndio maana Rais alienda!

- Lakini ninakubaliana na wewe kwamba Rais alikosea sana kwenda kwenye majimbo ya Chenge, Lowassa, rostam na Mramba, it was wrong na wala halina mjadala!

William @ NYC, USA.
 
Nafikiri Willie ama unakebehi watu ama haujaielewa CCM....kwanza nikuulize mafisadi CCM ni hao watatu tu?..Well kama una uvivu wa kuujua ama kuutafuta ukweli,ama kama umetekwa na cover la kitabu cha kujivua gamba unaweza sema ndio...CCM kamwe haiwezi kuwafukuza mafisadi hao watatu wala wale wengine,maana ukweli ufisadi hawakuufanya wao peke yao..ufisadi ulifanywa na CCM kwa manufaa ya CCM ili waendelee kuinyonya asali ya Tanzania..Kifupi Ufisadi na CCM havitengamani...sinema hii wanayoicheza CCM mimi nafananisha na mtandao wa maambukizi ya Ukimwi katika jamii fulani au kundi fulani then ikaamuliwa watatu wenye ukimwi wauae ili kuzuia maambukizi zaidi,wakati walioambukizwa ni 50..sasa ukiua watatu hawa 47 hawataendelea kuwaambukiza walio bado?.. Willie baba kuwa CCM siyo kigezo cha wewe kijana mwenye ufahamu kukumbatia CCM na mabaya yake....Taifa la kesho si CCM,amka sasa na acha kuendekeza magamba jiunge na CHADEMA kulikomboa Taifa...na bahati mbaya mzee wako naye anatajwa kuhusika na ufisadi...sorry for that lakini si lazima na wewe uunywe ufisadi eti kwa sababu mzee ni wale wale...Welcome CHADEMA!!

- Niwe mkweli tu kwamba hilo halitakuja kutokea hata siku moja!, lakini ahsante sana kwa ukaribisho!

William @ NYC, USA.
 
Heshima kwako W J Malecela.

Mkuu wangu niliwahi kukupa tahadhari kipindi fulani ulianzisha thread yako ya kushangilia kujivua gamba CCM nikakuonya hukutaka kusikia kabisa ukajiaminisha na kuwaamisha baadhi ya watu wenye mioyo ya kuku kwamba CCM itajivua gamba! .Nakumbuka nilikupa sababu kadhaa lakini moja kubwa ni kukosa msimamo kwa mwenyekiti wenu Rais J M Kikwete.Kama umefuatilia sakata zima lilivyoripotiwa na baadhi ya magazeti ya Raia Mwema ,Mwanahalisi na baadae kuthibitishwa na Mwananchi utagundua jambo moja muhimu sana "ukosefu wa msimamo madhubuti wa Mwenyekiti wa CCM taifa". Mwenyekiti wenu bado hajaonyesha msimamo wa kuchukia ufisadi na washiriki wa ufisadi kwa dhati,Washirika wakuu wa ufisadi walimsaidia sana kufika hapo alipo bado anawaonea aibu hata ingekuwa ni wewe ingekupa shida[dhambi ya kushirikiana na waovu].

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari Rais Kikwete alikutana na Lowassa kabla hajakutana na Mzee Msekwa.Mazungumzo baina ya Rais na Lowassa yaelekea hayakugusia kabisa suala la Lowassa kujivua gamba hata kama yaligusia huko yaelekea kabisa Lowasaa aliweza kupangua hoja zote kwa ukamilifu kabisa tofauti na alivyoshindwa kupangua hoja wakati Mheshimiwa Dr Mwakyembe alipowasilisha hoja za RICHIMOND mjengoni [ni siri baina yao].Yamkini yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida sana pengine Lowasa alimkumbusha Rais Kikwete jinsi alivyomsaidia hadi akaukwa urais wa JMT,jinsi alivyoratibu ukusanyaji wa fedha hadi kufikia kukwapua fedha kibao Benki Kuu [BOT],jinsi alivyopambana na wapinzani wake waliokuwa wakitishia nafasi yake pengine alimwambia Kikwete unakumbuka tulivyompakazia Salimu A Salimu kwamba alihusika na mauaji ya Sheikh A Karume kwamba yeye ni HIZBU,unakumbuka tulivyonunua vyombo vya habari na nk.Baada ya siku kadhaa Lowasa anaitwa na makamu mweyekiti Mzee Msekwa na kuambiwa mambo ya ajabu eti ajivue gamba mara ohooo achana na ndoto za urais hata kama ni wewe lazima ushangae iweje mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa chama ashindwe kukuambia msimamo wa chama amwachie jukumu hilo Mzee Msekwa !.Mkuu wangu W J M wewe nimtu mzima sana hakuna ubishi kwamba Mwenyekiti wako akiwa na Lowasa anazungumza masuala tofauti na akiwa na Makamu Mwenyekiti wake.Kauli za katibu wa Itikadi Bwana Nape na Katibu Mkuu Bwana Mukama zilitosha kabisa kukupa ujumbe kwamba kujivua gamba ni aina ya maigizo yasiyokuwa na mwongozaji,kila mmoja anaamua namna ya kuigiza apendavyo.

TANU/CCM chini ya uongozi madhubuti Mwl J K Nyerere iliwahi kujivua gamba mara kadhaa na wananchi wa kawaida wakalishuhudia kwa macho yao tofauti na huu usanii wa sasa.Mwaka 1967 TANU baba wa CCM ilijivua gamba kwa kuanzisha Azimio la Arusha[Miiko ya uongozi iliasisiwa na hili azimio].Mwaka 1984 CCM ilijivua gamba kwa kumwondosha aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.Mwaka 1987 CCM ilijivua gamba kilipobaini vyombo vya serekali na taasisi za kiuchumi zilikuwa zimeshindwa kuwahudumia watanzania ipasavyo,Mawaziri na wakuu wa mashirika ya umma kama ATC,NASACO na TIB walikwenda na maji.

CCM chini ya uongozi lege lege haiwezi kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa.

Mkuu W J Malecela ni wakati wako wa kufanya maamuzi sahihi sasa kwakuwa naamini wewe ni mtu mzima umeona mengi si vibaya ukaachana na CCM ukaelekeza nguvu zako sehemu nyingine.Muasisi wa CCM Mwl Nyerere aliwahi kutamka hadharani kwamba CCM si Mama wala Baba yake baada ya kuchoshwa na uoza usiokwisha ndani ya chama alichokianzisha[kadi namba moja hadi leo hajapewa mwanachama mwingine bado anaendelea kuimiliki hata kama ameshatangulia mbele ya haki].Najua ni uamuzi mgumu sana kwako hasa ukizingatia umekulia huko,umekuzwa huko na sehemu ya mafaniko yako yameanzia huko ni wakati wako sasa kuachana na siasa za udanganyifu dunia ya leo watu wanataka haki,wanataka kumiliki uchumi wao katika hali ya usawa umeona mwenyewe yaliyotokea na yanayotokea Mashariki ya kati.

- Wakuu naomba sana tujadili mengine lakini ya mimi kukimbia chama changu CCM halipo, isipokuwa kinahitaji sana msaada wangu kuki-reform na Revolution yaani Mapinduzi!

William @ NYC, USA.
 
William, do you think matatizo ya nchi yetu yametokana na mapacha watatu? Kwa maneno mengine, unadhani kwamba gamba la CCM na serikali ni mapacha watatu au Kikwete mwenyewe? Hawa mapacha watatu hawana madaraka yoyote makubwa serikalini yanayoweza kuathiri utendaji wa serikali. Cha ajabu hali ya nchi na maisha ya watanzania yanazidi kuwa magumu na yenye kukatisha tamaa.

Je mapacha watatu wana influence gani kwenye ugumu wa maisha ya watanzania kwa sasa? Labda ninaweza kusema Rostam ana impact kiasi fulani kutokana na kushikiria njia kuu za uchumi wa nchi. Lakini the rest, sioni kama wana madhara makubwa sana kwa nchi. Otherwise gamba kuu na gumu kwa CCM na serikali kwa ujumla wake ni Kikwete. Kushindwa kwa CCM na kushindwa kwa serikali hakujasababishwa na mapacha watatu, bali Kikwete. Mimi na wanaCCM wengine tunatakiwa tuache unafiki na tusema wazi kwamba gamba letu kuu ni Kikwete, tufanye kama ANC tumuombe ajiuzulu kama alivyofanya Mbeki. Uwezo huo kama wanaCCM tunao, lakini tatizo kubwa linalotusumbua ni unafiki. Tunakazana tu kuwataja akina Lowassa kwa kuwa hawana impact kwetu tunaacha kumtaja Kikwete kwa kuwa ameshika lungu na tunaogopa makali ya upanga wake.

Tuwe wawazi katika hoja zetu tuache unafiki, Kikwete ndiye aliyeshindwa kuendesha nchi na ndiye aliyeshindwa kusimamia misingi ya utawala bora na wa sheria.

- Wakuu please naomba sana tujadili hoja niliyoileta mezani, Rais wa sasa anamaliza muda wake soon na bado mpaka leo sijafikia hatua ya kuamini kwamba anahusika na ufisadi wa aina yoyote, so naomba tujadili hoja ya mezani kwanza!

William @ NYC, USA.
 
Naomba ninukuu sehemu ya tano ya "Azimio la Arusha na siasa ya TANU ya Ujamaa na Kujitegemea" iliyotolewa na Idara ya Habari ya TANU,1967.

SEHEMU YA TANO

AZIMIO LA ARUSHA

Kwa hiyo basi,Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka 29/1/67,inaazimia ifuatavyo:-

A. VIONGOZI

1.Kiongozi wa TANU au wa serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lolote la kibepari au kikabaila.

2.Asiwe na hisa katika makampuni yoyote.

3.Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4.Asiwe na mishahara miwili au zaidi.

5.Asiwe na nyumba ya kupangisha.

6.Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa,Mawaziri,wabunge,wakuu wa vyama vilivyoshirikishwa na TANU,Wakuu wa mashirika ya kiserikali.Viongozi kutokana na kifungu chochote cha katiba ya TANU,madiwani,na watumishi wa serikali wenye vyeo vya kati na vya juu.(Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).

B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE

3.Inahimiza serikali kutengeneza mipango yake kwa kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za ng'ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano.Halmashauri kuu ya Taifa inaazimia mpango huo urekesishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.

5.Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.
Mwisho wa kunukuu.

Kuthibitisha kuwa azimio la arusha ni moja ya nguzo za katiba ya CCM,tuangalie katiba ya CCM section 1,5(3):-
"To promote the building of Socialism and self reliance on the basis of the Arusha Declaration".

MY OPINION:
Katiba ya CCM imeonyesha wazi ni watu wa aina gani wanatakiwa wawe viongozi wa chama na serikali,sehemu ya kwanza ibara ya 5,kuanzia kifungu cha 3 na kuendelea vinaonyesha bayana kuwa uongozi uliokuwepo haufuati katiba na kanuni za chama na tukiungana wanachama tunaweza kuwapeleka mahakama kuu, ku question na ultimately dissolve their leadership based on contitutionality.
NAWASILISHA!

Mkuu Kobello, CCM ya sasa hakuna katiba! Naomba ufahamu hivyo ni bora liende tu!.....Sasa hivi wanashindana nani atakuwa na mabilioni mengi kuliko mwingine na hii ndio inasababisha mikataba ya kifisadi au manunuzi ya kifisadi kuendelea kuwepo hata leo hii pamoja na Watanzania wengi kupigia kelele ufisadi na kusababisha nchi kuendelea kwenda mrama.

Kiongozi tuliye naye anajua wenzie wanazijua dhambi zake na ndio maana anashindwa kutumia uwezo mkubwa aliokuwa nao kama Rais wa nchi na hii inasababisha nchi kuendelea kuangamia na Watanzania wengi kupoteza imani na Viongozi waliokuwepo madarakani.

Kama kanuni ulizoandika hapo juu zingekuwa bado zinafuatwa basi kelele hizi tunazozipiga kila kukicha labda zingekuwa hazipo au zingekuwa chache sana.
 
...CCM sasa hivi ni kama vile haina viongozi imara wa kuweza kutoa maelekezo/amri na kusikilizwa mara moja -- chama kimebakia kubembelezana katika masuala yoote!!
Zak Malang, unasema CCM ni kama vile haina viongozi imara..., naomba kukuuliza, unaposema ni kama vile haina, unamaanisha wapo, kama wapo, wataje ni wepi?. Kwa maoni yangu, ondoa neno 'ni kama', lililobaki ndilo jibu halisi kuhusu CCM sasa!.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom