My happy ending story

mimi nina ya mshkaji wangu, alikuwa anampenda kweli binti na akawa amepanga kumfanyia surprise ya kumvisha pete ya uchumba. Yaani jamaa alikuwa ameshadhamiria kumwoa binti. Siku ya siku ikafika jamaa kajiandaa na surprise yake tupo tunamngojea binti aje, basi ile kufika yupo na rafiki yake kumbe binti naye ndo alikuwa amepanga kumwaga jamaa siku hiyo....

Jamaa akaitwa pembeni, binti akamwambia bwana samahani ila inabidi nikueleze; kuna bwana nimempata na naona kuwa tunaendana naye zaidi na ameomba kunioa na mimi nimemkubalia, ila naomba tuendelee kuwa marafiki na tuwe tunasaidiana kama kaka na dada. Jamaa karibia azimie, kama jitihada za makusudi hazikufanyika....

Baada ya hapo binti akaolewa na bwana chaguo lake na rafiki yangu mungu si athumani akapata mke (tena yule rafiki yake binti aliyekuja naye siku ile) jamaa amebahatika kupata mapacha wawili na binti naye mungu kamjalia kabinti na muda si mrefu anategemea kupata kitoto kingine cha kiume. Mpaka leo wanaendelea na maisha vizuri kabisa na ni family friends na binti amemtambulisha jamaa kwa mumewe kama kaka yake na wanaheshimiana na kushirikiana utafikiri watoto mapacha vile. Kinachonifurahisha zaidi, jamaa ndiye mshauri mkuu kwenye ndoa yao, na binti halikadhalika amebeba jukumu la kuishauri familia ya jamaa yangu kwa maana anawajua wote vizuri.

hallo , yani hapa umenitoa. Nikifikia maandalizi ambayo hufanyika katika vitu kama hivi halafu ghafla kitu kinamwagika. Lakini uzalendo kama huu ndoo safi. Mungu abariki familia hizi kama kweli zipo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom