My great loss

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Ndio kwanza nimerejea kutoka Nachingwea kumzika mama yangu aliyefariki Jumamosi iliyopita.

Niliwafahamisha wachache hapa kwa sms lakini nilishindwa kuwajuza wengi kupitia jukwaa kwa sababu ya ghafla ya jambo lenyewe kwani nililazimika kuondoka Jumamosi mchana mara baada ya kupata taarifa za msiba ili niwahi mazishi Jumapili.

Nashukuru niliweza kudrive usiku na kufika salama na kuwahi mazishi na nimerejea jijini salama
 
Goooosh, WHAT A LOSS!1...Pole mkuu sana!...KIBINADAMU HAYO NDO MANENO PEKEE TUNAYOWEZA KUKWAMBIA, HATUNA FARAJA ZA ZAIDI!...Bali Mungu wa Mbinguni ndiye atakayewafariji kwa upole zaidi na kuondoa upweke na hasara mliyopata!...Mwogopeni Mungu sana, na mzidi kutafuta sana siri ya ukuu wake...AMEN
 
SORRY FOR THE LOSS MP!!!

Dah aisee....Mungu amrehemu mama yako mpendwa!!!
 
OMG! Am speechless! Pole sana MN!

May the Almighty God Rest Her Soul In Peace! Amen
 
Pole sana kamanda! Mungu aliyekupa Mama akupendae, amempenda zaidi, May her soal rest in Peace.
 
pole sana mpiganaji, kama jina lako linavyosema "MPITA NJIA" kwa hakika sote ni wapita njia.
 
Pole sana Mpita njia mwenyezi mungu awape faraja na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wenu
Amen .
 
Mpita Njia pole sana kwa msiba na mshukuru Mungu sana kwa ujasiri ulioko nao wa kuweza kuendesha gari usiku mzima na uko kwenye majonzi makubwa ya kuondokewa na mama yetu kipenzi. Naamini Mungu atakuwa amempunzisha kwa amani.
 
Pole sana Mpita njia. Kuondokewa na mama ni moja ya misiba inayouma sana. Mungu ampumzishe mahala pema peponi.
 
Pole sana Mpita njia.........Mungu ailaze Roho ya mama mahali pema peponi....Apumzike kwa amani...Amina
 
May Lord shower his blessings upon your entire family during these sad and emotional moments. Hakika yote ni mambo ya Muumba, na hayana makosa.
 
Pole sana mkuu! hapa inabidi ujipe moyo kufiwa kusikie tuu kwa mwenzio kuondokewa na mama jamani ni pigo kubwa sana jipe moyo endelea kumuombea mama alale pema peponi! tuko pamoja katika kipindi hiki cha majonzi mungu akupe faraja mkuu pole sana!

Najua hali uliyonayo sasa hivi ila jipe moyo utayashinda yote katika yeye atutiaye nguvu Amen
 
Pole sana Mpita Njia, Mungu akupe nguvu wewe na familia yako katika hiki kipindi kigumu. Mungu amlaze mahali pema peponi Mama Mpendwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom