klorokwini
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 8,648
- 5,139
hii story imenishangaza kitu kimoja, hivi huyo mume wako wewe kipindi chote hicho ameruhusu hiyo boundless friendship yako wewe na hilo jibaba? yaani unaletewa vizawadi na mnaonana kila siku? usiku unampigia akuje kukusaidia, khaaaa! nazani hii ndoa yako inahitaji msaada kabla hii ndoa ya rafiki yako.Mimi nina best frend wangu sanasana ni mwanaume na mimi ni mwanamke. ni rafiki yangu wa siku nyingi kiasi kwamba ndugu zangu wote wanamjua na mume wangu anamjua na wanapatana sana sometime tunatoka wote out sometimes tunafanya nyama choma kwake au kwangu tunaita rafiki zetu wengine tunakunywa pombe na kufurahi pamoja.
Kwa urafiki huo utakuta kila anachofanya lazima ataniambia, akiwa na mwanamke mpya ataniambia akiwa anataka kununua kiwanja tutaenda wote nimpe ushauri akitaka kubadili gari lazima atanishirikisha hata picha atanitumia nione ili nimshauri kama ni zuri au baya. Ikiwa bday yangu ni yeye atakumbuka na kuniletea zawadi hata kama mume amesahau, na sikukuu zingine pia, akisafiri lazima aje na zawadi yangu pia.
Kwa urafiki wetu ulivyo hata nikipata tatizo labda usiku nimeharibikiwa na gari nitampigia yeye simu aje kunisaidia, nikiwa na matatizo na mume wangu yanayosumulika huwa namwambia anipe ushauri, hata kuna kipindi tuko safarini mtoto aliumwa ni yeye tulimuomba ampeleke hospital. naeleza yote haya ili muelewe ni rafiki wa aina gani ili iwe rahisi kunishauri badae.
Rafiki yangu huyu ni playboy fulani hivi anapenda sana wanawake ,kila mara ana dem mpya nimempigia kelele sana mpaka mwaka juzi nikamuunganisha na msichana mmoja hivi,alikuwa nje kimasomo ni ndugu wa rafiki yangu mwingine, badae mwaka jana wakafunga ndoa. yule dem alikuwa ananipenda sana wakigombana nitawasuluhisha na mambo mengine.
Tatizo lililojitokeza sasa hivi mwanamke ananichukia sana nahisi ni sababu rafiki yangu ananijali sana kiasi hata mimi mwenyewe ningekuwa mke wa rafiki yangu ningesikia kawivu flani hivi. Sasa rafiki yangu kanambia wanagombana sana na mkewe kuhusu mimi kwa nini nilimtafutia mke ambae haelewi uhusiano wetu?Kanambia anampenda sana mkewe ila pia ana value urafiki wetu cause tupo kama ndugu.
Pia Kanambia nimwite nimueleweshe sasa mnafikiri nikimwita atanielewa? na nikimwita nimwambie nini? ni vizuri nimwite nikiwa na mume wangu? Mimi nimemwambia rafiki ndoa yake ni muhimu zaidi kuliko mimi rafiki tuwe tunaonana kwenye mambo ya muhimu kama sherehe msiba na kadhalika mnafikiri huu ushauri ni mzuri? Naomba ushauri wanajamvi am about to loose my very best friend
naomba kuwakilisha