Mwongozo wa JF: What should start Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba?

Entrepreneur na WildCard mmenena na kunifurahisha. RA anatakiwa apewe hoja zenu ili ajue anatakiwa kufanya nini na sio kutuchezea shele. Inaonyesha ni mbunge na hajui hata misingi inayosimamia ubunge wenyewe. Iweje mbunge usijue unatakiwa upatikane vipi, na uache vipi? RA hovyo kabisa - ati Nimemwandikia Mwenyekiti, Aibu!
 
Tume ya uchaguzi bado haijawa huru. ndo maana moja ya mapendekezo ya katiba mpya ni kuifanya iwe huru. kwailivyo sasa tutegemee mabo yatendeke kama ilivyo zoeleka
 
Wanajamvi hebu tujikumbushe hizi ibara za katiba yetuili tujue kinachotokea

Ibara ya 76
.- (1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.
(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge (ikiwepo kujiuzulu-msisitizo ni wa kwangu)

Ibara ya 149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:… (d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kjiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika …"

Sasa kinachosubiriwa hapo ndiyo hiyo taarifa ya kujiuzulu, ili Speaker aitaarifu tume

Mkuu umenena vyema na umetoa fundisho. Kwa hiyo spoka hawezi kukurupuka na kutangaza kwamba kiti kiko wazi hadi utaratibu ufuatwe
 
Hadi sasa RA ni mbunge halali wa jimbo la Igunga hadi hapo taarifa ya maandishi itakapomfikia spika. Tusishangae RA kukana kujiuzulu na kurejea bungeni kwa kishindo huku akisindikizwa na wale waliozimia, hii ndiyo TZ.
 
Bila kujali matokeo ya uchaguzi Igunga yatakuwaje sasa umefika wakati Watanzania wakaelewa maana halisi ya demokrasia ya vyama vingi. Najua CDM kwa upande wa bara wamejitahidi sana kuelimisha umma na mwitikio ni mkubwa lakini mabadiliko hayatakuja kirahisi kwa tume hii ya uchaguzi tuliyo nayo.

Na ninapozungumzia tume ni kwamba hili ni suala la katiba kwa hiyo muswada wa katiba ndio swala la msingi baada ya uchaguzi wa Igunga. Katika hili kila Mtanzania anatakiwa kuwa makini kwa sababu likifanyika kosa lolote katika katiba basi maumivu yataendelea kwa muda mrefu ujao. Igunga itakuja na matokeo yake pamoja na malalamiko kama vile ucheleweshaji wa matokeo lakini amini usiamini vita kamili ipo katika kuandika katiba mpya.

Siku zote anayefaidika kwa sheri mbovu iliyopo hawezi kukubali kubadilishwa kwa sheria hiyo. Watanzania tujiandae
 
mimi pia nafikiri tume huru ya uchaguzi ndio mwarubaini pekee wa hiki kiini macho kinachotokea kwenye chaguzi zetu.
 
yaaaani achaaa tuu itabidi iundwe tume huru na yenye haki sawa....wasipoangilia tutaingia barabaran kudai tume huruuuuu...!
 
Tume inaturudishaaaa nyumaaa,tume ndo inaleta vurugu,tume ya uchaguzi ndo inayoleta umwagikaji wa damu,tume ya uchaguzi ndiyo inayo ibeba CCM NA KUHALALISHA UCHAKACHUAJI WA KURA,WIZI WA KURA NI SAWA NA WIZI WA HAKI....MBONA CCM WAKIWA WAMESHINDA WANATANGANZA UPESI NA FASTA FASTA,ILA CDM WAKIWA NA DALILI ZAUSHINDI UCHELEWESHAJI WA UTANGAZAJI MATOKEO
 
acha unafiki wewe um eshona mmeshindwa uchaguzi unaleta lawama kwa tume kwa kosa lipi.kubali matokeo kenge wewe.
 
Ili kuwaondoa Magamba kwenye nchi yetu basi hakuna budi sisi Watanzania kuulilia mchakato wa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Kwa sababu tume iliyokuwapo ni Mtaji wa Magamba na wengi wanaofanyakazi kwenye hizo tume wmechaguliwa na M/kiti wa Magamba Ndugu Fisadi Kikwete a.ka Zee la Anga au Vasco Da Gama Pori
 
acha unafiki wewe um eshona mmeshindwa uchaguzi unaleta lawama kwa tume kwa kosa lipi.kubali matokeo kenge wewe.
We umekuja juzi tu hapa JF na unaanza kuporomosha matushi namna hii? Great Thinkers hawaropoki hovyo, ila kama umetumwa tekeleza lililokuleta then upotee,ili wabaki GT wa Ukweli,Tabia mbaya sana hiyo!
 
ni kweli bila tume HURU ya uchaguzi tutaendelea kuangamiza demokrasia na maendeleko ya nchi yetu. kupata katiba ya watanzania ni haki yetu, ila haitakuwa rahisi kwakuwa ni sawa na kuwanyang'anya magamba tonge mdomoni.
 
tume huru itatokana na KATIBA mpya wadau. tuhakikishe tunapata katiba mpya kabla ya 2015
 
Tunailaum tume au aliyeiweka tume? hebu tujiulize vizuri? Ebu tusubiri uone watakavyofinyanga mchakato wa katiba mpya! hapa cha kufanya ni kama misri au tunisia watachomoa tu! Otherwise tukae tutulie tuombe sana kwa mungu ili waendelee kugombana huko kwenye magamba yao mpaka wachomoke basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
kwa jinsi ninavyoona mambo yanakwenda katiba mpya itakuchua muda mrefu sana kupatikana hata kabla ya uchaguzi wa 2015. Hivyo basi kuna haja kubwa ya kudai tume huru ya uchaguzi kabla ya mwaka 2015.
 
Tuna miaka minne ya kuingia kwenye uchaguzi na kwa walio wengi bado ndoto ya kuiondoa CCM haijafa na kwanza ndio inakua.

Mabadiliko ya katiba in reality yanachukua muda mrefu sana, unless we need to rush into it na serikali iwe pamoja na wapinzani kitu ambacho si hakipo.

Ninavyoona naona kama pressure ikiwekwa kubadili tume ya uchaguzi angalau kunaweza kukawa na tumaini zaidi ya kuindoa CCM. Kwa mawazo yangu ya haraka ambapo nahitaji mwongozo kwa wanaojua je,

1. Kubadili tume ya uchaguzi ni lazima katiba ibadilike?
2. Je kama katiba ibadilishwe kwanza ndio tume ibadilishwe , je haiwezekani ikafanyika pressure ya kujadili ili kwanza?

3. Kama tume ya uchaguzi inaweza kubadilishwa kwa sasa naona kama ni vizuri tukaanzia hapo ili hali main objective/ajenda ya kubadili katiba isifutwe.

4. Hata kama katiba itabadilika kesho, we may have another time to implement it accordingly..that

Siasa za Afrika ni nani anatangaza matokeo ndio muhimu zaidi, si nani ameshinda

What do you think?

Mwanzo wa thread hii ni kwa sababu kushindwa CDM uchaguzi igunga ama vp ?. Timing yako sio nzuri mkuu ungeileta baadae kwani watu wana majonzi ya kupigwa dafrau la nguvu la Igunga
 
Katiba inayokidhi haja za watanzania ikiwemo tume huru ya uchaguzi ndio kinachotakiwa. Tatizo ni serikali kutokuwa na nia ya dhati ya kuunda katiba mpya. Kwa mfano, wameleta bungeni mswaada kandamizi unaompa rais madaraka makubwa na kuwa ndio mwamuzi wa mwisho wa namna katiba itakavyo patikana, afadhari umekataliwa.

Cha msingi kwa sasa ni kuendelea kudai kwa nguvu zote katiba mpya, tukisema tukomalie tume huru ya uchaguzi tu itakuwa mtindo ule ule wa viraka! Ni afadhari hata katiba ikichelewa lakini mwisho wa siku tume na katiba nzuri inayokidhi mahitaji ya watanzania wote wakiwemo CCM wenyewe!!
Umegusa mawazo yangu. Kuharakisha sasa kupata tume huru ni kuzidi kujitia kitanzi kwani waundaji tume ni hawahawa manyang'au magamba. Hakikia waitachakachua hiyo tume kukidhi maslahi yao. Cha kufanya na ambacho Watanzania tungekazania ni Katiba Mpya, ambamo hata hiyo tume imo ndani ya katiba.

Tatizo ni kuwa ili kupatikana kwa katiba Mpya kunaweza kuwa hadithi isiyo ukomo kwani magamba wamekamata mpini, au tuseme tumewapa mpini. Pengine mawazo yangu ni ya "msimao mkali", lakini hakuna njia mbadala kwa kundi la "watu wasiokubali kwenda hadi kwa mateke"; hawa ni CCM. Fikiria lile la mswada wa katiba, wananchi tulipokuwa sauti moja bila kujali itikadi wala dini, CCM hatimae walikubali kuteremsha suruali. Ni shinikizo tu la wananchi linaloweza kuwafanya magamba watafakari. Tusiogope kuambiwa tunafanya fujo kwa kudai haki zetu. Ule mpango wa maandamano namikusanyiko tuurudishe: kila kijiji, kila kata, kila wilaya, kila mkoa, kila palipo na uwanja au eneo la wazi tuandamane, tukusanyike, tupige kambi kama wananchi wenye hasira, wanaodhalilishwa na utawala. Tusiogope! Misri na Tunisia walianza, Yemen na Siria wanaendelea, Israel, Marekani, Spain, UK wamo mitaani...mote wanafanya maandamano ya amani kupinga dhuluma. Kinachotushinda sisi ni kipi? Pengine tukipata jibu la hili tutajua wapi pa kuanzia.
 
ivi huko kwingine ambapo upinzani uliweza, walibadilisha tume ya uchaguzi? Tuangalie Kenya, Zambia, nk. Ishu hapa ni kupambana. Tunahitaji kupambana wandugu. Kuondoa ccm sio vita ya kwenye mitandao...ni lazima tuwe askari miguu tukachunge kura na kuhamasisha watu!
 
Sitaki kabisa kuamini kuwa Tume ya uchakachuzi(uchaguzi) ilishindwa kutangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa igunga ndani ya masaa 24 kama walivyo ahidi, zoezi zima na mchakato mzima wa majumuisho ya matokeo yaliyotoka katika vituo mbalilmbali jinsi ulivyokuwa unanipa mashaka kuwa kuna ufundi potoshi hapo. nina uhakika kama CCM ingekuwa imeshinda kihalali basi matokeo yangetangazwa siku ileile ya jumapili hata kabla ya saa sita usiku, na kama mawazo yangu ni kweli , basi Tume hii ya uchakachuzi inafanya kazi kwa maslahi ya chama cha magamba na tusipo dai tume huru basi CCM itabaki madarakani milele.
nawasilisha.
 
Back
Top Bottom