Mwongozo kusitisha shughuli zote za Bunge kujadili Mgomo wa waalim 30/07/2012

mtendaji wa kijiji

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
533
114
Kama kweli wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wanajali maslah na wapo kwaajili ya kutetea haki za wananchi wao. Tunaomba jumatatu 30/07/2012. SPIKA Asimamishe shughuli zote Na kujadili swala la mgomo wa waalimu. Aidha hatutarajii kusikia majibu ya kipumbavu kutoka kwa Spika wala Lukuvi wala Werema kudai kuwa Swala hili lipo mahakamani. Kimsingi swala ambalo limesha anza kusikilizwa mahakamani ndo halitakiwi kuzungumziwa. Hili la waalimu bado halijaanza kusikilizwa kwani juzi ijumaa mahakama ilitaka pande zote mbili zikapange hoja zake vizuri ili jumanne zipokelewe mahakamani. Leo ni jumatatu, kesho juma4 hoja za pande mbili ndo zitapelekwa mahakamani. Tunaomba bunge litimize wajibu wa kuisimamia serikali. Hoja hii ikikataliwa tunategemea kuwaona wabunge wa vyama vyote wakitoka Bungeni ili kutoa msimamo wao nje ya Bunge. Mama ana Makinda jiandae kususiwa Bunge kama huna utu na kama huna watoto wanaoathirika na mgomo huu
 
Ngoja tusubiri hiyo kesho....ila mimi siendi shuleni, nitabaki nyumbani kama Mukoba alivyoniasa jana....!!!
 
mimi mgomo nilianza siku nyingi sema kesho nauendeleza tu mana toka nianze january hata topic mbili hazijafika.
 
Walimu wakigoma tunawachapa bakora tu. Tumewaweza madaktari itakuwa walimu?. Na pia tunaweza kuwafukuza kazi na watakuwa hawana pa kwenda. Vyeti vyao hata Malawi havitambuliki acha kenya. Nyie walimu acheni kufuata mkumbo, fanyeni kazi huku madai yenu yanashughulikiwa na Serikali.
 
Acha ma2c kwa waalim bilashaka una akil ndogo ka sicm. Ok wafukuzen wote mlete wengne toka kenya
Walimu wakigoma tunawachapa bakora tu. Tumewaweza madaktari itakuwa walimu?. Na pia tunaweza kuwafukuza kazi na watakuwa hawana pa kwenda. Vyeti vyao hata Malawi havitambuliki acha kenya. Nyie walimu acheni kufuata mkumbo, fanyeni kazi huku madai yenu yanashughulikiwa na Serikali.
 
Mgomo uko pale pale waende mahakamani CCM waifanye mahakama kutii wayasemayo walimu watagoma tuu!
Mahakama c inajua wajibu wake?
Kwanini ifuate maelekezo ya watawala(CCM)? Au kwa cvile mteuzi wao ni jk? Mgomo daima mpaka kieleweke!
 
mihimili iheshimiane. Hili swala lipo mahakamani. naomba ukae chini hakuna muongozo juu ya muongozo. sasa tunaendelea katibu.., Mia
 
Bunge hawataruhusiwa kujadili kama kawaida yao wameshapeleka hii issue kwenye chaka lao(mahakamani):eek2:
 
'Hivi jamani waheshimiwa wabunge hamjui tunaangaliwa na nchi nzima,mihimili mingine inalalamika kuwa inaingiliwa,MNYIKA nimesema kaa chini, katibu endelea'
 
Mh spika kwa taarifa tulizozipata ni kwamba asilimia 90% mashuleni leo asubuh wanafunz wametelekezwa baada ya waalimu kurejea majumbani mwao. Hivyo tunaomba tena kwa uchungu uruhusu bunge lako takatifu lijadili swala la mgomo wa waalimu. By Mh Tundulisu
 
Back
Top Bottom