Wafuatao waliwahi kukutana uso kwa uso na busara na hasira za Mwalimu Nyerere!..

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda....

2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...

Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......
 
mkuu yote ni ya kweli haya maana nyerere anamchapa sitta bakora hi mpya
 
ccm iliyokosa dira 'kolimba' hapana hapo ndipo alipo watungia kitabu! Kolimba na baba baharia
 
Nimeipenda #4 . Synnegy: Warioba na team ya Katiba kushauri serikali tatu si UJINGA bali ni njia ya kupitia ili kuwa na serikali moja.
 
6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...

Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......

Hapo Lowasa asingekuwa na chake, hata mpaka sasa Mkasi ni uleule hata ahonge na harambee za Matrilioni.
 
Angekuwepo si ajabu angemhoji JK, wale Majasusi wa Marekani wamedhibiti ikulu kwa masaa 48 wakati tuna wanausalama wetu imekuwaje?...(sijui kingefuata nini baada ya swali)
 
Hapana chezeya Baba wa Taifa. Kamlamba Sitta bakora ha ha ha ha!! Kweli usiku wangu umekuwa mzuri.
Alafu mzimu alio uachia CCM unawaumiza sana, pale alipowaambia nyinyi CCM mmemuacha yule kijana wa karatu akimaanisha Dr wa Ukweli Slaa. Alisema yule atakuja kuwa Rais. Awamu ya kwanza kweli kawa Rais ila ndio hivyo tu dhuluma. Sasa ccm wakitaka kuwa safi wamwache Dr wa ukweli achukue nchi iwe salama 2015.
 
Kipindi kile ukiwa mkaidi unachapwa bakora,kipindi hichi ukiwa mkaidi unang'olewa kucha,unapigwa bomu au unapotezwa,hapana chezea jakaya.
 
3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...
Rais anaenda kutatua mgogoro wa Maziwa na Siagi?! Ndio maana huyu tulie nae anaenda hadi kwenye misiba ya wacheza shoo...
 
5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......

Hapa kwenye issue ya Malecela, umeweka story za vijiweni.

Nyerere hakufurahishwa na Malecela kushindwa kuwadhibiti G55 walipodai serikali ya Tanganyika.
 
7. Baada ya Henry kissinger kuhitaji kufanya ziara Tanzania akiwa kama secretary of state (USA) kama kawaida yao USA wakaja na ulinzi wao ndipo mwalimu akamwambia henry, "Ulinzi wote huu wa nini.?", akajibu kuimarisha ulinzi, ndipo mwalimu akamwambia kama uliona hapa (TZ) hakuna ulinzi umefuata nini.?, Tuna ulinzi wa kutosha kama huitaji ulinzi wetu na unaona si mahala salama ni vyema ukaondoka. Vinginevyo suala la ulinzi wako ni juu yetu.
 
Baba Ritz walimuuliza una wake na vimada wangapi?akajibu 14,akatikisa kichwa akasema ukipata Urais utaoa wabunge wooteee na kuwapa viti maalum mamis wote na kila anayekusifia

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom