Mwl. Nyerere Angeruhusu JK Awe Rais wa Tanzania Mwaka 1995 Hali Ingekuwaje?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
WanaJF,
Kwa namna nchi inavyokwenda chini ya uongozi wa Jk, nimekuwa nikipata wasiwasi juu ya uwezo wa rais jk kiuongozi. Nimekuwa nikijiuliza kwamba hivi nchi yetu ingeelekea wapi endapo Jk angeachwa awe rais wa nchi yetu???? Kama leo hii, uwezo wake wa kuongoza upo hivyo, je, uwezo wake ulikuwaje kabla hata ya kuwa waziri kamili tena wa mambo ya nchi za nje kwa miaka 10 mfululizo??? Je, jitihada za Mwl. Nyerere za kuingilia kati 'move' ya kumteua Jk na hatimaye kuwezesha Mkapa ateuliwe kuwa mgombea wa urais zilikuwa na maana yoyote kwa mustakabali wa taifa hili? Ni udhaifu gani aliokuwa anaukwepa Mwl. kwa Jk ambao Mkapa hakuwa nao? WanaJF tafadhali karibuni kwa mjadala.
 
MWL nyerere alitoa maoni yake na ccm wakaogopa ndio ikawa hivyo, mwl alikuwa hataki malumbano na mtu, akisema ndio hilohilo na jamaa wa ccm hawapingi kitu akishasema mkuu wao. Mkapa ana uzuri wake na Mkwere ana uzuri wake na ubaya wake, sioni tofauti kati yao.
 
bado mnaongozwa na MFU?

nchi ina mihimili yake na hiyo ndio ya kuangalia. Si mtu ambaye keshakufa na alikuwa redundant when alive as well as dead

as a country i think tumehsa mature enough na kuacha mambo ya kutaka kumfanya Nyerer Mungu mtu.

Saa zingine nasikia kichefu chefu mtu analeta hoja ambayo inko centered on mfu
 
Madrasah Islamiyyah, JK Nyerere ni muasisi na baba wa taifa, aliisha sema mkwere amedumaa hawezi kukua hence hafai kuwa raisi.
 
Me namuona Mwl Nyerere kama dikteta anayependa maendeleo kwa wazawa...... the same na Hitler... asingekubali kumuona jk akifanya mzaha na watu halafu akanyamaza.... hii nchi inahitaji dikteta atakayejali wazawa...... ndo tutaendelea ila bila hivyo wakina rostam,karamagi na mafisadi wengine watazidi kunufaika...
 
SLIDINGROOF
Member

Join Date :Sat Dec 2010
Posts : 45
Thanks 4
Thanked 9 Times in 6 Posts Rep Power 0
 
Kama JK angechukua nchi hii mwaka 1995 basi hii nchi leo ingekuwa kama Somalia.Pili gharama za maisha zingekuwa juu maradufu na pesa yetu ingeshuka sana thamani na nafikiri dola 1 ingekuwa sawa na sh. 2600/-
 
Madrasah Islamiyyah, JK Nyerere ni muasisi na baba wa taifa, aliisha sema mkwere amedumaa hawezi kukua hence hafai kuwa raisi.

Hivi huyu Nyerere si ndie alie tupeleka pabaya zaidi ya kikwete na viongozi wengine waliopita ? Mmeshasahau kuwa wakati wa utawala wake maisha yalikuwa magumu zaidi ?

Kweli kuna watu wakina Rev wana short memory !!!!
 
Nyerere ni nyerere tu huwezi kumkompea na huyu mpare aha samahani huyu mkwere
 
WanaJF,
Kwa namna nchi inavyokwenda chini ya uongozi wa Jk, nimekuwa nikipata wasiwasi juu ya uwezo wa rais jk kiuongozi. Nimekuwa nikijiuliza kwamba hivi nchi yetu ingeelekea wapi endapo Jk angeachwa awe rais wa nchi yetu???? Kama leo hii, uwezo wake wa kuongoza upo hivyo, je, uwezo wake ulikuwaje kabla hata ya kuwa waziri kamili tena wa mambo ya nchi za nje kwa miaka 10 mfululizo??? Je, jitihada za Mwl. Nyerere za kuingilia kati 'move' ya kumteua Jk na hatimaye kuwezesha Mkapa ateuliwe kuwa mgombea wa urais zilikuwa na maana yoyote kwa mustakabali wa taifa hili? Ni udhaifu gani aliokuwa anaukwepa Mwl. kwa Jk ambao Mkapa hakuwa nao? WanaJF tafadhali karibuni kwa mjadala.

Ni udini tu kwani wewe hulijui hilo?
 
mh,mi nadhan ktk nchi hii bado sijamuona mwenye dhamira ya dhati,wanaoenda ikulu wapo pale kwa ajili ya familia zao na maji2mbo yao
 
Ni wale wenye mawazo na fikra mgando tu ndio wanaweza kuhoji dhamira na uwezo wa mzalendo huyu kuona mbali. Hata wengi wanaomchukia ni kwa hisia za udini tu hawana la ziada. Nyerere ndiye mzimu wa Tanzania ukikiuka misingi aliyo jaribu kuijenga utaishia kuweweseka tu. Pumzika ewe mwana mwema wa Afrika.

Ulimwengu daima huchukia watu wema na ndio maana hawana maisha marefu.
 
Mbona watu hawataki kutofautisha wakati wa utawala wa JKN ambapo kulikuwa hakuna demokrasia mtu ukimpinga kiongozi unafungwa huko kilwa km Mapalala, sasa ulimwengu umekuwa km kijiji mtu unatoa mawazo yako na mataifa yanakusikiliza.
suala la Dowans hakuna mtu leo angetaifissha km majumba ya Msajili au mashamba ya mkonge huko Tanga na Same.
Bado JKMrisho ndiye kiongozi bora katika wote wanne, technologia inambana mpaka ameruhusu demokrasia ya kujieleza na habari tofauti na Somalia vyombo vya habari hakuna. Kikwete ni Kiongozi anayechanganyika na watu, michezo, muziki wa Bongo flava, ni nani alikubali waingie Ikulu au kumpelekea kombe?
semeni yote Ikulu haitapata mtu asiye na ukabila wala udini, wote mnaowataja hata wa upinzani ni lini watajumuika na wananchi wa kawaida hata kuwaalika wenzao kusheherekea nao hata ubatizo, ni wabinafsi tupu.
Laabda

Attachments

  • pinda.JPG
    pinda.JPG
    20.1 KB · Views: 23
Back
Top Bottom