Mbogela
JF-Expert Member
- Jan 28, 2008
- 1,384
- 257
Mbogela,
Speak for yourself. Sijawahi kuquestion sababu za kwenda vitani na Uganda na hata hapa JF wanaoquestion au walioquestion wana agenda zao. Kila Mtanzania makini anajua sababu za kupigana na Idi Amin. Na katika vijiji vya ujamaa ni watu kama wewe mnaoamini bila ushahidi kuwa kuna binadamu walioliwa na simba. Naona mnajaribu kuandika historia upya.
Sababu tunazo na uwezo tunao lakini naomba uniambie sababu hizo, kwa ujumla sababu zilitengenezwa.
Turudi kwenye Nobel Prize. Bw. Nobel katika harakati zake aligundua formula mchanganyiko wa chemicals ambazo ukiziunganisha pamoja zilikuwa explosive kwa ajili ya kupasulia miamba kwenye migodi ya madini.
Kutokana na ufumbuzi huu alipata sifa na pesa nyingi sana. Lakini bahati mbaya wakati huo suala la amani lilikuwa tete, serikali zikatumia Formula ya Bw. Nobel kutengeneza mabomu ambayo yalitumika kuua watu na kusababisha madhara makubwa sana duniani ikiwemo uharibifu wa mazingira.
Bw. Nobel alisikitishwa sana kwa hilo, akajilaumu kwanini alidiriki hata kufikiria hiyo formula, alijua itarahisisha maisha sasa imakuwa kinyume imeharakisha maisha.
kwa hiyo kurekebisha hili alianzisha mfuko utakao wahamasisha vijana kubuni vitu vipya vitakavyosaidia kuleta amani na Ndio Nobel Peac Prize.
My Take: Kwa hiyo suala sio kushiriki kwenye kuikomboa africa kama mnavyodai, lakini kubuni njia mpya itakayoiwezesha afrika kukomboka bila vita. Sasa ukiangalia JKN hakuhamasisha kusimamisha vita ila alihamasisha vita kwa kuruhusu nchi za kusini mwa afrika kuweka kambi za mafunzo nchini mwake. Hii ni kinyume na Nobel Peace prize.
Nyerere hakutengeneza mazingira na vijiji vyake vya Ujamaa bali waliharibu mazingira kucreate vijiji na kudisturb equal system.
Akina Ysuph Lule wamewekwa kuzuizini
Akina Tuntemeke Sanga waliwekwa kizuini nchini mwao
Akina Toga (mbunge wa Iringa) waliwekwa kizuizini. Utampaje huyu Peace Prize.
Nimesoma Vitabu vya JKN, Kwame Nkrumah, nimeipenda filosofia yao, walikuwa na malengo mazuri, lakini bado hawaendani na malengo ya Nobel Peace Prize.