Mwl.Nyerere alilia machozi nyumbani kwa Malecela

SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
202
Mimi kiukweli nampenda sana mwl.nyerere,ingawa jamaa mmoja aliniambia kuwa mimi ni mtumwa wa legacy ya mwalimu,nakubali sana iwapo utumwa huo utanipa muda zaidi wa kupata interesting stories za Mwl.

Kama mnakumbuka vema,mwaka 1989,mh.Malecela alikuwa balozi nchini uingereza kabla ya kuitwa mwaka 1990 kuja kukamata nafasi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais Mwinyi.Wakati huo watoto wake wakubwa wa kike,yaani Dr.Mwele, Dr.Seche na Judge Mwendwa walikuwa wanasoma nje ya nchi.Dr mwele akiwa UK,Seche akiwa USA na Mwendwa akiwa chuo cha Birmingham nchini uingereza.

Mzee Malecela alisema kuwa Mwl alifika kwake ubalozini wakati watoto wake wote wakiwa likizo.Wakaitwa mbele za Mwl nakuanza kutambulishwa mmoja baada ya mwingine kwa majina na shughuli au masomo anayofanya.Dakika chache baada ya utambilisho Mwl.alitoa kitambaa na kuanza kufuta machozi kwa muda wa dakika kadhaa.Nikamuuliza mzee Malecela kama mwl. alisema ni nini kilimliza au kama anaweza ku-guess,akasema hajui.Na akakataa kata kata ku-guess.

Jambo hilo lilinishangaza sana,lakini binafsi nilihisi Mwl.alilia kwa sababu ya tofauti alioiona kati ya watoto wake na wa malecela,kielimu na hata kimaisha. Wenzangu mnasemaje?

Hata hivyo nitaendelea kuwaletea yale msiofahamu kuhusu mwl.Nyerere.
 
SAGANKA Walikuwa Majirani; Kina Mwele walipokuwa Wadogo MSASANI na Unajua Malecela alifiwa na MKWEWE; In a sense he was a SINGLE PARENT... Sasa labda NYERERE alilia kwa FURAHA kuona hao watoto waliofiwa na MAMA yao WAKIWA BADO wadogo na ni wa KIKE wameweza kuendelea na kwenda SHULE...

Kumbuka Baada ya Mama yao KUFARIKI; First Born wake kwa JINA SENYAGWA pia alifariki kwa Ajali ya Gari Pale St. Peters kwenye kile kimlima kidogo...

So, it was kinda REMORSE to the family...
 
Last edited by a moderator:
kama ndo angekuwepo sasa hv akiwaona wakina riz 1 si angezimia kabisa watoto wadogo mabilionea
 
Makongoro amemshinda yule jamaa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa E A Sasa unataka watoto wa Mwalimu wawe na elimu kiasi gani?
 
Le Mutuz inaonekana hakupenda kutulia home akiwa London,yeye viwanja tu,ndio maana hawakuonana na Mwl alipofika nyumbani kwao!
 
Huyo ndo Nyerere bwana alishawahi kuingia kwenye list ya watu 100 muhimu duniani namshangaa sana huyu Kichwa! Hebu jaribu ku-google Nyerere quotes.
A Selection of Quotes by Julius Kambarage Nyerere "You don't have to be a Communist to see that China has a lot to teach us in development. The fact that they have a different political system than ours has nothing to do with it."
Julius Kambarage Nyerere, as quoted in Donald Robinson's
The 100Most Important People in the World Today, New York 1970.
 
ila nafikiri sokoine angekua rais wa nchi hii pengine angefanya mengi kwa watanzania kwa kuendeleza mazuri ya mwalimu kwa sababu wakat mwalimu anaacha madaraka hali ilikua mbaya kias flan so angekuja mtu mwingine kuwezesha hali kua nzuri basi watu wasinge mkumbuka mwalimu kama ilivyo sasa! mim naamin watu wanamkumbuka mwalimu sana kwa sababu maraisi waliomfwata wameboronga sana! kwa mfano ile salaam ya "zidumu fikra za mwenyekiti" , sokoine aliikataa akairekebisha kwa kusema "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti" kwa maana hiyo sio sahii zisidumu!
 
Usisahau kuwa malecela naye alikuwa miongoni mwa watu 34 maarufu duniani mwaka 1984 na barani afrika walikuwa watatu tu na nyerere hakuwemo.
 
Back
Top Bottom