Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

Mhh... anachelea kusema itafika siku kila mtu amechoka lakini anaogopa kulianzisha sasa akawepo wa kuanza wanaweza jitokeza wafuasi wengi ikawa balaa kubwa kwani anayozungumzia ni ukweli kuwa inawezekana waajiriwa wakagoma ikazua maandamano wakajitokeza wabeba mizigo nao wakaunga msafara, wachuuzi wa biashara ndogo ndogo nao wakaingia,ikaja watu wasio na kazi maalum, basi inaweza kutokea hatari kubwa hapa.
Ni bora suluhisho lipatikane kupitia mezani kuliko barabarani.
 
Niko kwenye Mgomo hadi tarehe nane ole wake yeyote atakaye ni letea ujinga, Mkwere mimi hanitishi eboooo
 
Inatakiwa JK awaombe radhi wazee wa dar. Kwani kakusanya mashangingi na mimama mihuni kumshangilia then anasema wazee wa dar salam. Angesema wazee wa CCM tungemuelewa vizuri sana. Wazee halisi wa dar wapo wenye busara zao, hawawezi kushabikia upumbavu wa namna ile.

Nadhani hili linamaliza ubishi wa suala hili la wazee. Halafu ni lazima tuwe tunajua kuwa watu wanaoitwa wazee ni watu wenye nasaba bora sasa na hiyo mishangingi ya CCM ikipewa sh 5000 siku hiyo basi isharidhika na inashangilia! inakera sana. Nadhani itabidi awaombe radhi wazee wenyewe maana hajawatendea haki kabisa.
 
Mimi niliangalia kwa makini sana, wapo waliokuwa wanashangili ili wakumbukwe kupewa angalau ukuu wa wilaya, wengine walikuwa kimya tu na wengine walishangilia ili wasionekane wanapingana naye.

Lakini sidhani kama ukumbi mzima wote walikuwa 100% nayeye, kama walikuwa hivyo basi hawakutumia ile ya Akili za mwenzio changanya na za kwako
 
Masharubu inaelekea calculator ya ikulu inatoa hizo figure. Mbali ya petroli sukari ilikuwa 750 sasa 1800 unga,maharage,vyote lakini yeye haoni hayo. Ni wakati wa mabadiliko sasa.
 
nimefurahishwa na thread yako, kwanza kikwete amekiri wazi kua serikali yake haina uwezo wa kubadili hali ya maisha ya watu hata hali na garama za maisha zikipanda serikali kikwete amekiri kua haina chas kufanya kwani pato la serikali ni FIXED.

sasa watanzania tujiulize je garama za maisha jinsi zinavyozidi panda bei za basic need ziko juu, elimu, nishati nk huko mbeleni kuna future kweli kwani rais amekiri kua hali haiwezi badilika labda kwa muujiza.

watanzania sasa tumepata fundisho kutoka kwenye sera za wordl bank na imf kua hazifai pale iliposema serikali ijitoe kwenye kufanya biashara na kutegemea kukusanya kodi tu maana yake swerikali haina room ya kuongeza pato zaidi ya kuongeza makodi ya kuumiza watu kama haya payee etc ina maana umaskini utaongezeka zaidi ya apa kwani kama serikali inategemea kodi kuna vitu ambavyo vitaisha kwani vinatumika continuously kama madini.

Waafrica kiujumla tuelewe kua sera hizi zinatupeleka shimoni hazina future na clashes kati ya matabaka ktkt jamii ndio kwanza yameanza kwani serikali haina uwezo wa kubadili chochote itabaki maneno tu kwani budget yake iko FIXED na haina uwezo wa kuziongeza kwani haina chanzo cha mapato imezuiwa kufanya biashara.

Tunaweza ku conclude kua sera za imf na world bank hazifai tutabaki kulaumiana tu ni muda wa kurudi nyuma na kuifanya serikali I control njia kuu za uchumi, wengine watakuona chizi kwa nchi kama ii lakini amerika kusini wenzetu wakabwa na uu ubepari sasa imefika mwisho serikali zinachukua tena uendeshaji wa mashirika na njia kuu za uchumi kama kule Bolivia, Venezuela na brazil. Hatujachelewa tena sisi tuna afadhali resources zetu hazijaibwa zikaisha kama wenzetu wa amerika ya kusini.
Mie naona kinachotakiwa sikuwa na figure kubwa ya mshahara ndio turidhike. Ukweli kabisa serikali yetu haiwezi kulipa mshahara huo. Ikijiminya ikalipa basi tujue kabisa barabara hazitajengwa na wananchi wengine watakosa haki yao ya msingi kutoka serikalini. Wafanyakazi tuache ubinafsi. Hii sio serikali ya wafanyakazi pekee. Kuna kundi kubwa ambalo si la wafanyakazi nao wanategemea huduma kutoka serikalini. Madai ya mshahara wa 315000 mie naona ni ubinafsi. Tunawasahau wenzetu walio wengi na huku tukijua serikali haina uwezo huo.
Cha msingi kama nilivyosema si mshahara kiasi gani bali huo mshahara unauwezo wa kununua nini? Tungegangamaa kwenye inflation nadhani tungekuwa na hoja ya msingi na sio suala la figure. Hii haingii akilini. Uklipwa hiyo halafu kesho nainflation ikawa more than 300% utasemaje?
 
Hivi 350,000(wafanyakazi)x315,000(kima cha chini)x12= 1,323,000,000,000/= ni kama tirion 1.3 kwa mwaka na pato la taifa ni tirion 5. Je JK hajatudanganya hapo.Kweli Watanzania waoga.
 
Inaweza kulipa na hata zaidi ya hizo, kwa maneno ya JK makusanyo yote ni 5.8Trilioni, ikifanya hesabu ya watumishi 350,000 kwa mshahara wa 315,000.00 kwa mwaka (miezi 12) jumla ni 1.32 Trilioni. Kwa mahesabu hayo ni kuwa hakuna kisichoewezekana
 
In short Tz hatuna raisi,tatizo letu tunachagua chama badala ya mtu itaendelea kula kwetu milele!
Uyu uyu JK atashinda kwa kishindo tuu ngoja october ifike
 
Tunaomba waliopo Dar hasa watu kama Pasco na wengine, kama mna contact za watu wa gazeti la Mwananchi basi mumtafute huyu bibi na kupata habari zake zaidi. Chadema mjitahidi muende kupata BUSARA za huyu bibi na ikibidi CHADEMA kimrudishie nauli yake ya kuja Dar na Kurudi KISARAWE na kama atakubali basi awe ALAMA YA CHADEMA kwa UCHAGUZI.

TUCTA pia kwenye mapambano yenu yajayo, basi MSIMSAHAU huyu bibi kwenye VIKAO VYENU. Huyu bibi ni SHUJAA kwelikweli.
 
Aliogopa kubanwa kwa maswali na hao waandishi ambao wengi wao tunaamini wanauwezo mkubwa kudadisi na kuchambua hoja. Ndiyo maana akaamua kujichagulia kikundi fulani cha watu ambao hawana upeo mkubwa wa kuchambua hoja ili wawe wanampigia tu makofi hata kama anayoongea hayana ukweli wala maslahi kwa Taifa, na wale mimi nawaita ni wanaCCM tupu wliokuwepo pale ndiyo wakapewa jina la wazee wa Dar.
 
Tamwa, Tawla, Kituo cha sheria na haki za binadamu, ubalozi wa marekani na wengineo mnaotoa vyeti kwa watu kadhaa huyu mama anastahili kupewa nishani ya juu ya ushujaa, mwanaharakati wa kweli aliyesimama kusema yaliyomo moyoni hakuogopa jua, hakuogopa uexpose identity yake, hakukaa ofisini wala wapi ametoka openly kusema kitu cha kweli bila kuficha neno. Asipopewa Tuzo utakuwa unafiki wa hali ya juu kwetu sisi wote.

Inanikumbusha yule mama mweusi wamarekani aliyekataa kusimama ili kumpisha mzungu kwenye basi. mpaka leo anachukuliwa kuwa ni chimbuko la harakati za watu weusi kujikomboa. Ndio maana walisema sikimbuki vizuri yale maneno ila ni kama vile she sat so that we could walk, martin luther king walked so that we could run and obama is now running and he is the first black president.

The old lady has walked so that we do what is necessary for our beloved country. What will you do to support the lovely old lady???????

Contacts pls,nimtumie japo 10kgs za unga wa mahindi!
 
Hapo ni Mbayuwayu staili na akili za mwingine. Haya yote yanamrudi mkulu kwa kuwa yeye ndie muongo na mnafiki na sio Mgaya. Bravo mgosi.
 
Tunaomba waliopo Dar hasa watu kama Pasco na wengine, kama mna contact za watu wa gazeti la Mwananchi basi mumtafute huyu bibi na kupata habari zake zaidi. Chadema mjitahidi muende kupata BUSARA za huyu bibi na ikibidi CHADEMA kimrudishie nauli yake ya kuja Dar na Kurudi KISARAWE na kama atakubali basi awe ALAMA YA CHADEMA kwa UCHAGUZI.

TUCTA pia kwenye mapambano yenu yajayo, basi MSIMSAHAU huyu bibi kwenye VIKAO VYENU. Huyu bibi ni SHUJAA kwelikweli.

Sikonge, awe alama ya chadema ya uchaguzi, na kanga zake na ndala anarepresent wapiga kura wa kweli wa tanzania. UMENENA .
 
Kikubwa ambacho nadhani kina wasikitisha wafanyakazi ni kwamba viongozi wa kuchaguliwa(wabunge etc) na wale wa kuteuliwa(Gavana wa BOT, mkuu wa TRA etc) wana lipwa mishahara mikubwa na marupurupu ambayo hayaendani na hali halisi ya uchumi wa Tanzania. Wafayakazi wamechoka kusikia kila siku bunge liki jipandishia mishahara ikidai ni haki yao wakati wao kupandishiwa japo kidogo inakua ni nongwa. Wafanyakazi wamechoka kupanda dala dala huko waki pisha viongozi wakuu wa nchi na vingora vyao. Wafanyakazi wamechoka viongozi na wachache wenye bahati kwa na uwezo wa kwa somesha watoto wao nje wakati wao watoto hata elimu siyo uhakika. Wafanyakazi wamechoka kuwa wakulima wa shamba liitwalo Tanzania lakini mavuno kufaidiwa na wengine. Wafanyakazi wame choka kuwa wamwisho kufikiriwa linapo kuja swala la maslahi na tija.

Nadhani kinacho takiwa kufanyika ni cost analysis. Mishahara ya serikali ilingane na uhalisia wa maisha. Hicho ndicho kikubwa wanacho dai wafanyakazi. Wafanyakazi hawana tamaa na wala hawaombi mishahara itakayo watajirisha bali mishahara itakayo kimu mahitaji yao binafsi ambayo ni haki ya kila Mtanzania. Wafanyakazi wanacho omba ni kutishwa mzigo wa kuitumikia serikali na kulazimika kuwaza ni vipi wataendesha maisha yao. Hakika madai ya wafanyakazi siyo ya kibinafsi kama yalivyo wengi wetu bali ni madai ya malipo ya haki kulingana na jasho lao.

Wafanyakazi hawaji piganii maisha yao tu bali wana pigania pia ulinzi wa maisha ya watoto wao. Kama watoto wao hawata weza kurithi mali za wazazi wao kutokana na utumishi wa maisha ya wazazi wao serikalini je si haki walau wakarithi elimu na afya bora ambao katika ulimwengu wa leo una gharimu pesa? Wafanyakazi pia wana pigania maisha ya wazazi wao. Tanzania jukumu la kutunza wazee lina anguka kwa watoto. Kwa nini tufanye wafanya kazi wajihisi kushindwa mbele ya wazazi wao kwa kushinda kuwatunza kwenye uzee wao kama wao walivyo watunza kwenye utoto wao? Wafanyakazi wana pigania maisha bora ya Watanzania kwa sababu mfanyakazi aliye ridhika ni mfanyakazi mwenye bidii zaidi na anaye tumikia kwa moyo wake wote, nguvu zake zote a akili zake zote.

Kinacho sikitisha Watanzania wenzangu ni kwamba kizazi cha uongozi wa leo Tanzania umetoka kwenye familia zilizo kuwa za hali ya chini au kati. Wengi wa viongozi wetu walisoma bre kutokana na sera za Mwl Nyerere. Wengi wa viongozi wetu walitembea umbali mkubwa kupata elimu ili kuja kutumikia taifa lao. Leo hii wamesahau walipo toka na wame wasahau vinara haswa wa maendelo ya Tanzania ambao ni wafanyakazi na watumishi wa serikalini, nafasi ambazo baadhi yao wenyewe ndipo walipo anzia.

Siku taka kucomment kwenye thread yoyote kuhusu huu mgomo wa wafanyakazi kwa sababu mimi ni mwanafunzi si mfanyakazi. Sijui uchungu wanao pitia na wala sijui mzigo wa kutunza familia kwa bajeti ya mishahara yao. Lakini naweza kusema nawaelewa kwa sababu ipo siku na siku labda si nyingi na mimi nitakua katika nafasi yao. Najua fika wanacho pigania leo hakita wanufaisha wao tu bali kita nufaisha na sisi kizazi kijacho cha wafanyakazi. Kwa hilo nawa shukuru kwa maana kwa namna moja au nyingine wana pigania maslahi yangu ya baadae. Nawa pongeza wafanyakazi kwa ujasiri wao na nawaombea kwa Mungu mafanikio kwa maana hawa piganii kupendelewa bali kupewa stahiki. Siku taka pia kucomment kwa sababu mimi sipo serikalini na wala sijui pesa zilizopo. Najua viongozi wana lipwa vizuri lakini silaumu kwa maana najua madhara ya viongozi kuto kulipwa vizuri bali na pia najua madhara ya wafanyakazi kuto kulipwa vizuri. Nawaasa tu waendelea kutumia vifaa vya amani kudai haki zao na hakika sauti zao zita kuja kusikika. Hakuna nguvu kama nguvu za wafanyakazi na serikali yoyote inalo tambua hilo ni serikali yenye mafanikio.
 
Tall mbona una limit watu wasieleze bana? sasa siungeweka vote tu hakuna kuandika ukisema kuandika tena siyo uchaguzi kaka. Sasa mimi nacheza faulo hapa.
Kwanza ningeyaona tu ningesema kuna jambo hapa mpaka hawa wanasema hivi kwa sababu kila mtanzania alisikia hivyo gazeti ni playback sasa playback ikija vibaya inakuwaje? Potelea mbali magazeti yangu mimi huwa 1)Mwananchi 2)Tanzania Daima 3)Jumatano (2): Haya magazeti manne hata yakiandika heading mbaya lazima niyanunue. Sasa tall unakosea ukisema watu wachague gazeti watakalonunua kwa heading ya leo tu hapo unakuwa unataka nini katika uchambuzi wako hasa? Unataka kupandisha chati gazeti ambalo silo.
ok,mimi simo. huwezi kupandisha chati kwa toleo moja tu. HUJANIELEWA. soma vizuri thread nia ni hawa jamaa watuletee angalau habari inayofananafanana.
 
nimeifuatilia sppech yake, aliongea bila kujua mambo naye hajui hata mfanyakazi wa ndani aneongelewa na kapuya ni yupi? he knows nothing ila ni kulipuka tuu.
 
Back
Top Bottom