Mwita Waitara Mwikabwe Mbaroni kwa mauaji Singida

Huo ni uzuzu wa sheria. Kumbuka kesi ya akina Zombe nani ndiye alikuwa muuaji. Kuna aliyeua, waliamrisha mauaji, walioshiriki mauaji na waliohusika na mauaji. Sasa Mwita amehusikaje?
Hata ukiamrisha tu kuuwa au kufanya uchochezi na kifo kikitokea basi unahusika na uuaji moja kwa moja.
 
Nini Kazi ya polisi. kwani walienda pale kusikiliza sera kama wananchi wengine.. Kilianza kikundi kidogo kupiga mawe.. yakasimama... issue imepamba moto yakadai yameshindwa nguvu... Moto uanza taratibu usipouzima mdogo mkubwa utakushinda.. Maskini vyombo vyetu vya dola
 
tunaipongeza sana serikali yetu kwa hatua stahiki, dola isiwavumilie hawa wahuni wataharibu amani ya nchi yetu.
 
sasa si ccm au cdm wote wameoza kwa tuhuma za matumizi ya nguvu kufanikisha malengo ya kisiasa...............chaguzi ya 2015 inabidi tujifunge kibwebwe vinginevyo tutajikuta kisiwa cha vurugu za kuwapigania wachache na jamaa zao kujipatia mkate wao kwa damu yetu.........

Mkuu cdm inatumia nguvu gani?? Kwani ina dola???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mwita anakabiliwa kwa kesi ya kutumia maneno yasiyofaa jukwaani.
Kesi ya mauaji inawakabili jamaa sita ambao ni wapenzi wa chadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hapana!! Hajashitakiwa kwa mauaji. Amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) katika mkutano uliofanyika kijiji cha ndago.
 
tunaipongeza sana serikali yetu kwa hatua stahiki, dola isiwavumilie hawa wahuni wataharibu amani ya nchi yetu.

Wahuni sana CCM wanavamia mikutano ya CDM, wanatesa na kuua kule mabwepande. Waliwakata mapanga wabunge wa CDM mbele ya polisi kule Mwanza. Ole wao maana kila damu inayomwagika inawalaani na Mungu asiyependelea atawahukumu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom