Mwita Mwikabe Waitara: Mwanasiasa zao la UVCCM aliyemwacha shetani na mambo yake yote!

wanatarime tunajuta kuchagua laana maana nyambari hata baba yake mzazi alimkataa maana alitanguliza miguu wakati anazaliwa kikwetu huyo ni laana hivyo waitara asikate tamaa 2015 atashinda yeye ajipange sawasawa:target:
 
Ameshusha hadhi. Inaonekana Emeka hata hajui kuwa Waitara alikuwa CCM wakati Mwera anagombea kwa tiketi ya CDM, na aliondoka baada ya kuhitilafiana na wenzake kwenye kampeni za uchaguzi ule. Labda kama sijaelewa bandiko lake.
Nimesoma na Mwita Mwikabe, nitakupa habari kamili. Hapo awali akiwa Rais wa DARUSO (2005-2006), mwita alikuwa ni mwanachama makini wa CHADEMA. Hata pale alipoulizwa na waandishi wa habari wakati fulani kuhusu kukubalika kwa Kikwete UDSM, Mwita alimponda sana Kikwete, magazeti yakaandika habari ile. Mwita akaitwa na akina Kingunge, akawekwa sawa. Wakati ule, watu wengi nikiwemo mimi pamoja na Mwita tulikengeuka, tukajiunga na CCM. Siku kama ya tatu akakanusha habari kuhusu UDSM kumkataa Kikwete. Magazeti yakaandika, Rais DARUSO ala matapishi yake.

Tangu hapo CCM walimmwagia Mwita fedha ya kutosha ili aendeshe kampeni pale UDSM, actually ndiye aliyepanga mkakati wa kumkutanisha Kikwete na wanafunzi wa UDSM pale diamond Jubilee. Akamwagiwa Tshirt za kutosha na midola teletele. Akafanya kazi kwa ufasaha sana, CCM ikashinda kwa kishindo pale UDSM, wakampongeza kwa kumpa ukatibu wa UVCCM wilaya ya Kinondoni. Mimi nikaambiwa nisubiri nafasi itakapopatikana watanipa ukatibu na mimi. Sijui wangenipeleka wapi. Niliwahi kumtembelea Mwita wakati ule pale Kinondoni kabla hajahamishiwa Tanga na tukaongea mambo kadha wa kadha, lakini roho yake haikuwa CCM kabisa, kulingana na maongezi yale. Iinaonekana pamoja na kuondoka kwake CHADEMA mwaka 2005, mapenzi yake kwa chama hayakuwa yameisha, akaanza kuonyesha jeuri kwa CCM, wakamhamishia Tanga, kama adhabu,baadaye Nchimbi aliyekuwa bosi wake wakati huo akamtaka Mwita aende makao makuu ya CCM akawe desk officer. Mwita akaona ni utoto akarudi kwenye chama chake (CHADEMA).

Kwa hapa naweza sema Mwita ni kama mwana mpotevu, aliyepotea akaingia CCM na baadaye akajua kwamba alipotea na kuamua kurudi alikotoka CHADEMA. Sioni sababu kwanini tumbeze, maana tangu alipoingia CCM hakuwahi kusimama popote kuiponda CHADEMA, ni dhahiri mapenzi yake kwa CHADEMA hayakuwahi kuisha. Tumuunge mkono, ninaamini ana uwezo mzuri kisiasa. Ni mtu wa kujishusha, mara nyingi napanda naye daladala hadi kule Kitunda, sijui ndo anaishi huko au huwa anakwenda kwa ndugu. Lakini wakati wote, hana makuu.
 
Mwita ni kamanda mpambanaji. Tumekuwa wote katika harakati za kuingia DARUSO na kuunda serikali ya wanafunzi iliyojipatia heshima kubwa zaidi.

Check list ya wapiganaji waliounda DARUSO 2005/6

Mwita Mwikwabe Raisi
Mrema John - Waziri Mkuu
Aurelia Kimaro - Vice President
Samwel - Fedha
Cosmas Gabriel - Usafiri
Engineer Mseti
Bahati Tweve - Accomodation
Marehemu spika wetu mungu ailaze pema peponi

Hiyo list ndogo tu na wengine wengi waliounda DARUSO chini ya uimara wa kamanda Mwita Mwikwabe.
Speaker alikuwa ni nani? Simkumbuki na wala sina taarifa ya kifo chake.
 
Tusihusishe siasa za vyuoni, nilikuwa kiranja chekechea.

Ila namkubali Mwita kwa determination na guts zake.

Go Mwita!
 
Mwita ni kamanda mpambanaji. Tumekuwa wote katika harakati za kuingia DARUSO na kuunda serikali ya wanafunzi iliyojipatia heshima kubwa zaidi.

Check list ya wapiganaji waliounda DARUSO 2005/6

Mwita Mwikwabe Raisi
Mrema John - Waziri Mkuu
Aurelia Kimaro - Vice President
Samwel - Fedha
Cosmas Gabriel - Usafiri
Engineer Mseti
Bahati Tweve - Accomodation
Marehemu spika wetu mungu ailaze pema peponi

Hiyo list ndogo tu na wengine wengi waliounda DARUSO chini ya uimara wa kamanda Mwita Mwikwabe.

Wewe ulikuwa mmoja wa hawa wapinaji sio?? Mlikuwa mnapigania sasa, maana tuna maneno yasiyostahirika kwa wakati wake. Kwa mara ya kwanza pale chuo kikuu mwaka huo ktk utawala huo, vyumba viliuzwa kama jungu, habari kubwa ya uuzwaji wa vyuma haikuwa siri tena, watu waligawana vyumba wajuavyo, kwa Mwita yeye alifanya vizuri, maana aliwasaidia sana vijana kupata vyumba kwa urahisi, na pale hall V ulikuwa ukiita Chacha, wanaweza kutoka vyumba vyote. Upiganaji unalipwa.
Endelea kuwauliza na hata kama wewe pia, watu walikuwa wanapeleka payslip kwa mhusika na kisha kupata chumba, lipa pata,
Usirudie sana kusema kama unazani ni shaihi, mwache Waitara aendelee na upambanaji, ila usilete habari ya Daruso, haina mashiko.
 
Nimesoma na Mwita Mwikabe, nitakupa habari kamili. Hapo awali akiwa Rais wa DARUSO (2005-2006), mwita alikuwa ni mwanachama makini wa CHADEMA. Hata pale alipoulizwa na waandishi wa habari wakati fulani kuhusu kukubalika kwa Kikwete UDSM, Mwita alimponda sana Kikwete, magazeti yakaandika habari ile. Mwita akaitwa na akina Kingunge, akawekwa sawa. Wakati ule, watu wengi nikiwemo mimi pamoja na Mwita tulikengeuka, tukajiunga na CCM. Siku kama ya tatu akakanusha habari kuhusu UDSM kumkataa Kikwete. Magazeti yakaandika, Rais DARUSO ala matapishi yake.

Tangu hapo CCM walimmwagia Mwita fedha ya kutosha ili aendeshe kampeni pale UDSM, actually ndiye aliyepanga mkakati wa kumkutanisha Kikwete na wanafunzi wa UDSM pale diamond Jubilee. Akamwagiwa Tshirt za kutosha na midola teletele. Akafanya kazi kwa ufasaha sana, CCM ikashinda kwa kishindo pale UDSM, wakampongeza kwa kumpa ukatibu wa UVCCM wilaya ya Kinondoni. Mimi nikaambiwa nisubiri nafasi itakapopatikana watanipa ukatibu na mimi. Sijui wangenipeleka wapi. Niliwahi kumtembelea Mwita wakati ule pale Kinondoni kabla hajahamishiwa Tanga na tukaongea mambo kadha wa kadha, lakini roho yake haikuwa CCM kabisa, kulingana na maongezi yale. Iinaonekana pamoja na kuondoka kwake CHADEMA mwaka 2005, mapenzi yake kwa chama hayakuwa yameisha, akaanza kuonyesha jeuri kwa CCM, wakamhamishia Tanga, kama adhabu,baadaye Nchimbi aliyekuwa bosi wake wakati huo akamtaka Mwita aende makao makuu ya CCM akawe desk officer. Mwita akaona ni utoto akarudi kwenye chama chake (CHADEMA).

Kwa hapa naweza sema Mwita ni kama mwana mpotevu, aliyepotea akaingia CCM na baadaye akajua kwamba alipotea na kuamua kurudi alikotoka CHADEMA. Sioni sababu kwanini tumbeze, maana tangu alipoingia CCM hakuwahi kusimama popote kuiponda CHADEMA, ni dhahiri mapenzi yake kwa CHADEMA hayakuwahi kuisha. Tumuunge mkono, ninaamini ana uwezo mzuri kisiasa. Ni mtu wa kujishusha, mara nyingi napanda naye daladala hadi kule Kitunda, sijui ndo anaishi huko au huwa anakwenda kwa ndugu. Lakini wakati wote, hana makuu.
Muulize Bahati Tweve kwa uzuri kabisa kama unamfahamu, Hyo alikuwa ni manachama mzuri sana wa NCCR-MAGEUZI, kuanzia akiwa Azania/Tambaza Sekondari, sasa kilimpeleka nini ccm, kilimtoa nini ccm, fursa zilikosekana maana ndo zilizompeleka, kwa sababu alikuwa ni mwanamageuzi akaangalia ni wapi ambako kuna upepo mzuri unao vyuma ndo akaenda zake CDM,
 
Umeingia huku jana na kuibuka na nyuzi za aina hii.....tuache kushusha heshima ya JF.Huwa hatujadili watu.

Awali ya yote tambua kuwa ubora wa mawazo ama fikra hautokani na umri wa uanachama katika vyama vya siasa.Vivyo hivyo kwa uanachama katika mitandao ya kijamii ikiwemo JF.Mara unapojiunga unakuwa na haki sawa na wanachama wakongwe.Yaweza kutokea Profesa fulani akajiunga JF leo na akaanza kuchangia leo na wakati huo huo akaanza kuchangia mawazo yake katika eneo alilobobea!bila shaka hutaweza kumtaka akae kimya maana umejiunga leo.
Wewe uliyejiunga muda mrefu ulipaswa kuonyesha uvumilivu wa kisiasa.
Ni sawa na kuamini kuwa watu wenye umri mkubwa wana akili kuliko wenye umri mdogo!
Hata dini zinatufundisha kuwa wakwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza.Hilo nalo hulijui, kama walijui walipuuza kwa sababu zako.Kifupi kabisa, kila mmoja wetu ,popote pale,anao uhuru wa maoni bila kulazimika kuomba ruhusu ya yeyote yule kabla ya kuweka wazi mawazo yake ,wala hakuna anayelazimika kumfurahisha yeyote na mahali popote pale.Hizo ndio moja ya gharama za demokrasia.
Aidha,ni vigumu kujadili siasa na dyanamics zake bila kugusia watu wanaoziendesha.
Naomba ajitokeze mtu ajadili siasa za TANU na harakati za uhuru aone kama hatalazimika kumtaja na kujadili nafasi ya Nyerere na wenzake.Akishindwa ,ajaribu kuchambua siasa za NCCR Magezi aone kama hajaishia kuwataja kina Marando!
Afanye vivyo hivyo kwa vyama vyote,then atapata jibu.
Pendekezo la kutojadili watu haliwezi kukubalika ikiwa lengo ni kufanya uchambuzi makini wa siasa..
Vinginevyo ni kama kula ugali bila mboga.
 
mwikwabe ni jembe la ukweli na msimamo wake wa kupignia haki haufanyi ndani ya cdm tu bali tangu akiwa anasoma pale chuo kikuu cha dsm ambako aliongoza maandamano kupinga ubaguzi wa wanachuo kukopeshwa kwa ubaguzi na wote wakafanikiwa kupewa fedha kwa 100% huu ulikuwa mwaka 2005.
 
Back
Top Bottom