mwisho wa kutumia analogy broadcastong techn.

Mnyaluhala.

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,430
1,773
Wadau wa jf me nakwazwa na uhamasishaji wa upande mmoja juu ya muda wa mwisho wa matumizi ya matangazo ya tv ya analogy, kwani kampuni zitakazotoa huduma za digital bado hazijajiimarisha hasa wilayani na kipindi hiki ilitakiwa wawe wameanza kutoa huduma na wananchi wapate kujua ubora wao kabla ya desemba mwaka. Pia gharama za ving'amuzi bado ni kubwa kwa wilayani kwani TING wanagharimu lakimbili na ishirini, zuku laki moja na ishirini hapo bad gharama za kila mwezi hujalipia na star time wapo makao makuu ya mikoa tu ! Sasa tujiulize kama serikali imejipanga kumsaidia mwanchi kweli. Naomba maoni yenu!
 
Ujue sawa som how kwakuingia huko 2nakuwa 2mepiga hatua but iv wa2 wanawafkiriaje kwa wale watanzania ambao hawana uwezo wataweza kumudu iyo hali
 
Ninasikia kuwa television za ndani zitakuwa bure na ushindani utakuwa ktk station za nje pia kwa makampuni yatakayohusika yatalazimika kuonyesha station zote za ndani. labda issue ni kuwa kwa miezi hii michache iliyobaki wataweza kujitanua mikoani kote? na watumiaji kutumia antenna ya kawaida badala ya dish? maana ktk gharama kwa watumiaji wengine kununua set kama ile ya ting ambayo ni karibu laki tatu ni gharama sana na hadi sasa kwa mikoani ni lazima wateja watumie king'amuzi kinachotumia dish
 
namimi wasiwasi wangu upo hapo kwa hayo makampuni kutanua huduma zao kabla ya desemba na gharama je zitakuwaje kwa wau wa kipato kidogo!
 
Wakati TCRA wanaamua watu walipiga makofi, hamna aliyewakumbuka Walala hoi! Wakati US wanafanya uamuzi kama huu waliwalipia hela wananchi ambao hawakuwa na uwezo. Sisi tusiokuwa na uwezo tunajiamulia Tuuu! Bila kufikiria!
 
habari wanatechnolojia wenzangu.suala la mabadiliko kutoka analogia kuelekea digital linaeleweka vibaya hasa na Mtanzania wa kawaida.mabadiliko haya ya mfumo yatahusisha mawimbi yanayosafiri kufuuata umbo la dunia kitaalam terrestrial(DVB-T,ndo mfumo wake).
mabadiliko haya hayatahusisha mifumo inayotumia satellite(DVB-S) hivyo watu ambao hawataweza kumudu gharama za ving'amuzi watalazimika kuwa na madish ili kuendele kufaidi ullimwengu wa digital.

nakili kwa upande fulani hili litakiwa gumu kwa watanzania wengi lakini haya mabadiliko sio ya Tanzania peke yake bali ni ulimwengu mzima na kwa wale watakaokuwa bado hawajabadili mifumo yao,mpaka 2013 hawatakuwa na haki ya kulalamika juu ya muingiliano wa masafa(frequency) kati ya watumiaji wawili.
mfano Uganda wanatumia 88Mhz kwa ajili ya television,mabadiliko haya yakija yataifanya 88Mhz kuwa huru kutumiwa na yeyote hivyo kuongeza upatikanaji wa masafa..
 
Wakuu , si lazima ununue "king'amuzi" , unaweza ukatumia dish na decoder kama ambavyo watu wa mikoani walivyokuwa
wanafanya siku za nyuma ili kupata station mbalimbali kama StarTV ,EATV , CH10 na kadhalika ambazo zilikuwa hazijafika
huko .
Kwa hiyo cha muhimu ni kuipigia kelele serikali ikakikishe gharama za hivi vifaa ni affordable kwa mtz yeyote mwenye uwezo wa kumiliki tv
 
76% ya watanzania haifikiwi na matangazo ya TV? haiwezekani ikawa kweli, labda kama Mr Mungi anaingiza kwenye equation yake hata sehemu ambazo kimsingi hakuna watu wanaishi kama water bodies (mfano. bahari, maziwa nk) na misitu
 
wanasema channel za bure zinatakiwa zionekane, watu wameshapewa maagizo lakini hao waheshimiwa wanakwepa swali la msingi. . . WHEN?

Lini tutaanza kuuona huo muingiliano maana hadi sasa hakuna! timeline ni muhimu, maagizo yasiyo na deadline hayatekelezeki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom