MWINYI Was A Visionary Leader

Mkandara:

Anza thread ya misaada na negative impacts zake kwa nchi za kiAfrika na nitakuja nichangie. Nikiendelea kuchangia katika mada hii itaonekana na-support waliomfuatia Nyerere.

Wako,

Z10.
Mkuu wangu hakuna sababu ya kuanzisha mada mpya kwa sababu tu ya kuelezea mabaya ya Misaada hali sote tunafahamu Ubaya wa misaada na hata mikopo kwa nchi maskini hata kama tukichukua mifano yetu sisi wananchi wenyewe tunavyoishi.

Maskini yule wa pale msikitini hata ukimpa millioni leo baada ya mwezi utamkuta kajipanga tena msikitini akiomba. Fedha ulompa atayafanya yote alokuwa hayafanyi ikiwa ni pombe atarudia kunywa, kuoa wake zaidi na kadhalika yaani kwa umaskini wetu mara zote tunatumia zaidi misaada hiyo ktk consumption expenditures na sii kututoa on development.

Tatizo kubwa la viongozi wetu leo hii ni Umaskini wenyewe na ndio tofauti ya Nyerere na kina Mwinyi, Mkapa, Kikwete na pengine viongozi wengi wa nchi maskini ambao huchukulia misaada kama vile ndio njia ya kuchuma (revenue) hivyo badala ya kutatua matatizo yaliyotufikisha hapo tulipo tunaangalia kwanza tunakosa vitu gani? (priorities) - ndio utayaona hayo mashangigi, ndege za marais wakishindana kwa ubora na uzuri, wakibadilisha suti kila siku n.k.

Nakuhakikishia fanya uchunguzi mkuu wangu utakuta hawa wote waliopita toka Mwinyi hadi Kikwete naweza kusema wametumia less than 40% ya fedha za misaada kwa development, nyingine ni Ufisadi na pengine kuwa allocated on consumption ili mradi tu wabembee kusahau shida na machungu kwa muda walioko madarakani.

Hivyo kama tungekuwa tume focus toka mwanzo tukachukua misaada na mikopo kwa malengo ya kujenga Uchumi wetu, kujenga infrastructure inayolenga Ufanisi na kuboresha njia za kukuza Uchumi hakika tusingekuwa tunalia leo hii na Umaskini wetu.

Kingine naweza sema ni Policies za kiuchumi zilizopo leo ni za kuiga, tunasoma madarasani zimeandikwa Ulaya tunakuja zi apply Tanzania kwa sababu tu Profesa fulani kavumbua mbinu ya kiuchumi inayotazama nchi tajiri kwanza na vipi maskini hao wanaweza kufanikiwa kwa sababu tu kinachozungumziwa ni Ubepari..

Ni sawa na leo wewe unaweza kuwa mwepesi sana kuandika kitabu kuhusiana na maskini wale ombaomba wa pale msikitini na makanisani na jinsi wao wanaweza jikomboa kutokana na umaskini wao lakini kwa sababu hujawahi kuwa maskini wala kulala pale mlangoni akili imefunga kabisa ukisubiri tu riziki yako kesho asubuhi, unaweza andika mengi yanayotokana na experience ya mwenyenacho au niseme mazingira ulokulia wewe..Trust me, huwezi kumtoa maskini ombaomba ktk umaskini kama yeye mwenyewe hataki kutoka hata kama uje na malaika - Ndivyo Miafrika Tulivyo.

Na ndio maana siku zote mimi binafsi naamini kabisa Ujenzi wa nchi yetu utatokana na sisi wenyewe kutambua kwanza tunataka kutoka hapa tulipo, tumechoka kusimama msikitini/makanisani na vibakuli vyetu tukisubiri misaada au kutembelea misikiti na makanisa mengine nje kila tunapoahidiwa kupewa misaada.

Hatutaki kutoka ktk umaskini asikudanganye mtu, na ndivyo wanavyofanya kina Kikwete na viongozi wengi wa Kiafrika yaani tunaishi kwa misaada sawa na maskini ombaomba na tabia hii imefika hata ktk jamii zetu yaani ndugu na jamaa zetu sisi wote huko waliko nyumbani wanasubiri misaada sisi tuwatoe...Ombaomba imekuwa utamaduni wa Mdanganyika!

Na kwa mtu yeyote hapa anayetuma fedha nyumbani kila mwisho wa mwezi, basi mhurumie yeye kwani ndugu na jamaa zake wamepumzika kabisaaaa!..wakisubiri msaada. Hii ndio tabia ya binadamu maskini na pasipo kufikiria tofauti hatuwezi kusingizia misaada kuwa ina athari kubwa bali athari ni sisi wenyewe kwani misaada inalemaza tu.

Waulize watu wanaoishi nchi za Ulaya na zile fedha za Zaka (Welfare) watakwambia zinavyowalemaza watu, kwani kila mwezi wanategemea cheki kutoka serikalini basi maisha yao yote huishia ktk ku bajeti na cheki ya mama (serikali), sana sana hutafuta kazi za chini ya meza (daywork) kuzibia matumizi ili mradi tu waonekane hawana kitu na kisu kile cha serikali kiendelee kushuka..

Tabia hii chimbuko lake ni Umaskini wa hali na mali na ndio mfumo walokuwa nao wote viongozi waliopita isipokuwa Nyerere lakini bahati mbaya alichokifanya Nyerere pia ilikuwa sawa na kumchukua maskini na kumrudisha kijijini kwao ukampa nyumba na shamba, mwezi mmoja tu ataacha kila kitu kule au hata kuviuza kwa bei ya njugu ili mradi tu arudi Dar kuendelea kuomba..Na ndipo tuliposimama leo hii.

Nachoweza ku conclude ktk hoja yangu labda niseme athari kubwa ya misaada ni - ADDICTIVE! ni kama vile Cocaine au Unga ukianza huwezi kuacha pasipo rehabilitation, kwa sababu mara zote misaada tunayopewa huitumia kwa vitu cisivyojenga ila kutubomoa zaidi.. tunachumia matumbo na faraja zetu, haya ndio maradhi alotuachia Mwinyi na IMF yake..
 
Back
Top Bottom