Kilbark
JF-Expert Member
- Feb 25, 2008
- 572
- 161
Wakati wa Mwinyi ndio kulikuwa na migomo mikubwa mikubwa, Wakati wa Mwinyi madaktari waligoma pamoja na wauguzi yeye akaenda kucheza kwasakwasa ya Kanda Bongo Man, wakati wa Mwinyi ndipo wafanyabiashara walipoifanya Ikulu kama gulio, wakati wa Mwinyi ndipo chembe chembe za sectarian violence na udini zilipojidhihirisha wazi ni yeye aliyeipigania sana hii hoja ya udini kama turufu ya kumpinga baba wa taifa, wakati wa Mwinyi nchi ilikuwa haikusanyi kodi , wakati wa Mwinyi ndipo nchi ilitaka kugawanyika, wakati wa Mwinyi ambapo hata Waziri Mkuu na mawaziri walikuwa hawawajibishwi ipasavyo, wakati wa Mwinyi ndipo tulipoona Tanzania inashuka kimaadili, Wakati wa Mwinyi ndipo tulipoanza kuona ulanguzi, wakati wa Mwinyi msomi hakuwa na maana zaidi ya mfanyabiashara, wakati wa Mwinyi ndipo tulipojua kuwa yeye ni fataki kwa kuoa binti wa Jangwani.........Listi haiishii hapo. Huwezi ukamsifia Mwinyi na wenye akili wakakusikiliza kimsingi Mwinyi hakuwa na guts alikuwa mdhaifu , mdini mwenye kuupiga vita Ukristo. Na ndio yeye aliyemtoa Muungwana kwenye jua kali ndio maana anamuheshimu kwa sababu ya Udini wake na sio utendaji wake. Tukubali tukatae.