Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri![/I]............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God


Bila kusahau ukatende mema, nafikiri hii haina shida kama kule kwa kakobe ambako anathubutu kusema kuwa wakati wa yesu umepita na sasa ni wakati wa kakobe, je inamaana yeye ni sawa ya yesu?
 
Kwa kweli huyu Mtume na Nabii anonekana kumkose hata huyo Mungu wake, yaani analaaani ili huduma hiyo ife na Babu afe. Mwngira hana uwezo wa kuumba binadamu kwa maana hiyo hana ruhusa ya kumwombea mabaya huyo binadamu, kama kweli hiyo dawa ni ya uwongo amwachie Mungu mwenye utaratibu mzuri itajulikana tu, na sio kujidai kumshauri Mungu cha kufanya.

Hatahivyo, ingawa Babu ni mchungaji mstaafu wa KKKT, sijaona kama huyo anatoa dawa kwa kuwalazisha wagonjwa kwa imani ya dhehebu hilo. bali kila mtu kwa imani yake kwa Mungu.
 
Mimi najiuliza ni kwanini hawa viongozi wa dini wanapinga mambo ya kiimani huku hata wao wakihubiri majukwaani mambo ya kiimani ambayo ni vigumu kuyathibitisha kisayansi. Inanisikitisha Mwingira kumlaani Mwasapile kisa eti anawatoza watu Tshs500 kwa huduma anayotoa, mbona yeye anawatoza watu wake sadaka?
 
si sahihi kuhalalisha ya babu kwa vile wengine pia kama kakobe, mwingira nk nao wanafanya. tupeni support ya kimaandiko please
 
Mwingira anaona sasa deal linaharibika badala ya watu kwenda kwake kanisani wanakimbilia kwa babu.
Inatakiwa kufahamu kuwa mtu huponywa huku akisaidiwa na imani na watu ama wagonjwa hawawezi kupona kwake kama hawana imani naye na hili linashuhudiwa na mitazamo tofauti binadamu waliyonayo huyu kakobe, huyu assembles of God mwingine katoliki mara Mzee wa upako yoye kwa yote ni imani na amani ya roho amabayo mtu anadhani akiabudu hapo ataipata na kukua kiroho.
 
...Babu Mwasapile huiombea ile dawa kabla hajawanywesha watu wake. Zaidi ya hapo, kitu gani hawa watumishi wa Dar wanachotaka kutuaminisha? Itanichukua miaka mingi sana kuwaamini na kujiunga na watumishi 'maslahi' waliojazana Dar, ambao hujali maslahi yao zaidi kuliko ya waumini wao masikini wa kutupwa. Kakobe, Mzee wa Upako, Mwingira and the like, hawajawekeza hata kwenye shule ya chekechea kutokana na sadaka zao, hawana udhu wa kumkandia mchungaji Mwasapile kwa kuchukua shilingi 100/- katika kila 500/- wanayolipa wagonjwa.
 
MAONI YA WASOMAJI WA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU MWINGIRA



Mhifadhi 2011-03-16 06:17
Tena la kushangaza muumini huyu wa Moshi alikuwa na cheo kikubwa sana ktk kanisa na inasemekana kwa uhakika kuwa Mheshimiwa Mtumishi mkuwabwa wa Mungu nabii na mtume alimtembelea mara kwa mara kwake kiboriloni na kumsisitiza kutokunywa dawa wala kuhudhuria hospitali maana uponyaji ungeshuka? Sasa watu wanaweza kuamini kuwa ile mali ndo iliyomsukumiza aishie ili tujimilikishie
Quote







http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #7 elibariki yerald 2011-03-16 05:27 PIA WEWE MWNGIRA UANFIKIRI BABUA ATAKULA WAPI NA YEYE HIYO NI HUDUMA NI SAWA NA BURE KABISAAAA.

HAJAWAITA WATU LOLIONDO NA WALA HAJWALAZIMISHA? WAMEENDA KWA HIARI YAO,, NA WATU WALIOKUFA WALIKUWA MAHUTUTI KOSA NI LA BABU?....

UNAFIKIRI WATU WASIPOTOA HELA YA MOTISHA BABU AKALE WAPI AU AKALE POLISI? ATAKULA VYA MADHABAHUNI KAMA HUDUMA YAKE INAVYOMURUHUSU..

SIKU ZA MWISHO NDIO HIZI MNAHANGAIKA NA MANABII WA UONGO UTAWAONA KWA MATENDO YAO NA SI KWA MANENO...

PIA SIKU ZILZOPITA NILISIKIA KUNA MTUMISHI, SIJUI MUUMINI WAKO HUKO MOSHI ALIKUFA KWA KUKATAZWA KUNYWA DAWA NA AKAFARIKI NASIKI KWA KANUNI AKIFARIKI MALI ZAKE LINACHUKUA KANISA?!!!! HAA HIKI NI KICHEKESHO............HIVI NANI NI MWIZI NA MUONGO HAPO NDIVYO YESU ALIVYOSEMA HAPANAAAAAAAAAA AAAAAAAA! HAKUNA SEHEMU KATIKA BIBLIA IANSEMA HIVYO TOKEA MWANZO HADI UFUNUO.......HEHEHEHEHEHEHEH EHEEEEEEEEEEEEE EEEEE UNACHEKESHA SAAAAAAAAAAAANA AAAAAAAAAA!!1

Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #6 elibariki yerald 2011-03-16 05:12 HUYU MWINGIRA NI [NENO BAYA] KABISAAAAAAAAAA A, MBONA YEYE AMELAZIMISHA WAUMINI WAKE WAMETOA MAMILIONI YA FEDHA KUJENGA KANISA LAKE PALE MWENGE, NA PIA KUANZISHA BENKI Y AEPHATA SAS NANI ALAANIWE? HUU NI UHUNI. JE, BENKI INAFANYA KAZI KWA FAIDA AU HASARA KAMA ANA SEMA MCHUNGAJI NI MWONGO NA YEYE AWAAAMBIE WAUMINI WAKE WASITOE SADAKA HAYO SI MALIPO BWANA ,,KWANI KWA BABU 500 SI SADAKA YA KUTENGENEZEA DWA NA WATOA HUDUMA?

PIA BENKI YAO YA EPHATA WATOE MIKOPO BURE KAMA NI HUDUMA YA MUNGU? ACHA UNAFIKI NA UZANDIKI...NA WEWE USITEMBELEE GARI ZAKO ZA KIFAHARI HIZO FEHDA UMEPETA WAPI? PIA NA SHAMBA KUBWA LA EKERI ULILONUNUA PWANI ULIUZE KWA WATU WASIO NA ARDHI..NAJUA TUU NYIE WATU WA MADHEHEBU YA KIPENTEKOSTE SIKU ZOTE MNAJIFANYA NYIE NDIO MMMEOKOKA SANAAAAAAAA KULIKO NA WENGINE NA NYIE NDIO MTAKWENDA MBINGUNI..NIMELIONA HILO WAKATI NIKO SEKONDARI NA HATA CHUO KIUKUU,,HUWA WANASEMA WAO NDIO WATAKWENDA MBINGUNI SISI WENGINE HATUJAOKOKA TUKUTAKA OKOKA TWENDE KWAO HUOO NI UJUHA....

NENO LA MUNGU LINASEMA"ALIYESIMAMA AANGALIE ASIJE ANGUKA" PIA KWA KWANZA ATAKUWA WA MWISHO NA WA MWISHO ATAKUWA WA KWANZA" SIO HIVYO TU KUMBUKA YA ZAKAYO..PIA YULE MWIZI ALYEOKOLEWA NA YESU MSALABANI.....LA ZIADA PIA YULE MAMA MJANE ALIYETO SENTI TANO NA YESU AKAMBARIKI KWASABABU ALITO KWA DHATI..

KAMA WEWE NI MTU WA MUNGU TOENI SADAKA ZENU ZOOTE KWA MASKINI WANOKUFA KWA NJAA, MAYATIMA WANOKOSA ADA, NA OMBA OMBA WOTE WA DAR-ES-SALAAM NAFIKIRI WENGINE WAPO HAPO MWENGE NA KILA SIKU UNAWAONA WAMEONGEZEKA SANA SIKU WANAKAA HADI KARIBU NA KANISA LAKO....JE, UMEWASAIDIA?

KIFUPI NI KWAMBA HATA WAUMINI WAKO WAMEENDA KULE KAMA HUJUI..USHAJIONA WEWE KAMA UANWAMILIKI WATU.HUNA HATIMILIKI NI MUNGU TUUUU..NA BABU 200 ANTOA KANISANI,,200 NYINGINE KWA WACHIMBA DAWA,INAYOBAKIA 100 NI YA KWAKE ,JE,HAPO UTASEMAJE? KULIKO WEWE UNAYESEMA FUNGU LAKUMI NA SADAKA NYINGINE KIBAO..JE, BABUA NAYE ANGESEMA KILA ANAYEKWENDA ATOE FUNGU LA KUMI LA KPATO CHAKE MNGESEMAJE?..ACHA UZUSHI ACHA KUPOTOSHA WATU

BABU SONGA MBELE HUDUMA HIYO SI LELEMAMA..HAO WATU WAMEKOSA FEDHA ZA MATAJIRI AMBAO HUENDA KWAO KUWAOMBEA NA KUAHIDIWA MAGARI NA SASA WANATAPATAPA..ALUTA CONTINUA........

Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #5 Mhifadhi 2011-03-16 05:03 Pole sana Nabii na Mtume Mwingira. Kama huyu babu wa Loliondo anadanganya ni vivyo hivyo kama nawe unavyowadangany a wengine. Wewe walioko chini yako hawafi? Kuna mmoja alikuwa chini yako mtumishi mzuri wa Mungu kule Moshi alifariki mwezi uliopita baada ya kudanganywa kuwa hakukuna na haja ya kunywa dawa, je hiyo haikuwa kuwadanganya watu? Na leo inasemekana mali zake zitakuwa za kanisa? ni kheri hata zingepewa masikini walio wengi ktk mji ule kuliko kulipa kanisa hilo ambalo limechangia kifo chake. Basi waache na wengine nao wajaribu maombezi yao kwa kadiri ya karama walizopewa. Hii ni woga tuu wa kukosa wafuasi. Wewe unahofu gani kama kweli wewe unajiita mapkwa mafuta wa bwana una wasiwasi wa nini? Mungu atakuinulia waumini ktk mawe ama umepungukiwa imani Nabii Mtume? Hii swala la kulaani mtumishi mwema, Nabii Mtume ulilitoa wapi wakati biblia inatuamuru kuzivunja laana na kuto kulipa ovu kwa ovu? sasa unaonyesha kuwa unayotufundisha siyo unayoyaishi. Hapa nina wasiwasi wewe na Kakobe this time mtayafunga makanisa. Hukumbuki hata wana wa Israeli waliwahi kuambiwa kumuangalia nyoka wa shaba jangwani ili wapone? japo Mungu huyo huyo hakutaka mwanadamu ajitengenezee sanamu wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni wala duniani? yachambue maandiko Mtumishi mwema, Nabii and Mtume
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #4 ksm 2011-03-16 03:24 wewe unaejiita nabii ni tapeli. huwezi kumuombea mtu alaaniwe kwa kutoa huduma kwa gharama. Yaani sh 500 we umeona ni gharama? inasemekana anatoa fungu la kumi sh 200 kwa kila 500 anayoipata, mia mbili anawapa wachimba dawa, mia nu yake. sasa hiyo si ni huduma ya bure kabisa. wewe ungeipata hii dawa si ungeacha kabisa na kanisa na ukaanza kupiga ramri. usirubune waumini wako.
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #3 prisca 2011-03-16 03:20 we mwingira acha hizo mbona wewe wanaotoa sadaka kubwa ndio huwa wanakaa mbele kanisani???????????? hebu usitutie kichefuchefu hapa,mnaponya kimazingaombwe na ndio maana magonjwa hayaishi,honger a babu loliondo
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #2 Ozzie77 2011-03-16 02:38 Heri Pengo anakemea ufisadi sana, lakini Askofu Mwingira anaona hili ni kubwa kuliko kukemea ufisadi. Watu wamekata tamaa, maisha magumu, wanahitaji matumaini. Kemea mafisadi kwanza ndipo anza na hizo imani zinatishia kupunguza waumini wako.
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#http://www.mwananchi.co.tz/habari/51-habari-nyingine/10118-mwingira-amlaani-mchungaji-loliondo#0 #1 Yona 2011-03-16 02:35 aache unafiki mbona yeye anakusanya hela kwa watu masikini na kujilimbikizia utajiri? kinachomuuma ni kwamba watu kwake wameanza kupungua

mwignira huyu huyu
ametangaza watu wa vitongojo...,anakusanya sh 3000 kwa kila mtu na kati kati wanapitidhas michango kiba imagine wewe kanisa lina w\atu zaidi ya laki2 na anakusanya sh 3000 kila mwezi wacha michango ya kati halafu mbaya zaidi anawaatishia viongozi make sure unamfwata muum mini mpaka anapokaa sidhan kama n haki..m nilikuwa mhudhuriaji mzuri wa ibada za jion nilipoona hayo nimebaki kuishia jumapili..kati kati namfwata mungu kanisa zingine...nafikiri ajaiulize huyu babu anaponya watu kwa 500 yeye amefanya nini kwa hiyo 3000 zake..na siku hizi kila siku kanisan anaanza na neno la mungu la sadaka na zaka usipotoa utalaaniwa wwewwe nakwambia mara iki mara kile huyu ambilikile wangemleta dar akika akuna angesali makanisa kama ya mwingira..mwingira jiangalie ujisafishe kwanza wanasema atutakiwi kumgusa masihi wa mungu kwa kuwa wewe umemgusa wacha na sie tukuguse maovu yako
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kama kuna mwumini anaenda kwa huyu shetani mwingira kwa matumaini ya kuona uzima wa milele ajue amepotea.mwingira ni kibaka tu wa neno la mungu na katu hana mamlaka ya kulaani au kumzuru mtu.hakuna mchungaji au askofu anaweza kusimama kwenye kanisa la mungu na kutoa maneno maneno ya laana kama anavypfanya huyu nabii uchwara.amefilisika kiakili na kifikra.tumsamehe tu huyu maana hajui alinenalo.kuna siku hili kanisa la dhuluma litawaka moto na kupotea kabisa maana halina baraka yoyote ya mungu ila uchu wa kujikweza nakujilimbikizia mali.mwulize mwingira hicho kiwanja alichokiiba na kudhuluma ili apanue kanisa lake hapo mwenge kweli alitumwa na mungu?yeye mwenyewe ni msafi wa roho?watu wanaomfahamu wasingeweza kusali kwenye kanisa hilo
 
si sahihi kuhalalisha ya babu kwa vile wengine pia kama kakobe, mwingira nk nao wanafanya. tupeni support ya kimaandiko please

Hizi kweli ni zama za kina Tomaso ni maandiko yepi Musa aliwapa wanawaisrael ili kuwaconvice wamgeukie yule nyoka wa shaba. Ni ruksa kuijaribu roho unayokuwa unawasiwasi nayo lakini ni vibaya kuongea ilikujaribu kuwashawishi wengine waamini kama uaminivyo.

Sijahalalisha kazi ya babu lakini sina haki ya kupinga afanyacho zaidi ya kuwa na shauku ya kuona moja ya ninaowafahamu anapona kwa kutumia dawa ya babu ili ni confirm kazi ya babu ni kweli au si kweli.
 
Natoa angalizo kwa kauli tunazo zitoa kwenye vyombo vya habari kuhusu babu anayetibu kwa kunywa maji,tunachohitaji ni taifa la watu waliopona, suala la ghalama la malipona ,hata yeye anahamasisha kutoa michango tena mingi ,mwingila ameanzisha benki,anashule yote hii waumini wamechanga eiza ni sadaka au michango na ufadhili mbalimbali lakini kwa babu unatoa tsh 500 tu,zaidi naambiwa anaigawa kuipeleka kwenye vyombo vya wumini tofauti.pia hivyi kuomba hadi upayuke au ushike biblia hebu soma mathayo anasema uombapo ingia chumbani ukaonge na mungu wako wa sirini kwa siri ,hivyo sio lazima upayuke ili ujulikane umesema yesu.pia lazima tujue utendaji kazi wa mungu na ndiyo maana anayeshea mvua watu wote bila kujali watenda dhambi au dini .wazima au wagonjwa.
 
alafu siku hizi kama umemsikia ameanza kutishia watu wanaohama kanisan kwake ati nakwambia wewe ulieenda uko upati kitu kama mungu wa MWINGIRA amekuandalia mwingira utaruka koteeeeeeeee
jamani kuna Mungu wa ambilikile wa mwingira..huyu MUNGU wako wangapi..majuzi nilienda na mdogo wetu mmoja anasali DPC kinondoni alisema mwanzo na mwisho kumpeleka pale..alipofika akaanza kukandia na nyie mnaokimbia makanisa yenu kukimbilia ibada za EFWATA nawaambia mmepoteza muda wenu hapa baraka natoa kwa wana efwata tu hata ukae mpaka saa moja..nikaona watu wanaanza kuondoka kichekecho ati kuna walinzi wamefunga mlango akuna kutoka mpaka amalize ibada..sasa kama akuna baraka mnangangania watu wabaki kanisan wa nini???waachen watu wawe huru usibague makanisa MCH MWINGIRRA HUU SIO MUDA WAKE....muwen na upendo na amani na si Kujiona huyu zaidi mimi zaidi amtafika kumbukeni lengo lenu ni kusudi la MUNGU litimizwe lakini naona WACHUNGAJI WENGI SASA WAMEKUWA ZAIDI YA MAGUFULI WANATAFUTA UMAARUFU WAO BIINAFSI BADALA YA KUTAFUTA SIFA ZA BWANA YESU

WENU
MTUMISHI/KANISA LA MWINGIRA
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God

Mungu anapewaje?utukufu hapo? Utukufu nikutenda mema yanayompendeza mngu jee? Babu kuponya sikaziyakumpendeza mngu? mwingira sikaziyake kuhukumu wakuhukum ni mngu anayejuwa kuwa mwingira anatumia ni rohoyakweri nani? Au babu katumwa namngu wakujuwahayoyote ni mngu siyo mwingira
 
Mchanganuo wa pato la babu, katika Tshs 500 anayokusanya kwa kichwa

Tshs 200 - Wachimbaji na wabebaji kutoka porini wa dawa
Tshs 200 - Anapeleka kanisani
Tshs 100 - Hii ndio ya babu.

Source ni moja ya watu waliomhoji Babu kuhusu pato lake.

Watu wanahoji haya kama Mwingira lakjini ikumbukwe babu kwa sasa anafanya hii kazi almost 24/7 je wanadhani akale wapi pili mwingira mwenyewe anapata mshahara kama anaona ni batili akatae mshahara na marupurupu yote. Kakobe yeye anawalazimisha wafanyakazi wapeleke Salary Slip ili aweze kujua fungu lako la kumi pamoja na kujua kama unamuibia mungu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kaazi kweli kweli. Sadaka anapata ngapi kwa kila misa yeye hapo alipo??? Anazipeleka wapi??? Kwa nini anatembelea magari na sio Punda kama Yesu??? Duniani kuna vituko kweli kweli. Huduma kapewa mwingine, maelekezo kapewa mwingine, yeye anazuka anajua mkataba wa mtu huyo na Mungu akitaka ulingane na jinsi Mungu alivyomwita yeye!. Mie simo kwenye kunyooshea wengine vidole, nirekebishe yangu kwanza na Mungu - kila mtu atasimama mwenyewe siku ya hukumu. :car:
 
mbona topic haindani na maelezo uliyoyatoa? tujuze huyo nabii mwingira kasemaje kuhusu mchungaji babu ktk vyombo vya habari sio ishu ya yeye kua na benk au kumiliki shule.
 
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God

MISS JUDITH = kakobe = MWINGIRA
 
Aache wizi nae Mwingira, basi na yeye asingekusanya michango kanisani. Tena kwa kupanga watu kwa mafungu ili wanaotoa sana waonekane! Haya makanisa mengine biashara tupu.

Wale vijana wa babu wanaoenda kumtafutia dawa wataishije? Umeona nyumba anayoishi babu? Yeye yake ni 100 kati ya 500 bado mnaona anapata nyingi?

Kweli mashetani ni wengi humu duniani,tutaishi na kuona mwisho wenu..

Mbona yeye anapokea sadaka na zile account anazo pitisha za nn?
 
Back
Top Bottom