Mwimbaji Dar Modern akimbiwa na waifu wake!

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615

Muimbaji wa vidole juu toka Kundi la Dar es Salaam Morden Taarab (pichani chini), Hashimu Said, amedaiwa kukimbiwa na mkewe, Zainabu Omary, Amani linashuka nayo.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Amani, mke wa Hashimu alianza kusikia habari za mumewe kuwa ‘klozi’ na wanaume wenye ‘tabia chafu’ kitambo ambapo alimkanya mumewe lakini jamaa huyo alimjibu kuwa ni maneno ya wakosaji waliolenga kurudisha nyuma maendeleo yake.

Kihabarishi hicho kilibainisha kuwa, tangu aunyake mchongo huo, ‘waifu’ huyo wa jamaa amekuwa akihoji uhalali wa taarifa hizo hivyo kuibua malumbano miongoni mwao.

Kikaendelea kusambaza umbeya kuwa, baada ya kufanya utafiti na kutia majibu kibindoni, Zainabu aliamua kufunga virago na kuelekea nyumbani kwa wazazi wake jijini Tanga kwa lengo la kwenda kusaka ufumbuzi wa suala hilo.

Baada ya kuzinyaka ‘nyiuzi’ hizo, Amani lilimwendea hewani Hashimu kupitia simu yake ya kiganjani ili kujibu mapigo ya ishu hiyo ambapo mbali na kukiri alisema kuwa ana imani mama watoto wake huyo iko siku atarejea.

“Ni kweli mke wangu kanikimbia, yuko kwa wazazi wake Tanga, kama alikuwa anafanya utafiti juu yangu, basi majibu aliyoyapata siyajui, nina imani akifanya uchunguzi zaidi atarudi tu nyumbani,” alisema Hashimu kwa masikitiko makubwa ya ‘kummisi bebi’ wake.
 
.....Hwa wa vidole juu huwa nawachukia sana. Utakuta dume zimalinakatika mauno,eti yuko kazini mi nadhani wengine ni mibwabwa!!
 
Macho yake yanaonyesha mtoto si riziki.
 
Huwezi kuwa unaimba nyimbo za kurembua af wadau wasikutafute.....wateja wao asilimia kubwa ni wanawake na mashoga....

Wadau em tupeni majina ya waimbaji wa taarabu ambao si rizki...
 
Sioni kuwa ni busara kumwita jamaa huyo majina ambayo yanaashiria kuw ni @()*%. Ndoa hasa kwa wanawake wa pwani na akikuchoka atakupaka sifa mbovu nyingi na hata yeye mke kutangaza kuwa watoto siyo wa mume. Kwa maoni yangu ni matatizo ya ndoa na mwisho wa siku mtashangaa kufahamu kuwa mambo si kama mnavyofikiri sasa sijui mtasema nini. Hii tabia ya kunukuu magazeti ya udaku na kuleta jamvini kunaipunguzia hadhi JF ambayo kutokana aina ya michango kutoka kwa wanajamii imevuta wengi. Sasa naona vitu vya ajabu vinakuwa posted mwishowe JF itakuwa haina maana.
 
Back
Top Bottom