Mwili wa mtoto mkiristo wafukuliwa

Status
Not open for further replies.
[h=2]Mtafaruku wazuka makaburini Bagamoyo[/h]

Na Mwandishi wetu

4th October 2012

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Mtafaruku umezuka Wilaya ya Bagamoyo baada ya watu wanaodhaniwa kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wa msikiti wa Majani Mapana kuvamia makaburi ya kiislamu ya Tandika Kata ya Magomeni kwa lengo la kutaka kubomoa kaburi moja la mtoto Aruina Rolan Mitaban.

Watu hao walitaka kubomoa kaburi hilo wakidai kuwa mtoto aliyezikwa katika makaburi hayo ni Mkristo, hivyo haruhusiwi kwa kuwa si muumini wa dini ya Kiislamu.

Tukio hilo limetokea juzi wa Jumapili na waumini hao baada ya kulibomoa kaburi hilo, waliwataka ndugu wa marehemu kufukua mwili wa mtoto huyo kabla wao hawajachukua hatua za kufukua.

Walisema kitendo cha Wakristo kwenda kuuzika mwili huo katika makaburi hayo na kuujengea kwa marumaru na kuweka msalaba ni uchokozi kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.

Kipozi aliwataka waumini wa dini zote mbili kujenga tabia ya kuvumiliana wanapokuwa na matatizo badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.

Mwili wa mtoto huo baada ya kufukuliwa na ndugu wa marehemu walikwenda kuuzika upya jijini Dar es salaam.

Aidha, alisisitiza kuwa viongozi wa dini hizo wahakikishe wanasiliana na ofisi yake ili kushughulikia matatizo kama hayo mara moja yanapotokea.

“Nawapongeza ndugu wa marehemu kwa watulivu na kuamua kufukua kaburi la ndugu yao bila kuleta pingamizi, hawa wameonyesha uzalendo wao wakuitakia nchi yetu amani iliyopo isitoweke,” alisema.

Baadhi ya ndugu wa marehemu huyo walisema kitendo kilichofanywa na waumini hao si kiungwana kwani kama kulikuwa na tatizo iliwapasa kwenda kuwataarifu badala ya kusambaratisha kaburi hilo.

CHANZO: NIPASHE
 
Swali kabla hujaswaliwa... huyo maiti anafahamu nini mpaka watu wanajisumbua namna hiyo?
 
ndugu zanguni waislam tupendane, dunia tunayoishi ni moja. Imenisikitisha sana hii ni kukosa elimu au chuki binafsi, siamini km Quran tukufu imeagiza haya mambo!
 
Tatizo la wakristo wa bongo ndiyo hilo, hadi leo hawajui kuwa waisilamu hawajaribiwi. oneni sasa baada ya uchche wa busara munazika Bagamoyo na dar maiti moja. si mtu akikunyang'anya kaburi la kichanga unampa na kaburi la babu yake alibomoe vile vile tatizoliko wapi?
 
hawajaribiwi (NI UNTOUCHABLE HAO!)NJOONI KWA YESU JAMANI,FULL SHANGWE NA AMANI ILIYOTUKUKA!
 
Inaeleka hilo eneo linaikwa waumini wa dini ya kiislam na wakristo walikwenda kumzika mtoto wao nae mkristo
Tujiulize kwani hakuana maeneo yanayo zikwa waumini wa dini ya kikristo kwenye mji wa Bagamoyo...Niliwai kuona kule Mission kuna eneo kubwa tuu la maziko ya wakristo sasa ilikuaje wakazike eneo la waislama si kama kumpeeb Kova kwenye maandano yasiokuwana kibari
Sasa wamekwenda kusambaratisha kabuli na wafiwa hao wamekwenda kuzika Dar-Mda mwengine wanawaambia waislam wakorofi kumbe zengwe linaanzishwa na wengine
 
Bumpkin Billiionare ulitaka kumaanisha nini? Maana sijakuelewa zaidi ya kuona maswali yasiyo na majibu.
 
Wakristo tumepewa amri kuu 'pendaneni kana kristo alivyotupenda'
Mungu ni mwema kweli laiti hawa ndugu zetu wangepewa utajiri wa mashule hospitali vyuo mabenk na makampuni kama tulivyopewa sisi maisha yangekuwa magumu Tz zaid ya tuonavyo allah amewakirimia moyo wa ubaguzi na kisasi after all sisi ni waTz am so proud to be CHRISTIAN am so happy JESUS CHRIST is in me!
 
Inaeleka hilo eneo linaikwa waumini wa dini ya kiislam na wakristo walikwenda kumzika mtoto wao nae mkristo
Tujiulize kwani hakuana maeneo yanayo zikwa waumini wa dini ya kikristo kwenye mji wa Bagamoyo...Niliwai kuona kule Mission kuna eneo kubwa tuu la maziko ya wakristo sasa ilikuaje wakazike eneo la waislama si kama kumpeeb Kova kwenye maandano yasiokuwana kibari
Sasa wamekwenda kusambaratisha kabuli na wafiwa hao wamekwenda kuzika Dar-Mda mwengine wanawaambia waislam wakorofi kumbe zengwe linaanzishwa na wengine

Makaburi ya Kinondoni (haya ya juu baada ya shule ya Muslim) yana mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo lkn sijawahi hata siku moja kusikia marehemu mmoja katoka na ku-complain kwa nini jirani yangu ni wa dini tofauti.

Wewe nyoosha maongezi nini tatizo. Meli ilipozama baharini miili iliyoharibika uliwahi kuona inagombana sababu ya dini?

Shida ni kukaa na mutu ya Yesu, mnajua ibada za matambiko zitafeli. Itafikia mahali tutakuwa hatuzikani kwa mtindo huu
 
P Billionare nimekuelewa kuwa kumbe najadiliana na mtu ambaye kuna tatizo upstairs. Thanks hata hivyo, kwa halil yako, umejitahidi sana.
 
Makaburi ya Kinondoni (haya ya juu baada ya shule ya Muslim) yana mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo lkn sijawahi hata siku moja kusikia marehemu mmoja katoka na ku-complain kwa nini jirani yangu ni wa dini tofauti.

Wewe nyoosha maongezi nini tatizo. Meli ilipozama baharini miili iliyoharibika uliwahi kuona inagombana sababu ya dini?

Inshu kwa mujibu wa vyanzo vya habari-Hilo eneo waliozikwa hapo ni waislam na kuna eneo lengine kubwa linazikwa wakristo,,Tofauti na Dar eneo la Kinondoni-Ukubwa wa jiji umefanya watu kuzikana eneo moja kama (Kinondoni)
 
Tatizo la wakristo wa bongo ndiyo hilo, hadi leo hawajui kuwa waisilamu hawajaribiwi. oneni sasa baada ya uchche wa busara munazika Bagamoyo na dar maiti moja. si mtu akikunyang'anya kaburi la kichanga unampa na kaburi la babu yake alibomoe vile vile tatizoliko wapi?

Kwa hiyo kwa akili yako unaona wameshinda saaana wale? Vile ni vita vya roho. Kuna mambo ambayo hamyajui na kamwe hamtaambiwa. Kwa akili yako unaona jibu lilikuwa kupigana, lkn kwa wenye busara zao suala lilikuwa ni kuhamisha tu mwili wa huyo innocent, ili usiharibu mipango ya watu.

Kuwa huru sasa kwenda kuvunja mayai na nazi pale
 
Makaburi ya Kinondoni (haya ya juu baada ya shule ya Muslim) yana mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo lkn sijawahi hata siku moja kusikia marehemu mmoja katoka na ku-complain kwa nini jirani yangu ni wa dini tofauti.

Wewe nyoosha maongezi nini tatizo. Meli ilipozama baharini miili iliyoharibika uliwahi kuona inagombana sababu ya dini?

Shida ni kukaa na mutu ya Yesu, mnajua ibada za matambiko zitafeli. Itafikia mahali tutakuwa hatuzikani kwa mtindo huu
Inshu kwa mujibu wa vyanzo vya habari-Hilo eneo waliozikwa hapo ni waislam na kuna eneo lengine kubwa linazikwa wakristo,,Tofauti na Dar eneo la Kinondoni-Ukubwa wa jiji umefanya watu kuzikana eneo moja kama (Kinondoni)
 
Mtafaruku wazuka makaburini Bagamoyo

Na Mwandishi wetu

4th October 2012

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Mtafaruku umezuka Wilaya ya Bagamoyo baada ya watu wanaodhaniwa kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wa msikiti wa Majani Mapana kuvamia makaburi ya kiislamu ya Tandika Kata ya Magomeni kwa lengo la kutaka kubomoa kaburi moja la mtoto Aruina Rolan Mitaban.

Watu hao walitaka kubomoa kaburi hilo wakidai kuwa mtoto aliyezikwa katika makaburi hayo ni Mkristo, hivyo haruhusiwi kwa kuwa si muumini wa dini ya Kiislamu.

Tukio hilo limetokea juzi wa Jumapili na waumini hao baada ya kulibomoa kaburi hilo, waliwataka ndugu wa marehemu kufukua mwili wa mtoto huyo kabla wao hawajachukua hatua za kufukua.

Walisema kitendo cha Wakristo kwenda kuuzika mwili huo katika makaburi hayo na kuujengea kwa marumaru na kuweka msalaba ni uchokozi kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.

Kipozi aliwataka waumini wa dini zote mbili kujenga tabia ya kuvumiliana wanapokuwa na matatizo badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.

Mwili wa mtoto huo baada ya kufukuliwa na ndugu wa marehemu walikwenda kuuzika upya jijini Dar es salaam.

Aidha, alisisitiza kuwa viongozi wa dini hizo wahakikishe wanasiliana na ofisi yake ili kushughulikia matatizo kama hayo mara moja yanapotokea.

"Nawapongeza ndugu wa marehemu kwa watulivu na kuamua kufukua kaburi la ndugu yao bila kuleta pingamizi, hawa wameonyesha uzalendo wao wakuitakia nchi yetu amani iliyopo isitoweke," alisema.

Baadhi ya ndugu wa marehemu huyo walisema kitendo kilichofanywa na waumini hao si kiungwana kwani kama kulikuwa na tatizo iliwapasa kwenda kuwataarifu badala ya kusambaratisha kaburi hilo.

CHANZO: NIPASHE

Binafsi sijaona mantiki ya kwenda kuzika ktk makaburi ya binadamu wenye imani tofauti na ya kwako ilhali sehemu za kufanya maziko zipo. Sielewi!

*Wavamia makaburi ya Wakristo,DC ashangaa
*Kaburi lafukuliwa, mwili wazikwa upya Dar

KUNDI la waumini wa dini ya Kiislamu (Mujjahidina), kutoka Msikiti wa Majani Mapana Tandika, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, limefanya vurugu kubwa baada ya kuvamia makaburi ya Kiislamu na kutaka kaburi alilozikwa mtoto Aruina Rolan Mitaban lifukuliwe.
Waislamu hao, ambao walionekana kujawa na jazba, walidai mwili wa mtoto huyo, hauruhusiwi kuzikwa katika maeneo yao, kwa sababu ni Mkristo.
Tukio hilo lilitokea Septemba 30, mwaka huu, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuzikwa kwa mwili wa mtoto huyo, katika makaburi hayo.
Tukio hilo, limeonekana kuibua hisia kali kwa wakazi wa Bagamoyo, ambao miongoni mwao walidai huo ni unyama wa kupindukia.
Haiwezekani kaburi la mtoto kama yule, malaika wa Mungu asiyejua kitu, linakwenda kufukuliwa kinyama vile nadhani tunakoelekea ni kubaya sasa, alisema Suleiman Wahid.

Huwezi kusambaratisha kaburi namna hii, ilitakiwa wakutane na viongozi wa makaburi kwanza, marehemu yule ana kosa gani? Watanzania tunapotea, alisema Wahid.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, aliamua kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha dharura ili kujadili.
Baada ya kuitisha kikao hicho, aliziita pande mbili zinazohusika, ilikupata ufumbuzi wa suala hilo.
Kipozi aliwataka waumini wa dini hizo na wakazi wa wilaya hiyo, kujenga tabia ya kuvumiliana pale kunapokuwa na matatizo, badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.
Mara baada ya kikao hicho cha kamati ya ulinzi na usalama, upande wa marehemu huyo wakiongozwa na baba wa marehemu, Rolan Mitaban, Oktoba 2, mwaka huu walilazimika kwenda kufukua mwili huo wa marehemu na kwenda kuuzika upya jijini Dar es Salaam.
Tukio hili limetokea, nikalazimika kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama, na pande zote zinazohusika.
Moja ya maazimio tuliyokubalina ni kwamba, kaburi lile lisibughudhiwe na mtu yeyote na ndugu zao walijengee kama yalivyojengewa makaburi mengine.
Lakini katika hali ya kushangaza, nimesikia jana baba mzazi wa marehemu akiwa na ndugu zake, waliamua kwenda kufukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika Dar es Salaam, alisema Kipozi.
Kutokana na tukio hilo, DC Kipozi alitoa wito kwa viongozi wa dini, kuhakikisha wanawasiliana na ofisi yake, ili kushughulikia matatizo ya aina hiyo yanapojitokeza, ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea.
Baadhi ya ndugu wa marehemu, ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema kitendo kilichofanywa na waumini wa dini ya Kiislamu si cha kiungwana, kwani kama kulikuwa na tatizo hilo, walipaswa kuwataarifu wahusika ili waweze kwenda kushughulikia kwa kufuata sheria.
Hii ni mara ya pili kutokea kwa vurugu katika makaburi ya Tandika, itakumbukwa mwanzoni mwa mwaka huu, kuliibuka uvumi kuwa kuna joka kubwa la kishirikina katika makaburi hayo nakupelekea mganga wa kienyeji maarufu Zoazoa, kwenda kuweka matambiko ambayo hayakuzaa matunda.

My take:
hao wajahidina wenye chuki zakidini wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria, pasipo kuwaonea haya

source :mtanzania 04/10/2012
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom