Mwigulu Nchemba: Tuhuma dhidi yangu hazina ukweli wowote

Great thinkers heshima kwenu! Sikuhizi baadhi ya watu wamekua na kasumba ya kutuhumu wengine kwa lengo la kuwapaka matope mbele ya jamii huku wakujua dhahiri kwamba tuhuma hizo nizakuzusha tu. Mimi ni mwana-Iramba na imenilazimu kujibu tuhuma za uongo, zilizotolewa na Patriq kuhusu Mh. Mwigulu Nchemba.

Mimi namashaka sana kama Patriq yuko hapa Iramba, otherwise asingekuja na siasa hizi za majitaka. Personally, nimewasiliana na Mh. Mwigulu na ameonesha kushangazwa sana madai haya. Pamoja na kwamba ilimlazimu Nchemba kujibu madai haya hapa jamvini,(Gonga hapa na usome post #20 https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-jimboni-spesho-kwa-wanairamba-magharibi.html) lkn bado nimeona nisiliache hili jambo lipite hivi hivi. Mbunge alikuwepo jimboni mwezi April na kama kweli Patriq alikuwepo basi angekua anafahamu hili kwani tuhuma hizi alizitoa tarehe 30 April siku chache baada ya ziara ya mbunge.

Mbunge alifanya ziara katika maeneo yafuatayo:- Tarehe 23/04 alikuja Ng’anguli na Maluga Tarehe 24/04 alikuwa kitusha na Uwanza Tarehe 25/04 alikuwa Galangala na KBI ambapo alizunguka sokoni akiongea na vijana pamoja na watu wa rika mbalimbali kuhusu njia bora ambayo wangependa kuwezeshwa katika ujasiriamali wao.

Mbunge pamoja na kwamba Chama kimempa majukumu ya kutunza fedha za chama ambayo kwake ni mepesi kutokana na taaluma yake ya uchumi na uzowefu wake pale BOT bado ameendelea kuwa pamoja na wanachi wake na imani yake kwa wana-Iramba bado iko juu.

Sisi wana Iramba kama kweli tunataka maendeleo kwa ajili yetu na vizazi vijavyo basi tuna kila sababu ya kushirikana kwa umoja wetu kuleta maendeleo yetu. Ni wazi tunaweza tukawa na different political Ideologies lakini tusiziruhusu zikatugawa bali tuzitumie kama chachu ya kuongeza kasi ya maendeleo jimboni kwetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI IRAMBA MAGHARIBI

Mkereketwa wa Maendelo ya Iramba

Hiyo niliyoiwekea nyekundu, imenikumbusha Mnazi Mmoja 60s na early 70s ilipofika siku ya Eid tulikuwa tukienda kuwaona kina Faruku na Fadhili wakicheza "nachi".

Jamani, maandiko muhimu muwe mna-ya-edit, msije kutukana wananchi wenu!
 
Sasa Mkuu wewe huelewi kitu gani? Si nimeweka bayana kwamba nimewasiliana naye? Uzuri na mimi pia nilikuwepo kwenye mikutano hapa jimboni! Hivyo nilioona kila mara hio thread ya Patriq inapandishwa hapa jamvini kila mara nikaona kama Irambian ni wajibu wangu kuijibu. The way nilivyo-frem Title ni kuonesha kwamba kauli ya kupinga tuhuma imetolewa na Mwigulu!

We hata sio mwigulu,Sema ni makada uchwara tu.Capacity yako ndogo sana.Pole
 
Back
Top Bottom