Mwigulu Nchemba atuzwa mapesa bungeni kwa kuitukana CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba (CCM), juzi alituzwa Sh210,000 na wabunge na mawaziri wa CCM baada ya kumwaga matusi na kuiponda bajeti ya upinzani na kuiita ni ya kipuuzi na haitekelezeki, wapinzani wamejaa uigizaji na kumrushia kombora Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuukuu, na baada ya ya kupewa jipya alikubali kimya kimya.

Nchemba akizungumza na waandishi nje ya bunge, alisema jumla ya fedha alizopewa na wabunge na mawaziri kadhaa zilifikia Sh210,000.Aliwashukuru wabunge wote wa CCM kwa kuona mchango mzuri aliotoa bungeni kwa maendeleo ya Taifa

Source:Mwananchi
 
Pia alisema ana Degree ya uchumi first class, hivyo anaujua sana uchumi. Pengine ndiyo maana hata kule Igunga alijitahidi asifumaniwe
 
First class honours degree, inamruhusu ku pursue academic career, siasa ya nini bana?
 
Ukitupa jiwe gizani na kisha ukasikia kelele basi ujue limempata mtu.

Kufa kufaana ya mwiguru yanachoma kotekote.... ameamsha hasira ya wapinzani.
 
Kutoka Tanzania Daima

TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.

Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.

Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).

Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.

Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.

"Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa chama chetu Igunga," alisema ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na gazeti hili.

Hata hivyo, ofisa huyo alisema uchunguzi walioufanya awali kuhusu tukio hilo umebaini taarifa za kigogo huyo wa CCM kuwa na uhusiano usiofaa na mke wa mtu zilivujishwa na kundi la vijana wengine wa kiume walio katika timu hiyohiyo ya kampeni ya CCM ambao ndiyo waliopenyeza taarifa hizo kwa mume wa mwanamke anayetuhumiwa.

Wakati chama hicho kikihaha kulifunika sakata hilo ili lisivuje, viongozi wake waandamizi walipata wakati mgumu kumnadi mgombea wao, Dk. Peter Kafumu, kwenye ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Kata ya Nyandekwa, katika jimbo la Igunga.
 
Kama siasa ya tanazania ni ya aina hii basi mungu aniepushe na kikombe hiki.
 
Wasanii wanapokuwa kwenye maigizo na wanapofaulu kuigiza huwa wanatuzana.....hawakuwa na jipya bali kututhibitishia usanii wao....
 
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba (CCM), juzi alituzwa Sh210,000 na wabunge na mawaziri wa CCM baada ya kumwaga matusi na kuiponda bajeti ya upinzani na kuiita ni ya kipuuzi na haitekelezeki, wapinzani wamejaa uigizaji na kumrushia kombora Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuukuu, na baada ya ya kupewa jipya alikubali kimya kimya.

Nchemba akizungumza na waandishi nje ya bunge, alisema jumla ya fedha alizopewa na wabunge na mawaziri kadhaa zilifikia Sh210,000.Aliwashukuru wabunge wote wa CCM kwa kuona mchango mzuri aliotoa bungeni kwa maendeleo ya Taifa

Source:Mwananchi
Achekelee tu lakini yanamwisho hayo
 
Sasa si umeona "wabunge wa CCM" ni mwendelezo wa akili ndogo kutawala akili kubwa, ujinga kutawala akili na busara!!!
 
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba (CCM), juzi alituzwa Sh210,000 na wabunge na mawaziri wa CCM baada ya kumwaga matusi na kuiponda bajeti ya upinzani na kuiita ni ya kipuuzi na haitekelezeki, wapinzani wamejaa uigizaji na kumrushia kombora Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuukuu, na baada ya ya kupewa jipya alikubali kimya kimya.

Nchemba akizungumza na waandishi nje ya bunge, alisema jumla ya fedha alizopewa na wabunge na mawaziri kadhaa zilifikia Sh210,000.Aliwashukuru wabunge wote wa CCM kwa kuona mchango mzuri aliotoa bungeni kwa maendeleo ya Taifa

Source:Mwananchi

Sijawahi kuona hiyo ya utuzwaji bungeni. huu ni ukilaza wa hali ya juu. Mtu anaongea kinyesi watu wanampa pesa eti wanamtuza. Sijui hiyo point ya kumtuza imeongeza nini katika taifa hili. Nyie wabunge mliotoa tuzo pelekeni mambo hayo kwa ISHA MASHAUZI - Wanamipasho wakubwa nyie!!!!
 
Kama yale maneno machafu yasiyofaa mbele ya watu na mbele ya wasomi ndiyo yaliyomfanya atuzwe basi kuna tatizo kwa viongozi wetu. Because wanapalilia uchafu, how can a man who insult others infront of children and others and he is awarded?? What is the meaning of Award, means to encourage him to speak such words?? Can Pastors in the House help him please!!! He needs counselling.
 
ukweli ni kwamba wanachezea mali za taifa letu,tunaomba kuwambia siku zinahesaboka 2015 sio mbali wahamia ughaibuni na familia zao.ukeli hawa magamba wana kera sana watu walala njaa,watoto wa masikini hawaendi shule,madawa hospitalini hakuna, vyakula bei juu, mama zetu wajawazito wana kufa kwa kukosa madawa, kisha wao wana sifiana na kupeana pesa za sisi walalahoi, nasema walahi waombe NCHI TUSICHUKUE.
 
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba (CCM), juzi alituzwa Sh210,000 na wabunge na mawaziri wa CCM baada ya kumwaga matusi na kuiponda bajeti ya upinzani na kuiita ni ya kipuuzi na haitekelezeki, wapinzani wamejaa uigizaji na kumrushia kombora Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuukuu, na baada ya ya kupewa jipya alikubali kimya kimya.

Nchemba akizungumza na waandishi nje ya bunge, alisema jumla ya fedha alizopewa na wabunge na mawaziri kadhaa zilifikia Sh210,000.Aliwashukuru wabunge wote wa CCM kwa kuona mchango mzuri aliotoa bungeni kwa maendeleo ya Taifa

Source:Mwananchi
Kijogolo sina nyumba eeh!! kajenga barabarani!! Kajenga nyumba ya mawe eeh!! ghorofa ndani kwa ndani!! Hiyo ndiyo CCM mwana wanahonga mabinti na wanaume!! Laana kum!! Au huyo kijogoo ni balaa kote kote!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom