Mwigulu Nchemba ana kesi ya kujibu kabisa

Mimi nashangaa watanzania. Hivi kweli Mwigulu Nchemba ndiye mtu wa kupotezea watu mida? Kweli kweli hili suala tulipe uzito wowote kweli!!! Badala ya kufikiria watoto wetu wenye uwezo darasani lakini hawezi kulipa ada watafika vipi huko mbele kukidhi ndoto zao katika maisha....

Mwigulu sio mtu wa kutupotezea muda kumjadili hata siku moja
 
Mkuu naomba kujua kitu kimoja je ukienda kupata print out kwenye mobile operator unaweza kupata na hii SMS na ikaonyesha imetoka wapi kwenye mitandao ya hawa operators naomba unipe jibu mkuu tafadhali sana sana

mkuu hata mimi ndo swali nililonalo, kuwa imei namba itakayoonekana ni ya namba ipi? na kwa kuwa kwa program hiyo, haihitaji uwe na simu nyingine, yaani kwa kutumia computer tu, unaweza kutuma sms na ikasomeka imetoka kwenye simu moja kwa moja.

hivyo sina majibu kwa swali lako, ila jana nimekuwa nikimtafuta jamaa yangu aliyeko voda, nilipomdokezea alisema hakuwa kusikia kitu hiyo, labda akipata lolote anaweza kutufahamisha
 
imei ya simu yako au ile uliyotumia.

nimekumbuaka kitu kimoja cha msingi kuwa, kwa program hiyo, hakuna simu inayohusishwa ispokuwa wakati wa kupokea ujumbe tu. sasa ipi itasomeka imetuma ujumbe? computer uliyotumia inaweza kujulikana?
 
Hivi ile leso ina maana gani, maana ni yeye pekee anayevaa leso ya bendera ya Taifa !!!
Ndivyo wafanyavyo mafisadi waliokubuhu kuwapoteza uelewa kuhusu yeye. Anatafuta umaarufu tu kujifananisha na watu maarufu ambao wengi ni wasafi, kama Kaunda na leso yake nyeupe mkononi, JKN na kifimbo chake mkononi, Museveni na kofia lake ya tarabushi
 
By Msalagambwe:
Vijana technolojia ni yenu,
muitawale muitumie,
kuleta mabadiriko.

Hawa Nunda bado wameikumbatia jana,
waonyesheni kwamba,
umri wenu ni mdogo,
lakini kazi yenu ina umri na chumvi nyingi.

Muda wa kujificha nyuma ya mabo ya kutunga,
umekwisha,
Ni wakati wa kukabiliana na ukweli uso kwa uso,
Ya mafichoni kuwekwa hadharani,
Ya kizani kutiwa nuru.

Wakati ni huu.


Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom