Mwigulu na tuhuma dhidi ya CHADEMA

Uongo ni asili yake,jina analotumia si lake,mtu anaeiba hata jina ni kuogopwa,leta huo mkanda kaka tuuone. Watanzania wa leo si kama wa jana. Kwa kumtazama tu Mwigulu anaonekana ana mtindio wa ubongo,tumsamehe bure anahitaji maombi.

Jamaa ni bonge la zuzu,nasadiki kweli sasa jina sio lake. "Tajiri atalindwa na jirani yake mwenye shibe" by Mwalimu Nyerere.
 
kitu ambacho ccm wamekosea ni kuweka vijana kama Mwigulu Lameck kwenye nafasi za juu za chama,hawajuwi kujenga hoja kabisa,hawa ndio wanaoharibu chama

Kitu ambacho CCM tumepatia ni kumweka Mwigulu kuwa Naibu katibu mkuu.........nyie mnachama chenu na sie tunachama chetu....pilipili usiozila zakuwashia nini?
 
Naona hayo ndo waliyotuma wananchi wake aje kufanya lakini akumbuke 2015 wananchi wake watamuweka kizimbani kumuuliza ndo tulikutuma ukasemee ya chdm na kuuza sura wakati ahadi hazitekelezwi
 
Naangalia EATV, namuona Mh. Mwigulu Nchemba akiijadili CHADEMA na moja ya vitu anavyozungumza ni CHADEMA kuwa na makundi mawili huku kundi moja lenye nguvu linaongozwa na wanakaskazini ambao wanawatumia wanachama wao kama karai wakimaliza kazi Yao (CHASATA).

Lakini mheshimiwa alienda mbali zaidi akisema anamshangaa msajili wa vyama vya siasa kwa kukiacha chama hicho kiendelee na kazi huku akijua ni chama kinachopanga mauaji ya watanzania na yeye akiwa na ushahidi wa mkanda video.

Wadau ikoje

Ameishiwa sera huyo jamaa.
 
[h=2]Mwigulu HADHI YAKO NI YA a, e, i, o, u ukiweza hii nitakupa hii a,b,c,d,e .....tangu utoe RUSHWA KWA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KULE MERU HUJATULIA NA HUTATULIA MPAKA MWISHO.JITAFAKARI SANA KIJANA.[/h]
 
teh MWIGULU anaiogopa sana CDM ila naona anakitetea kitumbua chake tu mbele ya wakulu...si unajua tena hivi vyeo vya kupeana...
 
Kama kweli mwigulu anao mkanda wa video unaoonyesha Chadema wakipanga mauaji kwanini asiupeleke katika vyombo vya dola ili viweze kuchukua hatua za kisheria?

Ni wazi kwamba hiki anachokihubiri ni propaganda nyepesi sana kwakuwa wananchi wanafahamu kuwa wao ndio wenye serikali na kama wanamfahamu mhalifu wangeshamshughulikia.

Haya ni maajabu ya ccm kufanya siasa kama vile na wao ni wapinzani, so sad indeed!!
 
Viongozi wa namna hii ni wavivu wa kufikiri na wamekengeuka. Wakati ukifika watajifunza kuwa kuna mambo yasiyohitaji porojo
 
Nimepata mshituko baada ya kusoma jina hilo na sitaki hata kulitamka maana linanuka kama mdomo wake.
 
Nchemba ni kati ya watu waliopewa nafasi ndani ya chama cha mabubaliano ya kutaka kukichafua CHADEMA kwa mbinu ambayo inaonekana kuwa dhaifu maana waliomtuma pia dhaifu. Hivyo anahaha kujinasua asije akatemwa kabla ya wakati. Atazunguka channels zote nchini kutangazia umma kuwa CHADEMA wanapanga mauaji bila mafanikio, mwisho wake waliomtuma watamtema kama walivyomtema mkongwe WM-Wilson Mkama!! Jeshi la polisi lenye watu wa profession za upelelezi wameshindwa kubaini kuwa CHADEMA wanapanga mauaji, leo yeye hata sifa za kuwa polisi jamii hana, anakuja na polojo za kitumwa, try other options, hiyo ime-fail!!

Nawaonea huruma hao wanaokubali kutumiwa ktk mkakati huu mbovu wa kuichafua CHADEMA. Nawashauri wachunge maisha yao kwani magamba hawakawii kuwakolimba ili kuthibitisha madai yao.
 
Mwigulu sasa anaonyesha uwezo mdogo alionao katika kujadili hoja za msingi. Hoja yake kubwa akilala, akiamka ni CDM. Yeye kama mbunge wachama tawala akazane kutekeleza ahadi zao kwa wananchi, mambo ya kujadili chadema...oh itakufa baada ya 2015, na si vyama vingine inaonyesha dhahiri kwamba CDM inamtisha mno. MWIGULU KUMBUKA ARUMERU ULIKUJA NA MAUWONGO YAKO PAMOJA NA KAMATI YA KUPOROMOSHA MATUSI LAKINI MWISHOWE MKAPIGWA CHINI.
 
Mwigulu anaiogopa sana Chadema, kwake yeye vyama vingine vya upinzani vilishakufa kimebaki chadema! Na anahisi chadema wanakaribia kuchukua nchi, anashindwa kulala.
na hivi akiangalia mikoa waliyokua wakiitegemea kama Mtwara imeanza kuwaponyoka baada ya round moja tu ya M4C mnadhani atapataje usingizi? Mwigulu ni kama mwanaume aliyenyang"anywa mke anayempenda na jirani yake, ataanza kuongea hata peke yake njiani anatamka jina lake, yeye pia si ajabu ucku anahisi magwanda yanamjia ndotoni!! Pengine mke wake anaweza kuwa na siri nyingi za huyu jamaa na hiyo Chadema inayompa kichaa
 
Naangalia EATV, namuona Mh. Mwigulu Nchemba akiijadili CHADEMA na moja ya vitu anavyozungumza ni CHADEMA kuwa na makundi mawili huku kundi moja lenye nguvu linaongozwa na wanakaskazini ambao wanawatumia wanachama wao kama karai wakimaliza kazi Yao (CHASATA).

Lakini mheshimiwa alienda mbali zaidi akisema anamshangaa msajili wa vyama vya siasa kwa kukiacha chama hicho kiendelee na kazi huku akijua ni chama kinachopanga mauaji ya watanzania na yeye akiwa na ushahidi wa mkanda video.

Wadau ikoje

mim nkisha muona mwigulu alimaarufu mzee wa kujipatia wake za wtu,alimaarufu janga la kitaifa,napata sana kichefuchefu!!!!!!!lakini naishanga police inayoongozwa na shemeji wa kikwetebwana Mwema asiy kuwa mwema,najiuliza,wanaongoza jeshi hilo kwa misingi ya haki na sheria au wanayo ya kwao mfukoni?!!haingii akilin kwa mtu kama mwingulu atangaze kuwa mtu au kikundi fulan cha watu wanapanga mauaji ya raia wema,na andhibitisha mwenyewe kuwa ana video ya mipango hiyo hatari asiitwe kuhojiwa!!!!!!!!!hii ni dhambi kubwa kwa mwema na serikali anayoiwakilisha
 
EATV nayo imeshakuwa kituo cha kitoto.inakubalije mtu ambaye hana hoja yoyote ya kutatua kero za wananchi kazi chadema tuu kupoteza muda bure.mengi nae anazeeka vibaya.mbona hawamualiki deo filikunjombe ambaye anazungumzia kero sio maujinga ya huyo mpumbavu anayeza ngono muda wote kama aliye mteuwa.

Kauli zako tu..punguza kuropoka boss wangu!! am very sure hujui ulisemalo
 
Naangalia EATV, namuona Mh. Mwigulu Nchemba akiijadili CHADEMA na moja ya vitu anavyozungumza ni CHADEMA kuwa na makundi mawili huku kundi moja lenye nguvu linaongozwa na wanakaskazini ambao wanawatumia wanachama wao kama karai wakimaliza kazi Yao (CHASATA).

Lakini mheshimiwa alienda mbali zaidi akisema anamshangaa msajili wa vyama vya siasa kwa kukiacha chama hicho kiendelee na kazi huku akijua ni chama kinachopanga mauaji ya watanzania na yeye akiwa na ushahidi wa mkanda video.

Wadau ikoje

kama Police wa Serikali yake wameshindwa kuupokea ushahidi wake unatarajia Tendwa amwamini,
yule ni kibaraka hana ushahidi wowote bali anakurupuka
 
Naangalia EATV, namuona Mh. Mwigulu Nchemba akiijadili CHADEMA na moja ya vitu anavyozungumza ni CHADEMA kuwa na makundi mawili huku kundi moja lenye nguvu linaongozwa na wanakaskazini ambao wanawatumia wanachama wao kama karai wakimaliza kazi Yao (CHASATA).

Lakini mheshimiwa alienda mbali zaidi akisema anamshangaa msajili wa vyama vya siasa kwa kukiacha chama hicho kiendelee na kazi huku akijua ni chama kinachopanga mauaji ya watanzania na yeye akiwa na ushahidi wa mkanda video.

Wadau ikoje

Mimi namshangaa sana huyu Bwana Mwigulu Nchembe pamoja na watu wa media zinazokubali kurusha mahojiano haya ya kipuuzi yasiyokuwa na tija kwa Watanzania! Huyu mtu ni mchochezi ilitakiwa akamatwe mara moja na afunguliwe mashtaka mara moja. Kama ana mkanda wa video wenye ushahidi wa kupanga mauaji ya Watanzania kwanini hajafungua kesi Mahakamani? Anangoja nini kichaa huyu???

Mimi naomba wanasheria wa Chadema wako wachukue hatua za kisheria haraka kumshughulikia huyu Bwana Mwigulu. Wapo kina Tundu Lissu,Mabere Marando,Mnyika na Halima Mdee walifanyie kazi swala hili. Kenya mwaka 2007 walichinjana kwa unafiki na uroho wa madaraka wa Wakenya wachache wachochezi kama anavyofanya Nchemba.

Pia Msajili wa Vyama Bwana John Tendwa tunataka atoe tamko kuhusu hizi kauli za Mwigulu. Tulisha wahi kumsikia akitishia kukifuta CDM kwa maandamano ya M4C. Mbona kwa hili la Mchembe wa CCM amekaa kimya kama vile hasikii wala haoni??? Kuna nini katikakti hapo???
 
Viongozi wa namna hii ni wavivu wa kufikiri na wamekengeuka. Wakati ukifika watajifunza kuwa kuna mambo yasiyohitaji porojo
maajabu ya tanzania ni kuwa kila likija swala jipya utasikia "wananchi hawajaelimishwa" (Refer kwenye katiba, ving'amuzi, migodi, barabara, miradi ya maji nk) wakati tunaambiwa zaidi ya 90% yetu tumemeliza elimu ya msingi! Sasa tulijifunza/kuelimishwa nini huko????
Cha kusikitisha zaidi ni huyu mtu mwenye Bcom/MBA zenye gpa za juu kabisa na mchumi daraja la kwanza naye hawezi kuchambua hata hoja na hata kujua ni nini aongee na wakati gani!!!!Je, nae hajaelimishwa??????
Hali hii ndiyo inaongeza mashaka juu ya watz mpaka baadhi wanafikia kuamini kuwa profesa wa Tanzania ni sawa na Form IV wa nchi zingine ...sababu ya watu kama hawa

Back
Top Bottom