Mwigulu Kumbe Inauma Eehhh!! Ulipoitupa kwa Kejeli Bajeti ya Upinzani Uliona ni Sawa!

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Wadau,

Leo kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha ITV nimemwona Bw. mwigulu mchemba akimlalamia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mhe. Mbowe kwamba eti alimwandikia kimemo cha vitisho. Bila aibu anasema eti hali hiyo ilijitokeza baada ya yeye kuipitia bajeti ya upinzani na kuitupilia mbali baada ya kuona hakuna cha maana.

Kinachonishangaza ni namna kibuli kilivyomjaa Bw. mchemba kiasi cha kutotambua kwamba kitendo cha kuitupa bajeti iliyoandaliwa na Kambi Rasmi ya Upinzani usiku na mchana kilikuwa ni ishara ya dharau kubwa isiyoweza kuvumilika kamwe.

Kimsingi, mpaka leo bado najiuliza ilikuwaje spika hakumchukulia hatua za kinidhamu Bw. mchemba kwa kitendo hicho cha dharau na dhihaka kubwa kwa upinzani makini kama wa CHADEMA!!!
 
Ofcoz Nchemba alichemka kutupa ile Bajeti....ile ni dharau iliyopitiliza na kiburi anachojazwa na maBwana wakubwa zake.
 
Kwa nini hakulalamika bungeni mara alivyopata hicho kimemo? Why now? Muda wote huo alikuwa alikuwa anasubiri nini kama kweli aliona hicho kimemo kinakwaza? Mbona hakusita kwenye ile sms (well, spoofed sms?). Huyu mchumi daraja la kwanza ana hoja gani hasa, ya sms za kumtishia au kimemo alichopata mwezi uliopita?

Pili, kuandikiana vimemo baina ya wabunge ni kinyume na kanuni za bunge? Kosa liko wapi?
 
Mapinduzi halisi yatakapowadia hawa ndio kuku wa kuchinja kwa ajili ya sherehe!
 
Mwigulu huyu si ndo alifimaniwa guest na mke wa mtu au nafananisha
 
Back
Top Bottom