Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,176
103,656
Kuna tuhuma zimekuwa zikisienea kwa kasi sana kabla na baada ya kukua kwa matumizi ya mitandao ya kijamii.

Tuhuma hizi zimekuwa zikiwahusu mawaziri na vigogo wengine wakubwa serikalini kuhusishwa na wizi wa majina.Viongozi hao wanatajwa kutumia majina yasiyo yao jambo linalotajwa kuwa upo uwezekana katika ngazi fulani ya elimu walichukua majina ya waliokuwa wanafunzi na kuyatumia kujiendeleza.

Udanganyifu ni udanganyifu tu.Hili halina tofauti na kufoji au kutumia cheti cha mtu mwingine. Umeghushi majina kujinufaisha kielimu!

Kwa uchache Mh.Mwigulu Nchemba, Hamis Kigwangala na RC Makonda wametajwa sana katika hili. Watata wameenda mbali sana kuhusu Waziri Nchemba, kwamba yeye anaitwa Lameki Madelu Mkumbo na jina analotumia ni la Kisukuma na sio Kinyiramba na kwamba hakuna ndugu zake wanatumia ubini wa Nchemba!

Katika uhakiki wa vyeti unaoendelea wako watu watakaokutwa na masaibu kama haya, hii imedhihirishwa na aina ya maswali na upekuzi wanaofanya wataalam hao.

Ni wakati muafaka sasa kwa viongozi hawa kujitokeza hadharani na kujibu kwa ushahidi na mamlaka husika zitoe tamko baada ya kuhakiki ukweli. Jambo hili likipuuzwa litakuza mpasuko ambao ni dhahiri umeanza kujitokeza.

Zipo tetesi mbaya zisizo na ukweli kwamba usakaji wa vyeti feki na udanganyifu mwingine unawahusu sana watumishi wanaoshabikia UKAWA. Sasa kitendo cha kuwapekea na kuwaanika kina Kigwangala kitaondoa upotoshaji huo.

========

Majibu ya Mwigulu Nchemba..
Salama comrades?

Nimeiona thread hiyo hapo juu, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,


Majbu haya ya Waziri yanaendelea kwenye mada hii >>
Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina
 
Mwigulu Nchemba,ndiyo ni Jina la Kisukuma!Na Ni Kweli Lameck Alilichukua Kutoka Kwa Mwanafunzi wa Kisukuma Aitwae Mwigulu Nchemba!

Kwahiyo Baada ya Kufeli Mtihani wa La Saba,Lameck Akaenda Kulichukua Jina la Mwigulu Nchemba na Kulisomea La Saba na Kufaulia Kuendelea O-level,A-level,First Degree and the Second Degree of Economics Pale UDSM!

Hii Trend Ilikuwa ya Kawaida Enzi Hizo, na Mifano Iko Mingi, kuna Hata Waislamu Walichukua Majina ya Kikristo Waweze Soma kwenye Shule za Misheni:

a)Shabaan Robert
c)Bernard Membe

Sipingi Kuwa Wengine Wamewazurumu Wengine kwa Kuwaibia Vyeti au Hata Kuunga unga Majina ya Watu Tofauti! La Saba Anaitwa "A", Kidato cha Nne "B" Na Kidato cha Sita na Chuo "C"! Hawa Tuwalaani Vikali!

Iila Wale Waliosotea Elimu kwa Shida Miaka Ile ya 50,60,70,80 na Tisini kwa Majina Mengine na Bado Wakatusua Tena Huku Kukiwa na Shule Chache za Sekondari na Walimu Wachache, Ebu Tuwape "Thumbs Up"! Huyo Ndiyo Lameck Mkumbo!

Yeye Alilichukua Jina la Mwanafunzi wa Kisukuma Aliyeacha Shule na Kwenda Kuchunga Ng'ombe! Kwa Jitihada Zake Ametusua! Kafanya Kazi B.O.T, Kawa Naibu Katibu wa CCM,Kawa Naibu Waziri wa Fedha,Waziri wa Kilimo,na Sasa Waziri wa Mambo ya Ndani!

Jina Huwa Halisomi, Mtu Ndiye Husoma!
 
Hili swala litaitafuna serikali yetu lisiposhugulikiwa..

Kama hizi tuhuma ni za kweli basi hali ni mbaya kuliko tunavyoweza kudhani maana ikiwa kama ni kweli viongozi wenye kuheshimiwa sana kama hawa hawana sifa za kuwepo waliko je, hao wanaowaongoza si ndo hali mbaya zaidi? Watashindwa kweli kuiba hali wakijua wakubwa wao hawajafata maadli ya kazi?

Kwa namna hii, ikiwa hizi tuhuma ni kweli basi his excellency JPM ana shughuli nzito sana.. itakuwa ni sawa na daktari anayetibu dalili badala ya ugonjwa unaoashiriwa na dalili
 
Back
Top Bottom