Mwigulu chupuchupu kukamatwa na Takukuru

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Ni Kwenye kikao chake na viongozi wa serikali zilizo kuwa zinafanyika kwenye ofisi ya Kata ya maji ya chai...Awali habari ziliwafikia viongozi wa CHADEMA kuwa Mwigulu na wafanyakazi hao wa serikali wako kwenye kikao cha siri wakipanga mikakati ya ushindi kwenye ofisi ya kata ya Maji ya chai ndipo viongozi wa CDM na TAKUKURU wakajipanga kwenda kutibua mchezo huo mchafu wa ccm lakini mita chache kabla ya kufika kwenye ofisi hiyo viongozi hao wa serikali pamoja na mwigulu walitimua mbio huku CDM na TAKUKURU wakiambulia viatu..

=============
Msimamizi wa Uchaguzi ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru amekiri ofisi hiyo kutumika na kikao cha CCM ambayao ni ofisi ya Serikali ya kata ya Maji ya chai na ameamua kuchukuwa Hatua kali kwa Mtumishi huyo ambae tyr amekiri kosa na kikao ni kweli kilitimka
Update
Mambo yamezidi kuwa magumu kwa CCM baada ya wazee na wachungazi wa makanisa mbalimbali kukata katakata kumpigia kampeni kama walivyo kuwa wameomba na Mwigulu ni kutokana tetesi kuwa Siyo Sumari ni Freemason na wanasema ana dalili zote kama kotoboa masikio, kuwa tatoo na nk...wamesema iliwaweze kumfanyia kampeni ni lazima Mwingulu ampeleze Siyoi Sumari kwa wazee hao wakajilizishe....
Na kufatia tifu tifu la Mwingulu na makada wa CCM pamoja na viongozi wa kata kukoswa koswa na TAKUKURU na baadae viongozi hao kurumbana sana wakishutumiana kuwa kuna wasariti kati yao hali iliyopelekea vikao kutokuendelea, kitendo hicho kimepelekea Mwingulu itwe Dar es Salaam kwenda kutoa maelezo kwa uzembe huo. Wakati huo CCM imempa jukumu la kukusanya pesa bw. Paul Kiligini ambae alikuwa mfanyakazi wa benki kuu akasimamishwa kwa kashifa ya kufoji risiti alizo kuwa amewapeleka watoto wake mapacha kwenda kutibiwa India wakati aliekuwa mgonjwa ni mmoja yeye akafoji na badala ya US$ 35000 ikawa US$ 70,000...hivyo amepewa jukumu la kutafuta pesa kupitia makampuni mbalimbali na kuziwasilisha kwa Mwingulu kwa kumkabidhi na si kupitia mabenki na hilo ni jukumu lake Paul ili arudishwe kazini...

Wana JF salam.

Nimeiona thread hii kama inavyosomeka. Naomba kuweka sawa kuwa mtoa maada hana taarifa sahihi. Mimi sujakimbia wala kukimbizwa wala kuonana na TAKUKURU. PIA SIJAFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA SERIKARI BALI NIMEFANYA KIKAO NA MAKATIBU, WENYEVITI WA CCM MATAWI NA MABALOZI.

KUHUSU VIONGIZI WA CDM SIO KWAMBA WALIKUJA PALE NA TAKUKURU BALI MIMI NILIWAKUTA WAKIWEPO MH VINCENT NYERERE NILUPOFIKA TUKASLIMIANA WAKAONDOKA WAKANIACHA NDIO NIKAANZA KIKAO CHANGU. KILICHOTOKEA WALIAMBIWA KUNA WANA CCM WANAFANYIA KIKAO KWENYE OFC YA SERIKALI NDIO WAKAENDA ILI WAHAKIKI WAPATE KITU CHA KUKATA RUFAA BAADA YA MATOKEO. WALIPOFIKA WAKAELIMISHWA KUWA HIYO NI OFC YA CCM NAMI NDIO NIKAFIKA TUKASALIMIA NA MH NYERERE PEACE KABISA AKAONDOKA.

SASA NAFANYA KIKAO CHA WANANA CCM NIKIMBIE NINI HATA KAMA NILIKUWA NA HELA NIKIMBIE NINI MBONA TAR MOJA NILILIPA KIKAO CHOTE WAJUMBE NA TAKUKURU WALIKWEPO NDANI NA HIYO NI STAHILI YA WAJUMBE. WANA JF POSHO YA KIKAO YA KIKATIBA HUTOLEWA KWA MJIBU WA KATIBA HAIKOMI WAKATI WA UCHAGUZI.

TUSITAFUTE VISINGIZIO TUTAFUTE PANADOL ZA KUPUNGUZA MAUMIVU MAANA NDIO HIVYO YAMEANZA POLEPOLE. TUNA IMANI CCM INASHINDA
 
Mwigulu atawapeleka puta uchaguzi huu......mwishowe ni CDM kuangukia pua kama ilivyo kawaida kwenye chaguzi kama hizi.
 
Mwigulu bisha na hilo waanike picha hahahahah Magamba kwisha,nimeona FACE book ya kamanda Nyerere sasa hivi ni kweli tukio limetokea na ameandika
 
Na siku nyingine chadema waende kabla hawaja wataarifu TAKUKURu wala Polisi wakisha wakeka kati ndipo wawajulishe TAKUKURU maana kuitofautisha Takukuru na CCM napata shida sana.....
Ingekuwa vita ya majimaji.
 
Ni Kwenye kikao chake na viongozi wa serikali zilizo kuwa zinafanyika kwenye ofisi ya Kata ya maji ya chai...Awali habari ziliwafikia viongozi wa CHADEMA kuwa Mwigulu na wafanyakazi hao wa serikali wako kwenye kikao cha siri wakipanga mikakati ya ushindi kwenye ofisi ya kata ya Maji ya chai ndipo viongozi wa CDM na TAKUKURU wakajipanga kwenda kutibua mchezo huo mchafu wa ccm lakini mita chache kabla ya kufika kwenye ofisi hiyo viongozi hao wa serikali pamoja na mwigulu walitimua mbio huku CDM na TAKUKURU wakiambulia viatu..
I hope hicho kiatu kitakuwa cha Nchemba maana ana tabia ya kukimbia na kuacha vitu kwa nyuma.
 
Mwigulu atawapeleka puta uchaguzi huu......mwishowe ni CDM kuangukia pua kama ilivyo kawaida kwenye chaguzi kama hizi.
Tanzania tuna safari ndefu yaani una shabikia kuona democrasia ina bakwa mchana kweupe halafu unaleta ushabiki wa kijanga hapa....tumia akili na siyo makamasi
 
Nafikiri strategy ya cdm na wananchi wapenda haki iwe kukamata ili baadae wataarifu takukuru na polisi. Kikatiba kila raia ni mlinzi wa amani wa nchi yetu.kwakuwa leo imesanuka siri basi badiri utaratibu.pili ni vyema ikajulikana nchemba hizi pesa anazitoa benk hipi.kama ni benk then ni bora apatikane informer toka benk atakayekuwa anaeleza pesa wanayotoa kwa siku,jina la a/c nk. Tendwa aseme kiasi kilichoidhinishwa ili kitumike hicho tu la sivyo pesa za nchemba anyang'anywe ata ikiwezekana mchana kweupe.zoez la kunyang'anywa litashindikana iwapo anatumia cheque tu. Nashauri wana arumeru msilale kwani pesa za kurubuni wananchi ni kodi zetu
 
Ni Kwenye kikao chake na viongozi wa serikali zilizo kuwa zinafanyika kwenye ofisi ya Kata ya maji ya chai...Awali habari ziliwafikia viongozi wa CHADEMA kuwa Mwigulu na wafanyakazi hao wa serikali wako kwenye kikao cha siri wakipanga mikakati ya ushindi kwenye ofisi ya kata ya Maji ya chai ndipo viongozi wa CDM na TAKUKURU wakajipanga kwenda kutibua mchezo huo mchafu wa ccm lakini mita chache kabla ya kufika kwenye ofisi hiyo viongozi hao wa serikali pamoja na mwigulu walitimua mbio huku CDM na TAKUKURU wakiambulia viatu..
Siasa za wakati huu kwa kweli mtu unatakiwa uwe fit sana...maana hapo angekuwepo mtu kama captain Komba asingetoka.
 
Tunao watu wanaojiita wanasiasa leo hii ambao hawana hata fununu kuhusu mambo ya msingi kabisa ya Taifa hili.

Kwao historia ni simulizi za wafu na ambao wanaamini kwamba wanaweza kushika madaraka ya nchi bila ya kutaka kujua nchi yenyewe imeanza vipi,imepita mabadiliko gani, na imekuwaje hadi ikawa hivi ilivyo leo - Jenerali Ulimwengu

Siasa za wakati huu kwa kweli mtu unatakiwa uwe fit sana...maana hapo angekuwepo mtu kama captain Komba asingetoka.
TAKUKURU watakuwa wamewasanua au kuna mtu alikuwa sehemu anawaangalizia sooo....lakini siku wakiingia kwenye 18...hahahah itakuwa wanzo na mwisho wa tabia hiyo maana Takukuru naona wameshindwa kuwa zibiti....
 
Mimi huwa sielewi ufanisi wa rushwa kwenye uchaguzi. Kwani wapiga kura wanashindwa kutambua kuwa chama chochote kinachotumia rushwa kupata ushindi kinapaswa kutoswa? Hii ngoma si ya Takukuru maana Takukuru ni serikali ni CCM, hii ngoma inapaswa kuchezwa na wananchi wapiga kura wa Arumeru. Wao ndio wataenda kupiga kura kumchagua huyu au yule na kama rushwa itawabadilisha akili basi Tanzania tuna safari ndefu sana ya kuelekea democracy ya kweli.
 
Back
Top Bottom