Mwigulu ashutumiwa kwa kuleta mkanganyiko Arumeru - Apendekeza Jina la 1 hadi 4 yakatwe

Kiongozi big up kwa ufafanuzi. Watu wengine wa ajabu sana sijui ni chuki binafsi? JF inasomwa na wengi na kuaminiwa mtu unapoandika kitu cha kizushi huwatendei haki wanaotegemea JF kama chanzo cha kuaminika. Mwigulu is not such a cheap person na infact ndiye pekee so far hajakumbwa na kansa ya makundi. Kama kijana mwenetu bila kujali itikadi nampongeza kwa kuwa independent in thinking, keep it up. Wanaokupakazia wataendelea kuumbuka kama huyu ndugu yetu mwenye chuki binfsi
Punguza mapovu sema nini wanampakazia huyo mwanenu na amejibu nini.
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.
Join Date : 25th February 2012 Posts : 10 Rep Power : 303 tokea baba yenu PINDA atumie data za ufisadi wa blandina nyoni(alizopata humu JF) kumfukuza mmekuwa mkimiminika sana humu jamvini...ID yako ya pili ni nani vile?
 
[Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...]

Kigwangala, wewe kaa unasubiri vikao vya CC wenzako wanachanja mbuga kisiasa. Unavyoshangaa kuhusu mwigulu kutokuwa na mandate yoyote ya kuamuru nani apitishwe, ndivyo na UVCCM arusha wanavyoshangaa inakuwaje mwigulu anataka kuwaamulia mgombea?? Kwani we hukumbuki Bashe alipigwa zengwe kwa namna gani? Staili hiyo hiyo ndio anayopikiwa SIOI SUMARI.
 
mwigulu kwa uwongo!!!!...eti nilifungua kikao kisha nikaondoka...kha
 
Wakuu jf
Kwanza nafurahi sana kuona hawa wabunge vijana wa CCM wanauthubutu wa kujiunga na JF kama hivi na kujaribu kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali

Ombi langu kwenu ni kuwa tujikite kwenye hoja badala ya kejeli, hoja iliyopo mbele yetu ni kuwa Mwigulu analazimisha apewe ukampeni meneja na ametolea ufafanuzi pamoja na mwenzake Hkigwangala, tukome hapo

Sasa naona yameanza mashambulizi binafsi hapa, mara Bashe mara wake za watu, huu si uungwana au mnataka na wao waombe ma mod wawe wanawalinda kama anavyofanya Dr Slaa pindi mtu akianza tu personal attack mod wanafuta fasta na kutoa ban?

Wakati mwingine ndio maana wanakimbia humu sio kwasababu wameshindwa hoja la hasha sababu watu wanakejeli zaidi kuliko kujenga hoja, na hapa haijalishi hoja iwe nzuri au mbaya kwake, kama tunajadili kitu basi tubaki kwenye hicho na si kuanza kejeli matusi dharau nk, mtu hana hata cha kuandika anaropoka tu madudu

Twedeni nao taratibu hoja kwa hoja
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.

ha ha ha.. mkuu nafurahi umekuja kujumuika na sisi huku.. inawezekana mliowa2ma wameshindwa kazi na sasa mmeamua kuingia wenyewe front.. naomba kutofautiana na ww hapo kwenye red.. ninachokiona kuongoza kampeni kwako ni starehe au ilikuwa starehe.. kuleee igunga.. halafu lazima change (money) ibaki bana.. maana umekabidhiwa mikoba yote.. kuhusu hilo la printing unit kariako achana nalo.. wenzio waliambiwa wana utajiri.. wakabisha na kutishia kwenda mahakamani.. mpaka leo cijacikia kesi yeyote ya madai toka kwao.. sasa huu mkwala wako.. ati akaichukue..
 
Tatizo hapa ni mpunga wa kampeni, CCM ni rushwa na rushawa ni CCM, kila mtu wa CCM anafikiri kwa tumbo.Mwingu kaka;Meru napajua mzazi wakikupa hicho kikombe kitupe huko watu ni sime- rungu - sime mtindo moja.............hakuna rangi mtaaacha ona chalii..........huko ndo kwao
 
Mimi sio msemeji wake ila jana ni moja ya maswali alioulizwa na kuyatolea ufafanuzi povu liko wapi hapo. Umeshikilia kama vile ulikwepo
 
Guya @JF, to be sincere I thought and expected Mwigulu to be some kind of an intellectual, but alas what a disappointment to me he has turned to me! This his tenth post with full of flexuous notations. Naona anongea kama Yusufu Makamba.

Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.
 
mwigulu kwa uwongo!!!!...eti nilifungua kikao kisha nikaondoka...kha
Labda yeye ndio Mwenyekiti wa CCM u never know, maana kwa upeo wangu mdogo kazi ya kufungua kikao na kufunga ni kazi ya Mwenyekiti na katibu kazi yake ni kusoma ajenda za kikao na kutunza kumbukumbu za kikao, sasa huyu Mwi gulu wa JF alifunguwa kikao yeye kama nani!!?? Fun,......
 
Kiongozi big up kwa ufafanuzi. Watu wengine wa ajabu sana sijui ni chuki binafsi? JF inasomwa na wengi na kuaminiwa mtu unapoandika kitu cha kizushi huwatendei haki wanaotegemea JF kama chanzo cha kuaminika. Mwigulu is not such a cheap person na infact ndiye pekee so far hajakumbwa na kansa ya makundi. Kama kijana mwenetu bila kujali itikadi nampongeza kwa kuwa independent in thinking, keep it up. Wanaokupakazia wataendelea kuumbuka kama huyu ndugu yetu mwenye chuki binfsi
Bahati mbaya mleta mada ameleta kama tetesi wakati mimi nina uhakika na niliweka bandiko la ripoti ya mwingulu kuhusu kukata jina la kwanza mpaka la nne ili kuondoa mgawanyiko uliopo kati ya makundi ya Lowasa na Membe.....
 
Bahati mbaya mleta mada ameleta kama tetesi wakati mimi nina uhakika na niliweka bandiko la ripoti ya mwingulu kuhusu kukata jina la kwanza mpaka la nne ili kuondoa mgawanyiko uliopo kati ya makundi ya Lowasa na Membe.....
Crashwise, wengi walibeza bandiko lako lakini leo yanayotokea ni ushahidi tosha.
 
Kikao cha CC kinachoendelea kinasemekana kitakuwa kugumu kutokana na taarifa ya mwigulu nchemba aliyoiwasilisha kwa CC kuleta mkanganyiko.
Taarifa hiyo inapendekeza kuwa ili kuondoa makundi yanayoonekana kushamiri sasa majina ya wagombea namba MOJA hadi NNE yakatwe na majina ya namba TANO na SITA yafanyiwe maamuzi ya mmoja wao kupitishwa. Mkanganyiko katika jambo hili unakujwa pale ambapp mgombea namba TANO Antony Musani ameshajitoa CCM na kwenda CHADEMA ambako nako amechukua fomu ya kugombea ubunge. Mgombea namba SITA URIO aliyepata kura 11 yeye alishachoka katika hatua za awali na kuwa alishatangaza kujitoa kwenye mchakato.
Habari zinasema UVCCM arusha wamekasirishwa na taarifa hiyo ambayo wameilalamikia inajadiliwa kwa sababu zipi wakati ujio wake na ziara yake arumeru haukuwa wa kutumwa na CC ili kutoa mapendekezo.
hii kitu nilisha iweka hapa jamvini na wala siyo tetesi

Siku chache baada ya kuchakachuliwa hatimae vijana wawili Elirehema Kaaya na Wiliamu Sarakikya watangaza nia ya kuhamia Chadema kama uchaguzi hautafanyika upya.

Walisema uchaguzi uliofanyika rushwa ilitumiaka kwa kiwango cha juu sana, hivyo hawako tayari kuendelea kukaa kwenye chama cha mafisadi wanaotumia kodi ya wananchi kujinufaisha kwa faida ya familia moja wameahidi kama uchaguzi usipo rudiwa basi wana hamia chadema kwenye chama makini na kuwahakikishia jimbo hilo linaenda chadema, haya yalijitokeza usiku wa kuamukia jana baada ya kuamua kukutana na kamanda Godbless Lema kwenye hotel ya Impala ilikuangalia uwezekanao wa kuhamia Chadema.

Nilifanikiwa kujipenyeza na kuchukua picha ingawa haionekani vema.

attachment.php


Wa kwanza kulia ni Elirehema Kaaya katikati ni Kamanda Godbless Lema na kushoto ni Wiliam Sarakikya.
wakiwa kwenye kikao cha siri hoteli ya Impala Hotel.


=========================
Upadate
Baada ya kubaini mpasuko uliko ndani ya kambi Mbili za Membe na Lowasa. Ripoti ya Mwigulu imependekeza kukata majina ya Kwanza hadi namba 4, kama njia ya kupunguza uhasama ndani ya chama hivyo itafanya kambi ya Lowasa na Membe zote kukosa kama hili litafanyika litakuwa pigo kubwa kwa Sioi alietumia kiasi cha 100mil kuhonga wajumbe hiyo Huku chama kikitumia kiasi cha mil 68 kama posho kwa wajumbe waliokuwa wakipewa kuanzia 50,000.
 
Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...tusubirini vikao vya juu viamue nani atatayetuwakilisha huko, sisi tutaenda kumnadi tu! Obviously, kuna watu wanamuogopa Mwigulu (Jembe la ukweli kutoka Iramba Magharibi) na kwa vyovyote vile akipewa jukumu hilo atawasumbua sana tu maana hana papara na anaweza mikiki mikiki ya siasa za sasa...


Daktari, nitoke nje ya mada kidogo:

Hivi hizo MD, MPH na MBA zako unazifanyiaje kazi katika ubunge maana hata mimi nashangaa kidogo kwa jinsi ambavyo huenda una zi-under utilize huko kwenye ubunge na hata wengine kukutishia nyau ya kukufukuza chamani. Natamani kusikia jinsi unavyo zi-utilize effectively, maana miaka ulo kula ktk hizo isiwe ni bure kwako, na kwa taifa letu au kama huzitumii basi nakuomba usiziandike hapo maana ni ujiko usio na faida kwako, kwa familia yako, jimboni kwako na kwa taifa letu. Is a wastage of resources and time
 
Nashukuru, kwanza kwenye hiyo Mwi gulu ni Mwigulu? Ni mbwembwe tu ila ndio mimi na haileti tofauti pia inavutwa kwa kutamka. Kuhusu ushindi kila mwanadamu hutarajia ya yalio ya heri hivyo natarajia chama changu kishinde.

Mhe Mwigulu Mchembe,

Habari za Arumeru. Nashukru kwa kujitokeza kwenye ukumbi wa GT. Mimi nina maswali tuwili kama 6 hivi na ninaomba unijibu:
  1. Kule Igunga ni kweli ulifumaniwa na mke wa mtu?
  2. Kama ni kweli kwanini uliacha kazi ya kupiga kampeni za chama chako CCM ukaanza ufuska?
  3. Igunga CCM mliongoza kwa kampeni za kibabe ikiwemo kutumia silaha k.m.bastola.Je Arumeru nako mtatumia silaha ili kuwatisha wanachama na wananchi wengine wasijitokeze kupiga kura?
  4. Igunga kulitokea mauaji ya wakala wa CDM. Je,safari hii mna mikakati gani na mawakala wa CDM?
  5. Kwanini CCM mnatumia wizi wa kura,kununua shahada na rushwa ili kushinda kila uchaguzi?
  6. Je,wewe huoni kuwa CCM kwa sasa mmepoteza mvuto kwa Watanzania na hivyo mnatakiwa muwapishe wapinzani makini
Wasalaam.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom