Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
Hii inathibitisha kuwa MBOWE ni Hatari kwa CCM na ambaye anweza kutazamwa kwa jicho tofauti sana maana tazama uzushi huu tena, Hiyo siyo CV wala nini?? Acheni uzushi jamani
hii makala mbona kama imeandikwa na Mbowe
Mwandishi kaandika mambo mengi ya kupika sio kweli mfano anasema kuwa MBOWE ndio alimtafuta na kumkomaza Zitto.WAKATI kwenye mahojiano mengi tu Zitto anasema yuko Chadema toka mwaka 1992.na Mbowe kapata uenyekiti 2004.
yapo mengi ambayo anaonesha kuwa kaandikiwa na Mbowe au ni kujipendekeza kwake.
swali la Msingi hajasema kuwa Mwenyekiti huyu kasoma shule gani ana elimu gani?wasifu gani wa mwenyekiti wa Chama ambao hauelezi elimu ya Mwenyekiti?
kila jambo Mbowe ndiye aliyebuni jee sio KAMATI KUU ya Chadema ndio inayoamua kuwa kuwe na Helkopta au operesheni Sangara n.k?basi hakuna haja ya kuwa na Chama kama kila kitu ni Mbowe.
kama maendeleo ya Chadema huwezi kuandika na ukawaacha watu kama KABURU AMANI.pamoja na yote Kaburu anamchango mkubwa Chadema.mtu kama Zitto posible alipata ushawishi mkubwa toka kwa Kaburu.
.
Mkuu Kanda2 vp tena mbona Mengi anatumia vyombo vyake kujisifia!
Mbona Rostam nae anatumia vyombo vyake kujisifia nini cha ajabu hapo?
Kwani kuna nini kama gazeti likimsifia MBOWE, Sasa sio Ukweli, Acha mambo ya ajabu kama haya na uzushi kama huu hapa
Chadema chama cha wachaga rafiki zangu huko tanzania wmealalamika na wanataka kuhama chadema wanasema kinaendeshwa kimisingi ya ukabila ukiwa sio mchaga hupati kitu pale zitto angekuwa mchaga au mpare angepewa nafasi ya kuongoza
wacheni uchaga

Hivi huu uanademokrasia wa kibongo ukoje? Yaani hata uvumilivu wa kukosoana kistaarabu hatuujui. Sasa kama mtu ametokea kumsifia Mbowe iweje wengine wasiwe na haki ya kukosoa usifiaji ama wasifu huo?
Kama una maoni tufauti na ukosoaji huo si na wewe ukosoe ukosaji huo...
omarilyas
Kama elimu haina maana kwanini mwandishi anasema kuwa vijana wasomi wanajiunga na Chadema?Mwandishi kaandika mambo mengi ya kupika sio kweli mfano anasema kuwa MBOWE ndio alimtafuta na kumkomaza Zitto.WAKATI kwenye mahojiano mengi tu Zitto anasema yuko Chadema toka mwaka 1992.na Mbowe kapata uenyekiti 2004.
mkuu hivi Zitto wakati Chadema inaanzishwa alikuwa na miaka mingapi? Nimesoma sehemu Zitto ana miaka 33 so it means 1992 alikuwa hajafikisha miaka 18 Je inaruhusiwa kuwa member below 18?
Pia Mbowe amekuwa mwenyekiti 2004 lakini haimaanishi kuwa alijiunga na chama 2004.
yapo mengi ambayo anaonesha kuwa kaandikiwa na Mbowe au ni kujipendekeza kwake.
Mimi nadhani ungeyaweka wazi hayo mambo kuliko kuyaacha kwenye mabano.
swali la Msingi hajasema kuwa Mwenyekiti huyu kasoma shule gani ana elimu gani?wasifu gani wa mwenyekiti wa Chama ambao hauelezi elimu ya Mwenyekiti?
Elimu ya mtu haimfanyi ndiyo awe na uwezo wa kufikiri sana kwani tuna maprof wangapi serikalini na hakuna wanalofanya. Elimu si kigezo cha kiongozi bora japo elimu ni muhimu ili uwe kiongozi. Si kila mwenye elimu ni kiongozi bora.
kila jambo Mbowe ndiye aliyebuni jee sio KAMATI KUU ya Chadema ndio inayoamua kuwa kuwe na Helkopta au operesheni Sangara n.k?basi hakuna haja ya kuwa na Chama kama kila kitu ni Mbowe.
Kubuni ni tofauti na kuamua. Alibuni vitu lakini kuamua ni chama kizima. Nafikiri hii inabidi wanachadema wenyewe wajibu kama ni kweli au la.
kama maendeleo ya Chadema huwezi kuandika na ukawaacha watu kama KABURU AMANI.pamoja na yote Kaburu anamchango mkubwa Chadema.mtu kama Zitto posible alipata ushawishi mkubwa toka kwa Kaburu.
Huyo Kaburu hakuna aliyekataa kuwa alikuwa na mchango au la. Kwani hata katika maelezo jamaa kasema kuwa wabunge walikuwa wanafanya mikutano kwa hela zao za mfukoni including huyo Kaburu. Hivyo kuna mchango hajapinga. Hila hilo la zitto kuwa aliletwa na kaburu siafiki labda kama aliletwa na mama yake
Ina maana huyu Mwandishi pamoja na kuweka maelezo yote haya ameshindwa basi kuweka huo wasifu kwa kuonesha Mbowe amekata madarasa kwa kiasi gani?