mwenzenu nimefiwa

Poleni kwa msiba mkuu, Mungu awape faraja katika kipindi hiki cha majonzi
 
Assalamu Alaikum
Admins, Moderators na members wote
wa Jamiiforums
Kwa masikitiko makubwa nawataarifu
msiba wa baba yangu aliyefarik leo mchana msiba upo tanga makorola mi nipo iringa najichanga changa muda huu nianza safari nipate kuwahi mazishi hapo kesho kama mwenyezi mungu akisaidia mazishi ni saa 4 asubuh katika makaburi ya msambweni.

Pole sana baba
 
Pole sana Ndg yangu!

MUNGU ampe pumziko la milele ktk makazi yake!
Bwana ametoa na Bwana ametwaa!
 
Pole sana nio kazi ya muumba hiyo
nakutakia safari njema kwenye maziko ya mzee wako
 
pole sana kwa msiba na Mungu awatie nguvu na awafariji
 
Pole sana Mkuu kwako na kwa familia. Mungu akupeni nguvu ya kustahimili majonzi ktk kipindi hiki kigumu.
 
pole sana kwako na familia. Mungu awajaalie moyo wa subira
 
asanteni sana ndugu zangu!
kwa wanaopajua vizuri iringa muda huu nipo ipogoro hapa napima pima upepo nianze safari mniombee nifike salama!
 
Pole sana kwa kumpoteza baba. Mungu akutie nguvu na akutangulie katika safari yako. RIP baba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom