Mwenzenu Narogwa au?

Huna haja ya kuendelea kukaa hapo kwani si sehemu salama kwako,nenda kapange gesti na hutaona mambo kama hayo.Muombe Mungu hizo chale zisiwe na madhara na watakiwa kuzidisha maombi zaidi.
 
Du pole kaka, hama kwa huyo mtu beba vitu vyako vyote usimwachie chochote kilicho chako hata kitambaa cha mkono chukua na hata picha usimwachie then nenda kapange gest ya mbali na hapo huku ukiendelea kumwomba mungu. kuhusu hizo chale pole hizo huwa hazitoki labda ujaribu vipondozi vya alovera.
 
kaka hama haraka hapo
huyo rafiki yako sio mzuri!!

kusini nakujua sana

hawakawii watakutumia radi mchana kweupe
 
Wadau naomba msaada wenu.
Nipo kikazi huku kusini mwa Tanzania. ni karibia wiki moja sasa, na nitakaa kwa wiki nne.
Mara ya kwanza nilifikia katika gest moja hivi ya kawaida tu. Lakini kuna rafiki yangu ambaye anaishi huku aliniomba sana nikafikie kwake.
Nami bila hiana nikakubali, sasa naishi kwakwe.
Sasa cha ajabu kila nikiamka asubuhi nakuta nimechanjwa mwilini yaani kama nilijikwaruza hivi kwenye michongoma. Mara ya kwanza nikapuuzia.
Jana kabla ya kulala, baada ya sala nikaamua kulala na kitabu cha dini ninayoiamini.
Lakini leo nimeamka asubuhi, hadi usoni sasa nimekuta nina alama za kuchanjwa chanjwa.
Nimemweleza rafiki yangu kasema ni mambo ya kishirikina tu endapo nitayapuuzia basi sitopata madhara yeyote.
Kwa mwenye kuwa familiar na mambo kama haya, nini mwisho wa haya yote yanayonikuta?
Nifanye nini mwenzenu kwani hofu inanizidi sasa.

nasikia siku hizi unalala na baibo ndani. Nilikuwa kusini pia ila ilikuwa shwari tu. Anayekufanyia hayo anakujua
 
Kabla ya kulala itia Damu ya Yesu, unajifunika kwa damu ya Yesu, unafunika kila mahali kwa damu ya Yesu, Milango Madirisha Kuta . Halafu ualala,Anzia Hapo.
 
Nakemea mapepo, kwa JINA LA YESU TOKAAA, naenda kinyume na nguvu za giza, kwa jina la YESU nashusha moto katika chumba chako, nashusha malaika walinzi wakulinde usiku kucha, wakufunike kwa damu ya YESU, wafunike Nyumba yote kwa damu ya YESU, Wanga wote watumbukie katika shimo la moto wa YESU. Shetwani shindwaaa kwa JINA LA YESU.AMEEEN!!
 
Kuna wadudu tu wanaotambaa hapo au panya kwa wingi, angalia vidole vyako vyaweza kutafunwa!
 
Wadau naomba msaada wenu.
Nipo kikazi huku kusini mwa Tanzania. ni karibia wiki moja sasa, na nitakaa kwa wiki nne.
Mara ya kwanza nilifikia katika gest moja hivi ya kawaida tu. Lakini kuna rafiki yangu ambaye anaishi huku aliniomba sana nikafikie kwake.
Nami bila hiana nikakubali, sasa naishi kwakwe.
Sasa cha ajabu kila nikiamka asubuhi nakuta nimechanjwa mwilini yaani kama nilijikwaruza hivi kwenye michongoma. Mara ya kwanza nikapuuzia.
Jana kabla ya kulala, baada ya sala nikaamua kulala na kitabu cha dini ninayoiamini.
Lakini leo nimeamka asubuhi, hadi usoni sasa nimekuta nina alama za kuchanjwa chanjwa.
Nimemweleza rafiki yangu kasema ni mambo ya kishirikina tu endapo nitayapuuzia basi sitopata madhara yeyote.
Kwa mwenye kuwa familiar na mambo kama haya, nini mwisho wa haya yote yanayonikuta?
Nifanye nini mwenzenu kwani hofu inanizidi sasa.

Ndibalema kwanza naomba uondoe hofu kwani kuna uwezekano mkubwa sio ushirikina! Jambo kama hili linapokupata inabidi utulie na usiamini limetokana na ushirikina. Mambo yote ambayo yanaoneka kama yana-base kwenye nguvu za kishirikina katika dunia ya leo huwa yana maelezo ya kisayansi. Nakushauri uwe mdadisi, mvumilivu na jasiri: kuchunguza mazingira ya sehemu ya nyumba ya huyo rafiki yako. Je kuna wadudu au mnyama yeyote ambae anaweza akaweka hizo alama mwilini mwako wakati umelala? Nguo ulizotumia kujifunika je? Godoro ulilolalia je? Kwa kifupi.... dadisi dadisi dadisi!!! Utashangaa utakapogundua sio uchawi...
 
yawezekana si ushirikiana au ni ushirikina coz uchawi hata bible inasema upo,cha msingi ni kuamini kuwa hakuna mchawi anayemshinda mungu,ukiamini hivyo wala huitaji kuhofia na kuwaza sana juu ya hayo.sali sana kwa imani nothing will harm you!
 
Wapendwa.
Nashukuru kwa mwazo yenu.
Jana jioni baada ya kazi nikarudi nyumbani kwa rafiki yangu nilipofikia. Nikamwambia rafiki yangu pamoja na mkewe (ambaye alikuwa ni mcheshi kwangu kipindi ambacho nipo pale) kuwa kutokana na sababu za kiofisi imenibidi nihame nikafikie kwenye hotel ambayo ofisi imetupangishia pamoja na staffs wengine ambao wamekuja leo kutoka Dar.
Rafiki yangu akawa mnyonge sana akawa ananisihi kama inawezekana niendelee kuwepo pale kwake. Cha kushangaza mkewe kwa sauti ya ukali akamwambia rafiki yangu "Unamlazimisha nini? Mwache aende" Rafki yangu alijiskia aibu lakini kiaina akawa anazuga ili ile sentensi aliyotoa shemeji ionekane kama ni utani tu.
Usiku wakati nipo gest niliyofikia akanitumia sms hii "...sory kwa kauli aliyotoa mama...lakini unahama kwa sababu ya ile issue uliyoniambia?" Nikamkatalia kata kata.
Kimsingi nimelala vizuri sana lakini moyoni najistukia kwani nahisi rafki yangu anaona kama nimewaona wao ni washirikina.
 
Usijali! Endelea kuomba, Mwamini Mungu yeye ndiye Mlinzi wetu.

Ndibalema pole sana ndugu yangu.
Ondoa hofu maana umeiweka hapa hii hoja na ni jukumu letu kusaidiana.
Awali kabisa nakushairi usihame hapo unapoishi. ila fanya yafuatayo.

Unapoingia kulala fanya sala (sikupi maneno ya kukariri ila vigezo vya sala) kwa mtiririko ufuatao.

  1. tumia dakika mbili mpaka tano ukimwomba msamaha Mungu kwa yale yote uliyoyafanya kinyume na mapenzi yake.
  2. tumia dakika tano hadi saba au zaidi kuwaombea ndugu zako walale salama, na usisahau viongozi wa nchi walindwe mwombee ulinzi na huyo mwenyeji wako.
  3. tumia dakika tano hadi kumi kuomba Mungu akupe ulinzi wewe utakapopanda kitandani, kataa ndoto za kishetani, kataa kutumiwa kichawi lakini kikubwa zaidi mweleze Mungu kwamba unapokuwa unakitumia chumba hicho unavunja mikataba yoyote iliyowahi kufanywa ndani ya chumba hicho na nyumba hiyo, Vunja mikataba yote ya kishetani ya kichawi hata ya kihalifu.
  4. Mweleze Mungu kuwa unapolala atume malaika walinzi wakulinde na walinde boma.
nakwambia ukiomba kwa kuamini hakika ahsubuhi kesho utatuletea new story hapa.

Kuhusu kuchanjwa just do it ktk maombi kuvunja mkataba na chain yoote iliyoungwa ili kukuconect. Kataa kwa Jina la Yesu nawe utakuwa salama, zaidi ya hapo tegemea maumivu.

NB. Utakaposema uhame, huko uendako wanakungoja hakuna pa kujificha mbele ya shetani zaidi ya kumkimbilia Mungu kupitia Yesu kristo
 
yawezekana si ushirikiana au ni ushirikina coz uchawi hata bible inasema upo,cha msingi ni kuamini kuwa hakuna mchawi anayemshinda mungu,ukiamini hivyo wala huitaji kuhofia na kuwaza sana juu ya hayo.sali sana kwa imani nothing will harm you!

@ Cheusi Mungu au Yesu? Maana naona kila mtu kasema Yesu sijajua nani ana nguvu zaidi kwa hao walio sema Yesu naomba nifahamishwe....
 
ukienda sehemu jaribu kufikia hotelini achana na mambo ya kwenda kwa marafiki maana posho ya malazi na kujikimu ulipewa sasa wewe ukahamua kuzichanga kwa kwenda kuishi kwa rafiki yako ambapo yamekukuta makubwa zaidi ya hiyo posho. Next time ukusafiri kikazi kaa hotelini kama ni ndg, jamaa na marafiki watembelee tu jioni kisha rudi hotelini kwako
 
Pole kaka, kamua kiti moto mzeya lazima huyo mwanga asepe, ikiwezekana jipake mafuta yake.
 
Ndibalema pole sana ndugu yangu.
Ondoa hofu maana umeiweka hapa hii hoja na ni jukumu letu kusaidiana.
Awali kabisa nakushairi usihame hapo unapoishi. ila fanya yafuatayo.

Unapoingia kulala fanya sala (sikupi maneno ya kukariri ila vigezo vya sala) kwa mtiririko ufuatao.

  1. tumia dakika mbili mpaka tano ukimwomba msamaha Mungu kwa yale yote uliyoyafanya kinyume na mapenzi yake.
  2. tumia dakika tano hadi saba au zaidi kuwaombea ndugu zako walale salama, na usisahau viongozi wa nchi walindwe mwombee ulinzi na huyo mwenyeji wako.
  3. tumia dakika tano hadi kumi kuomba Mungu akupe ulinzi wewe utakapopanda kitandani, kataa ndoto za kishetani, kataa kutumiwa kichawi lakini kikubwa zaidi mweleze Mungu kwamba unapokuwa unakitumia chumba hicho unavunja mikataba yoyote iliyowahi kufanywa ndani ya chumba hicho na nyumba hiyo, Vunja mikataba yote ya kishetani ya kichawi hata ya kihalifu.
  4. Mweleze Mungu kuwa unapolala atume malaika walinzi wakulinde na walinde boma.

nakwambia ukiomba kwa kuamini hakika ahsubuhi kesho utatuletea new story hapa.

Kuhusu kuchanjwa just do it ktk maombi kuvunja mkataba na chain yoote iliyoungwa ili kukuconect. Kataa kwa Jina la Yesu nawe utakuwa salama, zaidi ya hapo tegemea maumivu.

NB. Utakaposema uhame, huko uendako wanakungoja hakuna pa kujificha mbele ya shetani zaidi ya kumkimbilia Mungu kupitia Yesu kristo
Ndibalema mpendwa,pole kwa yote lkn una Mungu aliye mkuu kuliko vyote mtumaini yeye pekee.Mtiririko aliokupa Msanii ni mzuri sana kuufuata wakati wa prayer,nami nakuomba baada ya no 1(TOBA),basi no 2:iwe shukrani,kumshukuru Mungu kwa yote yaliyofanyika kwako na hata kwa wengine kwa cku hiyo eg ulinzi,baraka,etc.Baada ya hapo endelea na mtiririko mzima according to Msanii.HESABU 23:23 inasema kuwa "Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo wala hapana uganga juu ya Israel"sasa while praying hapo kny Yakobo weka jina lako na kny Israel waweza eka kazi yako or family.Vile vile nakupa neno kutoka Psalm 4:8 "Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara maana wewe,Bwana peke yako ndiwe unijaliaye kukaa salama".
Mungu akutie nguvu na akuhifadhi:smile-big:
 
Wadau naomba msaada wenu.
Nipo kikazi huku kusini mwa Tanzania. ni karibia wiki moja sasa, na nitakaa kwa wiki nne.
Mara ya kwanza nilifikia katika gest moja hivi ya kawaida tu. Lakini kuna rafiki yangu ambaye anaishi huku aliniomba sana nikafikie kwake.
Nami bila hiana nikakubali, sasa naishi kwakwe.
Sasa cha ajabu kila nikiamka asubuhi nakuta nimechanjwa mwilini yaani kama nilijikwaruza hivi kwenye michongoma. Mara ya kwanza nikapuuzia.
Jana kabla ya kulala, baada ya sala nikaamua kulala na kitabu cha dini ninayoiamini.
Lakini leo nimeamka asubuhi, hadi usoni sasa nimekuta nina alama za kuchanjwa chanjwa.
Nimemweleza rafiki yangu kasema ni mambo ya kishirikina tu endapo nitayapuuzia basi sitopata madhara yeyote.
Kwa mwenye kuwa familiar na mambo kama haya, nini mwisho wa haya yote yanayonikuta?
Nifanye nini mwenzenu kwani hofu inanizidi sasa.

Nakumbuka mwaka 2007 nilienda kikazi mtwara nikalala gesti moja jirani na benki ya nmb mtwara mjini duu ilikuwa kasheshe usiku mzima sikulala kabisa maana kitanda kilikuwa kinatikisika kama vile mtu chini anakitingisha na hii hali ilikuwa ikitokea nikizima taa tu asubuhi nikahama ile gesti
 
Kama kifaa alichochanjiwa hakijawa sterilized ndo ka infection kanaweza kutokea au....?
kuwa jasiri muombe Mungu utashinda.....lala hapohapo usitoke hilo ni jaribu la shetani.....
 
Back
Top Bottom