Mwenza wa maisha (Mume) anahitajika

Haliu

Member
Oct 20, 2012
8
6
Habari zenu wana JF.
Jamani maisha ni safari ndefu na yanahitaji ustaamilivu na ujasiri. Napenda kuchukua fursa hii kwa mara ya kwanza kujitokeza katika jukwaa hili ili kuweza kupata mwenza ambae atakuwa mume kama M/mungu ataleta heri. Kwa aliye na nia ya dhati haswa naomba tuwasiliane kwa private message.

Sifa zangu
Umri: Miaka 31
Umbo:Ni mwembamba kiasi
Urefu:1.52m
Rangi: kahawia
Elimu: Degree mbili
Kazi: Muajiriwa
Dini:muislam

Sifa za Mtarajiwa
Umbo: wastani, si mnene si mwembamba
Urefu: ni vizuri kama atanizidi urefu
Rangi: yeyote
Elimu: Degree
Kazi: Ni muhim, maisha kusaidiana
Dini: Muislam, ila uwe hujaoa!

Umri: 33-39
Tafadhali wana JF hili si jambo la mdhaha, naomba tuweke kando mzaha, nia ni kujenga. Nipo tayari kwa maswali, karibuni

Enjoyments pass while consequences remain
 
Wanangu siku hizi mnafanya mambo rahisi kuwa magumu. Haya mambo ya elimu na dini naona ni kama kukuza mambo maana ndoa haina dini wala elimu bali mapenzi na sifa nzuri. Anyways endeleeni mtawapata wenye hivyo vitu lakini mabomu. Sifa ulizotaja nakushauri uende kwenye chuo cha Manzese uulizie wasichana wa kipare waislam. Wapo wengi wanavaa tena niqab ingawa ni jiko la mchina linapokuja suala la kugawa hayo mambo yenyewe.
 
Ungekua umepungua Umri labda kwa miaka mi-3 hivi ningekufikiria. Maana kwa umri huo ukweli tunalingana!!
 
Mashallah! Shungi hiyo bwana inanipita hivi hivi Mungu wangu, ila ok! all the best..............maana sisi wengine maskini wa bahati humu.
 
nI KWELI WATU WENGINE WANAPENDA KUTUMIA NJIA HII ILI KUPATA MWENZA LAKINI UNAPOWEKA VIGEZO VYOTE HIVYO NI VIGUMU KWANI YAWEZEKANA KUWA VIGEZO HIVYO HIVYO NDIVYO VIMEKUFANYA UFIKE HAPO BILA KUPATA WA KU-SHARE NAYE HII RAHA YA DUNIANI. MAISHA NI MKATABA MKAKATI KATI YA WAWILI WALIOCHANGIA UPEO WAO. JIJADILI KWANZA.
 
Duh, hiyo profile kubwa kumzidi hata naibu waziri mulugo bado hujapata mchumba au umekula kibuti, kunana
 
Kwa kweli hata mimi nimeweka kando mzaha, nikutakie kila la kheri
 
nasikitika hukua makini wakati unasoma huu ujumbe, niqab wanavaa wanawake, nami ni mwanamke, inamaana nitafute mwanamke mwenzangu?
 
Wanangu siku hizi mnafanya mambo rahisi kuwa magumu. Haya mambo ya elimu na dini naona ni kama kukuza mambo maana ndoa haina dini wala elimu bali mapenzi na sifa nzuri. Anyways endeleeni mtawapata wenye hivyo vitu lakini mabomu. Sifa ulizotaja nakushauri uende kwenye chuo cha Manzese uulizie wasichana wa kipare waislam. Wapo wengi wanavaa tena niqab ingawa ni jiko la mchina linapokuja suala la kugawa hayo mambo yenyewe.

Nasikitika hukua makini wakati unasoma huu ujumbe, niqab wanavaa wanawake nami ni mwanamke, unamaanisha nitafute mwanamke mwenzangu?
 
nasikitika hukua makini wakati unasoma huu ujumbe, niqab wanavaa wanawake, nami ni mwanamke, inamaana nitafute mwanamke mwenzangu?

Kinachoniskitisha ni vigezotu vinakua vingi sana.sijawah kusikia mt anatafuta mke mume bila vigezo vya sijui elimu kubwa.inamaana mwenye elim ya juu ndie mumebora?kama umuislam kweli rejea khadith na aya ndani ya quran tayari mungu ametufundisha mume na mke bora niyupi.usiwe na tamaa ya dunia
 
Si tamaa, mara nyingi mume anapokua na elimu ndogo, kumuelewesha/ kufanya maamuzi ni shida kitu hata kama kina faida anaona unamdharau, samahani kwa kukukwaza.
 
Si tamaa, mara nyingi mume anapokua na elimu ndogo, kumuelewesha/ kufanya maamuzi ni shida kitu hata kama kina faida anaona unamdharau, samahani kwa kukukwaza.

Hujanikwaza mimi nafikiri ndoa nyingi hua hazidumu kwa sababu kama hizi tunajifanya tunaenda kizungu zaidi.lakini kama tungeangalia nyuma kwanini wazazi wetu wameweza kuzeeshana wao walitumia njia gani kuoa au kuolewa tusingekua na talaka na usaliti kama leo.sikweli kwamba asiyekua na elim hana akili wala mwenye elim ana akili sana.wangapi hawana elim na wana maisha mazuri?wangapi wenye elim na hawana maisha mazuri?mimi nakushauri rudi kwenye vitabu mrejee mungu akupe mume mwema.huyo atakaye kupa yeye ndie mwemakwako,unaweza kumpata hata mwenye elim zaidi ya hiyo mwisho wa siku ukaaja juta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom