Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete akiwa Arizona!!!

Waliofaidika wapo kibao tu, nenda kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji utakuta shule ya kisasa imejengwa hapo zaidi ya bilioni 1.9 zimetumika na aliezitafuta ni yeye m/k wa WAMA Mhe Mama Salma Kikwete. Shule hiyo imechukua wanafunzi wa kike toka mikoa yote Tanzania nzima bara na visiwani ni shule pekee kwa wote. Wanafunzi hao ni wale wa familia duni na yatima. Wanagharimiwa kila kitu kuanzai ada,sare za shule na vyakula n.k wao kazi yao ni kusoma tu.

Wanawake wengine waliofaidika ni toka mikoa yote ya Tanzania kupitia ziara zake za mikoani mama Salma Kikwete alitoa misaada ya vifaa vya uzazi na vya kutolea huduma ya afya vyenye thanmani ya zaidi ya Milioni 300 katika vituo vya Afya 66 Nchi nzima . Na pia alichangia vikundi vya kina mama zaidi ya Milioni 152 . Pesa hizi zote hazikutoka Ikulu zimechangwa na Wasamalia wema wanaovutiwa na jitahada zake nae hazibania amerejesha kwa Wananchi husasan akina mama . Mwenye kutaka data kamili atembelee WAMA atapatiwa taarifa za Fedha na hesabu zilizokaguliwa WAMA inazingatia utawala bora , MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI MAMA SALMA KIKWETE AMETEKELEZA WAJIBU WAKE KAMA MAMA WA TAIFA

hongera zake....
 
mie nimesikiliza hio clip amejitahidi sana,wengi tunaongea kingereza lakini kuongea na members of the public ni noma sana sidhani kama tunaweza,hivyo mama salma hongera kwa kujikakamua.:director:
 
Nashangazwa na kitu kimoja ukienda kwenye youtube search hiyo Thunderbird School of Global Management ina lots of clips, lakini hizo za fl wetu hazipo kwa nini?
 
Nashangazwa na kitu kimoja ukienda kwenye youtube search hiyo Thunderbird School of Global Management ina lots of clips, lakini hizo za fl wetu hazipo kwa nini?

Yaani mpaka wanafunzi wa jioni wa hiyo taasisi kuna clips za video zao sasa iweje ya fl yetu hata moja haiwekwi?
 
hongera zake....

Ni kweli anastahili hongera sana, maana si hayo tu licha ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana anasomesha watoto wa kike toka familia duni na yatima tangu ameingia madarakani product ya kwanza ni mwaka 2010 ambapo jumla ya wanafuzi 126 walihitimu kidato cha nne ambao walifadhiliwa na WAMA kwa miaka yote minne kila mwaka laki tatu kwa mwanafunzi mmoja, kati ya hao wanafunzi kumi na saba wamechaguliwa kwenda kidato cha tano. Wanafunzi hao 126 ni toka mikoa yote, waliobaki watapata post za vyuo vya ualimu ,maendeleo ya jamii ,uuguzi n.k bila ya mhe mama salma watoto hawa wa kike wangekosa fursa ya kuendelea na pengine wangepata mimba za utotoni n.k

Bado WAMA Inasomesha wanafunzi zaidi ya 120 waliopo Kidato cha Tatu shule mbalimbali hapa nchini. Wapo wachache ambao wamedhaminiwa vyuo vikuu vya hapa nchini.

Upande wa Afya ameisaidia ametafuta mfadhili ambae alitoa milioni 200 akawakabidhi MEWATA kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Hospital itakayoshughulika na Saratani za kina mama , mkitaka uhakika Nendeni MEWATA watafahamisha. Ingekuwa mtu mwenye tamaa hizo pesa angechukua na kujengea apartments kama Investment.

Kupitia pia Taasisi ya kwake WAMA amejenga kituo cha Afya ya kijiji cha Hoyoyo Mkuranga chenye Thamani ya zaidi ya milioni 145 kwa kupitia Mkandarasi aliechaguliwa kwa taratibu za manunuzi karibu inakamilika.

Ujenzi wa hicho Kituo cha Afya hautokani na pesa za Ikulu la hasha ni za Wasamaria wema , orodha yao ipo , je kama hana nia ya kuwasaidia watanzania hususan wanawake angeyafanya haya.

Amefanya ziara nchi nzima pamoja na kufanya shughuli za WAMA, kupitia ziara hizo ameongea na wanafunzi katika maeneo yote aliyotembelea kuwanasihi juu ya kujiepusha na mimba za utotoni, ukimwi na kusoma kwa bidii, je f/lady gani aliewahi kufanya haya ? sio tu tanzania hata ktk nchi zingine bara afrika au hata huko kwenye mataifa yaliyoendelea.

Kimsingi hapa JF wakati mwingine mama wa Taifa anashambuliwa kwa ushabiki tu na kwa kutokufahamu, naamini wahenga walisema JAMBO USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA ! Wana JF tuzingatie NO DATA NO RIGHT OF SPEAKING !
 
Mnyonge mnyongeni haki yake... Alikusanya shule za Zanaki, Jangwani, Kisutu, Azania, zilikuwa shule sita hivi akawapelekea zawadi ya Jezi tatu (3) za michezo. Sijui wakuu wa shule waligawanavipi
 
Mnyonge mnyongeni haki yake... Alikusanya shule za Zanaki, Jangwani, Kisutu, Azania, zilikuwa shule sita hivi akawapelekea zawadi ya Jezi tatu (3) za michezo. Sijui wakuu wa shule waligawanavipi

Waligawana kupitia mashindano ya michezo kuibua vipaji , mshindi wa kwanza,pili na watatu walistahili zawadi . Mbona umeona zawadi ya jezi tu ? Je nasaha akizotoa hasa kwa watoto wakike juu ya 3JS{JITAMBUE, JILINDE,JIPENDE ) sio zawadi ? Wabongo hamjambo.
 
Back
Top Bottom