Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela afariki dunia

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Habari zilizonifikia sasa hivi ni kwamba Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela bwana Japhet Mwakasumi amefariki dunia asubuhi hii.

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.
 
Poti,

Kama huna uhakika nadhani ingekuwa ni vizuri ukasubiri, sasa kama ikitokea kuwa sio kweli utafanyaje? Angalizo tu
 
Kwa kweli hii pronouncement imetoka prematurely maana kama source iliyommegea ni ya uhakika basi kulikuwa hakuna haja ya kutuomba tufanye subira kupata confirmation. Labda na mimi nitapenda kujua, kama kifo hicho kinatoa mabadiliko yoyote kwa siasa za uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Kyela.
 
Kwa kweli hii pronouncement imetoka prematurely maana kama source iliyommegea ni ya uhakika basi kulikuwa hakuna haja ya kutuomba tufanye subira kupata confirmation. Labda na mimi nitapenda kujua, kama kifo hicho kinatoa mabadiliko yoyote kwa siasa za uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Kyela.

Utayapata tu subiri, wewe mwombe MOD asifunge hii thread!
 
Hii habari sasa ni confirmed. Mzee wetu Japhet Mwakasumi ameaga dunia asubuhi ya leo akiwa Dar.

Mungu ailaze roho yake mahali pema, amen.

Invisible naomba ondoa tetesi.

Mkuu Shalom,

Kutokuwa na uhakika na kutokuwa na confirmation ya asilimia 100 ni maneno tofauti sana. Ndio maana niliweka tetesi ili nijiridhishe kwa asilimia 100. Ni hayo tu kwasasa, vinginevyo tuwape pole ndugu na marafiki wote wa Mwakasumi.

Nilikutana na mzee Mwakasumi nilipokuwa TZ mwezi March. Alikuwa na afya yake njema kabisa. Inasemekana ni kisukari au BP ndio imemuua. Pole sana kwa ndugu, marafiki na wana Kyela wote.
 
Ameugua gafla?
Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu.

Fidel80,

Nafikiri ameumwa kwa muda. Hivi karibuni kulikuwa na vikao muhimu sana vya CCM wilayani Kyela na vyote hakuhudhuria kwasababu ya kuumwa.

Tatizo la BP au Kisukari, hata ukimwona mtu barabarani ni ngumu kujua kwamba anaumwa.
 
IT is the begining, Huko kyela sindo kuna vuta nikuvute ile ya nanihiiiii..........na busega nako kama hilo nimetukia, what, who is next.
 
Oooh maskini jamani nimesikitika...ametuacha kipindi kigumu cha kuelekea uchaguzi wakati ambapo huenda mchango wake ndani ya chama chake ungehitajika sana! Sijui aliku PRO au ANT mwakyembe jamani?! sijui alikuwa hana makundi? Naogopa kusema MUNGU amlaze au asimlaze pema kwani sidhani kama nimeruhusiwa kumshauri /kumuomba MUNGU juu ya hukumu zake....huu ni mtazamo wangu tu
 
RIP Mzee Japhet,

wakazi wa kitunda machimbo tutakukumbuka kwani ulituuzia mashamba/viwanja ambako tumejenga makazi yetu ya kuishi.
 
Fidel80,

Nafikiri ameumwa kwa muda. Hivi karibuni kulikuwa na vikao muhimu sana vya CCM wilayani Kyela na vyote hakuhudhuria kwasababu ya kuumwa.

Tatizo la BP au Kisukari, hata ukimwona mtu barabarani ni ngumu kujua kwamba anaumwa.

Pole mkuu najua kwa namna moja ama nyingine nipigo sana kwa Wanakyela.
Pole sana tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu.
 
Kazi ya mola haina makosa.BW.ametoa na tena ametwaa jina lake libaliwe,Amina
 
Pole sana kwa ndugu, marafiki na wana Kyela wote. Bwana alitoa na bwana ametwaa, kazi yake haina makosa.

Mkuu wa mkoa John Mwakipesile ambaye naye ni mwenyeji wa Kyela alikuwa hoi sana kwa Kisukari wiki chache zilizopita na madaktari wanasema aliponea bahati maana hali ilikuwa mbaya sana, alikuwa hata hawezi kuona. Kwasasa amepata nafuu. Tunamtakia na yeye heri ili apate nafuu haraka na kuendelea na majukumu yake.
 
Maskini Mzee Mwakasumi. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pema peponi, Amen na aipe faraja familia yake katika wakati huu wa majonzi makubwa.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi na kuwapa faraja familia ndugu na jamaa wakati huu wa majonzi. Amina.
 
Ni wakati mgumu sana kwa wanakyela, hasa kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi. Kwani ni kipindi ambacho msaada wake katika kulitumikia taifa na chama unahitajika sana. Poleni wanakyela wenzangu, Poleni wanachama wenzangu na pia poleni watanzania wenzangu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.
 
Back
Top Bottom