Mwenyekiti wa CCM Morogoro ampiga askari Msamvu kisa kasimamishwa na traffic

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Source ITV

Hivi kumbe hata wenyeviti wa vyama nao wanatumia madaraka yao kuiwajibisha dora kama mwenyekiti wa ccm mkoa wa morogoro (Mr. Kingu) kumchapa askari wa usalama barabarani kisa kasimamishwa hii imekaaje jamani
 
amejisahau anadhani zama hizi ni enzi zile za chama kushika utamu oohh!!!!!!!! sorry hatamu. HUYO inatakiwa akamatwe tu na kupelekwa mahakamani ajibu mashtaka. REMEMBER NO BODY IS ABOVE THE LAW
 
Source ITV

Hivi kumbe hata wenyeviti wa vyama nao wanatumia madaraka yao kuiwajibisha dora kama mwenyekiti wa ccm mkoa wa morogoro kumchapa askari wa usalama barabarani kisa kasimamishwa hii imekaaje jamani

mbwa wa mfalme ni mfalme wa mbwa wote
 
Huyo mjomba km amepiga kweli na mahakama ikizibitisha aende jela,ugali mbele mboga nyuma. Maana angekuwa kiongoz wa upinzan ingekuwa balaa.
 
Jk ni mwenyekiti wa ccm taifa=na amiri jeshi mkuu kwa hiyo Kingu ni mwenyekiti wa ccm mkoa=na amiri jeshi wa mkoa.

JK anapata kofia ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu kwa kuwa ni Rais. Mwenyekiti wa CCM Mkoa, ni kiongozi wa chama pekee, na huwa hawamo hata kwenye orodha ya watu ambao wanatakiwa kupigiwa salute na askari.

Bottom line ni kwamba viongozi wengi wa CCM wamelewa madaraka kiasi kwamba wanajiona wako juu ya sheria. Hii inatokana na viongozi wa Jeshi la Polisi kuwa na uswahiba na serikali. Ndio maana Bwana Robert Kisena (mgombea wa ubunge huko Maswa mwaka 2010) alimpiga kibao Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Maswa na hakukuwa na kesi yoyote. Akina Mwema na Chagonja wanachekelea tu huku mhusika akisema hewala Bwana.
 
La la la! Ama kweli haya Majambazi CCM yamefika pabaya, yani mpaka huyu mwendawazimu anampiga trafic? Na yule Abood anayetoaga mabasi kwenye misiba kasema nini juu ya hili? Kweli nimeamini ccm ni chama la majambazi(comfirmed)
 
Ulevi wa madaraka utaadhibiwa kwa hasira iliyo kuu,unaweza kupuuza kwa kuona hili ni kosa la mtu binafsi,lakini kwa hali ilivyo sasa tunaweza kuunganisha dots na kuhitimisha kua ccm imelewa madaraka hivyo inaona walioiweka madarakani si kitu hata kidogo
 
La la la! Ama kweli haya Majambazi CCM yamefika pabaya, yani mpaka huyu mwendawazimu anampiga trafic? Na yule Abood anayetoaga mabasi kwenye misiba kasema nini juu ya hili? Kweli nimeamini ccm ni chama la majambazi(comfirmed)
Viongozi wa CCM wamefanya yafuatayo bila kuchukuliwa hatua:
1. kuchukua mke wa Mtu na kufamaniwa na mwenyewe (Mwigulu)
2. Kutukana hadhrani (Lusinde)
3. Kuchukua changudoa na kupoteza nyaraka za serikali ( Malima)
4. Kumiliki silaha ya kivita (Malima)
 
Hapa nimecheka sana.
Baada ya kisa mkasa. Askari wamezowea
kutupiga bila ya kuchukuliwa hatua.
Nimefurahi kuwa kuna mtu anayethubutu
kuwapiga na wao bila ya kuchukuliwa hatua.
Hongera Mkuu wa CCM mkoa.
 
Source ITV

Hivi kumbe hata wenyeviti wa vyama nao wanatumia madaraka yao kuiwajibisha dora kama mwenyekiti wa ccm mkoa wa morogoro (Mr. Kingu) kumchapa askari wa usalama barabarani kisa kasimamishwa hii imekaaje jamani

Hilo ndio tatizo ndani ya ccm,unajiona kam Mungu mtu vile(Kama raisi hawezi kushitakiwa ikiwa aliwahi kufanya makosa Kama ya wizi Wa Mali ya uma ktk enzi za utawala wake!!!!?)angemvunja kbs huyo trafic polisi sbb wamezidi kuwatetea hawa watu Wa nguo za kijani.
 
Una uhakika amempiga kisa yeye ni mwenyekiti wa CCM mkoa?
 
Back
Top Bottom