Mwenyekiti wa CCM kata ya Ngokolo (Shinyanga) ajiuzulu huku akikituhumu chama chake

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Mkiti wa ccm kata ya Ngokolo mkoa wa Shinyanga amejiuzulu huku akikutuhumu CCM kuwa kimezidiwa na makundi yanayokiathiri chama hicho.

Ogweno amesema amejiuzulu kwa sababu Chama hicho kinaendekeza makundi na amechoka kuvumilia baadhi ya vitendo vinavyofanywa na viongozi wa wilaya.

'Mimi kwa msimamo wangu sipendi makundi, wenzangu walipoona hivyo wakaanza kunizonga, majungu, kunichafua na kuniharibia heshima mbele ya Chama'.

Ndani ya ccm nina mchango mkubwa tangu TANU Youth Leaque 1972. Pia ni mwanachama mwanzilishi wa ccm.

Katibu wa CCM wilaya shinyanga mjini alipoulizwa hakuweza kukataa wala kukubali badala yake alimwomba mwandishi aachana na mkiti huyo (Ogweno)
Naye mkiti wa ccm wilaya alipoulizwa alisema hata mimi ninatengwa na viongozi wa wilaya kwa sababu tu nilitoa udhaifu wa baadhi ya viongozi wenzangu wa wilaya kwa naibu katibu mkuu John Chiligati.

”Sasa hivi hata mimi natengwa. Viongozi wa kata wameambiwa wasinishirikishe chochote (Hakusema nani aliwaelekeza viongozi hao wa kata wasimshirikishe chochote) hadi akalalamikia ngazi ya mkoa.”

Hata hivyo, Ogweno hakutangaza nia ya kujiunga Chadema wala ya kubaki ccm. Amewaacha wanaccm njia panda.

My take;
CCM naona sasa hakukaliki tena. Mkiti wa wilaya naye anamlalamikia nani?

Juzi jumpili hapa Dsm kada maarufu wa ccm aliyejiunga chadema (jina liko kwenye thread nyingine -nimesahau) alisema ccm kata ya Pugu (nyumbani kwa Pinda) haina wagombea (si wapiga kura) wa nafasi za jumuiya ya wazazi ngazi ya kata.

Je, huu siyo uthibitisho wa wazi kuwa ccm imefika mwisho?
 
Magamba wanatakiwa wajiandae kuwa wapinzania kama tlp 2015
 
Nape mkumbushe huyo mwenyekiti wako amechana gamba ameshindwa kuvaa uzalendo.
 
CDM mwendo mdundo.... Ukitaka kuuangusha Mti kirahisi unang'oa mizizi ili ukisukumwa na upepo unaanguka wenyewe....
 
Nape mkumbushe huyo mwenyekiti wako amechana gamba ameshindwa kuvaa uzalendo.
 
Bwana,Ogweno au ni gamba lenu limewaka moto? Kwa nini usivumilie tu? Au na wewe ni oil chafu? Kama alivyosema Nepi?
 
Kweli CCM inaelekea kufa kila siku wanachama wake wanakihama mpaka tunafika 2015 tayari CCM itakuwa imeisha kufa huku ikisubiri kuzikwa.
 
Mkiti wa ccm kata ya Ngokolo mkoa wa Shinyanga amejiuzulu huku akikutuhumu CCM kuwa kimezidiwa na makundi yanayokiathiri chama hicho.

Ogweno amesema amejiuzulu kwa sababu Chama hicho kinaendekeza makundi na amechoka kuvumilia baadhi ya vitendo vinavyofanywa na viongozi wa wilaya.

'Mimi kwa msimamo wangu sipendi makundi, wenzangu walipoona hivyo wakaanza kunizonga, majungu, kunichafua na kuniharibia heshima mbele ya Chama'.

Ndani ya ccm nina mchango mkubwa tangu TANU Youth Leaque 1972. Pia ni mwanachama mwanzilishi wa ccm.

Katibu wa CCM wilaya shinyanga mjini alipoulizwa hakuweza kukataa wala kukubali badala yake alimwomba mwandishi aachana na mkiti huyo (Ogweno)
Naye mkiti wa ccm wilaya alipoulizwa alisema hata mimi ninatengwa na viongozi wa wilaya kwa sababu tu nilitoa udhaifu wa baadhi ya viongozi wenzangu wa wilaya kwa naibu katibu mkuu John Chiligati.

”Sasa hivi hata mimi natengwa. Viongozi wa kata wameambiwa wasinishirikishe chochote (Hakusema nani aliwaelekeza viongozi hao wa kata wasimshirikishe chochote) hadi akalalamikia ngazi ya mkoa.”

Hata hivyo, Ogweno hakutangaza nia ya kujiunga Chadema wala ya kubaki ccm. Amewaacha wanaccm njia panda.

My take;
CCM naona sasa hakukaliki tena. Mkiti wa wilaya naye anamlalamikia nani?

Juzi jumpili hapa Dsm kada maarufu wa ccm aliyejiunga chadema (jina liko kwenye thread nyingine -nimesahau) alisema ccm kata ya Pugu (nyumbani kwa Pinda) haina wagombea (si wapiga kura) wa nafasi za jumuiya ya wazazi ngazi ya kata.

Je, huu siyo uthibitisho wa wazi kuwa ccm imefika mwisho?

Tatizo la Shinyanga ni Mwenyekiti wa CCM mkoa yaani Mgeja, huyu bado yupo enzi za chama kushika hatamu na kibaya zaidi ni kujaribu kulazimisha wanaCCM wote Shinyanga wawe kundi la Lowassa na hapo ndipo CDM inapopata uchochoro kiulaini, SIKILIZIENI MAUMIVU 2015
 
Kweli CCM inaelekea kufa kila siku wanachama wake wanakihama mpaka tunafika 2015 tayari CCM itakuwa imeisha kufa huku ikisubiri kuzikwa.
 
Unapoona Magamba yanakimbiwa na watu hata wapole na wasiotaka vurugu ujue enzi mpya yaja.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom