Mwenyekiti wa CCM kata ya Msagati ahamia CHADEMA huko Ifakara katika operesheni ya m4c

Huo ndio nauita ushujaa...wako wengi ambao hawana ujasiri wa kufanya maamuzi magumu kama hayo lakini taratibu M4C inaanza kuwajengea ujasiri kwa kuwatoa hofu. Wananchi wengi, kwa woga wa kulinda maslahi binafsi, husita kuchukua maamuzi sahihi kwa swali la je, upande ambako wamejikuta kwa sababu moja ama nyingine ndiko upande ambako kwa kweli wangependa wawepo? Nina imani kuwa hadi tunafika mwaka 2015 jibu la swali la kwa nini kuna watu wanaendelea kubaki walipo litakuwa dhahiri hata kwa kipofu.

Kwamba hadi dakika hii kuna watu ambao, bila hata chembe cha aibu, wanao uthubutu wa kusimama mbele ya jamii na kuitetea CCM, ni jambo linalofedhehesha kwa kweli. Inakuwaje mtu huyo huyo analalamikia hali ngumu ya maisha, analalamikia rushwa na ufisadi uliokubuhu, analalamikia utawala dhaifu usiowajibika, analalamikia sheria zisizozingatia haki na usawa na mengine mengi tu...halafu bila haya wala soni anatetea uongozi wa chama tawala na serikali huku akibeza juhudi zozote zile za kupambana na hali hiyo!

Time is running out...na mtu yeyote ambaye anaendelea kuikumbatia CCM kwa sababu zozote zile za ovyo kama eti chama kujivua gamba au kupiga vita ufisadi ndani ya CCM, ni mlafi, mnafiki na adui mkubwa wa taifa. Tuko hapa tulipo kwa sababu ya CCM, si Chadema...ni CCM na serikali yake, ni CCM na sera zake, ni CCM na ufisadi wake, ni CCM na uongozi wake, ni CCM na ahadi zake, ni CCM na udanganyifu wake, ni CCM na...Watanzania tumekuwa mateka ndani ya taifa letu, tuko jela na wengine kama mazuzu wanashangilia, OMG!
Big like
 
Kule ni mbali kweli kweli. Mpakani mwa Morogoro na Iringa/Njombe katibu na Taweta. Ni eneo tajiri sana hadi kakao inalimwa huko.

Ndiko huko huko mkuu, mara nyingi watu wa ifakara huwa tunaenda huko kwani kuna mashamba yetu, ni very bush
 
Mikutano ya Operesheni Sangara huko Ifakara


source: chadematv ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Ndiko huko huko mkuu, mara nyingi watu wa ifakara huwa tunaenda huko kwani kuna mashamba yetu, ni very bush

Mkuu niliwahi kwenda huko katika shughuli za kusaka ardhi. Nakumbuka kukutana na Diwani mmoja pale Mpanga ni wa CDM nadhani anaitwa Kibiki au jina linalokaribiana na hilo. Nadhani huyu ndiye Diwani hadi Masagati kama sikosei.
 
Back
Top Bottom