Mwenyekiti wa CCM kata ya Msagati ahamia CHADEMA huko Ifakara katika operesheni ya m4c

Ndani ya matatizo lukuki yaliyoletwa na Chama Cha Mambwepande, M4C gives me a reason to smile.
 
Nyie watu mnamtaki mema kweli Mkuu Ritz kutia mguu hapa kwa ID yake ya siku zote wakati anajua fika maji tayari yako kwenye mustach wazee?
 
M4c haitawabakiza kamwe!


Ninahisi kuna kipindi watajinyonga wengine wakisia M4C inatua kipande yao!
 
Tena kata hiyo iko interior sana. Hapo tujue mabadiliko yamefikia pazuri.
 
Huo ndio nauita ushujaa...wako wengi ambao hawana ujasiri wa kufanya maamuzi magumu kama hayo lakini taratibu M4C inaanza kuwajengea ujasiri kwa kuwatoa hofu. Wananchi wengi, kwa woga wa kulinda maslahi binafsi, husita kuchukua maamuzi sahihi kwa swali la je, upande ambako wamejikuta kwa sababu moja ama nyingine ndiko upande ambako kwa kweli wangependa wawepo? Nina imani kuwa hadi tunafika mwaka 2015 jibu la swali la kwa nini kuna watu wanaendelea kubaki walipo litakuwa dhahiri hata kwa kipofu.

Kwamba hadi dakika hii kuna watu ambao, bila hata chembe cha aibu, wanao uthubutu wa kusimama mbele ya jamii na kuitetea CCM, ni jambo linalofedhehesha kwa kweli. Inakuwaje mtu huyo huyo analalamikia hali ngumu ya maisha, analalamikia rushwa na ufisadi uliokubuhu, analalamikia utawala dhaifu usiowajibika, analalamikia sheria zisizozingatia haki na usawa na mengine mengi tu...halafu bila haya wala soni anatetea uongozi wa chama tawala na serikali huku akibeza juhudi zozote zile za kupambana na hali hiyo!

Time is running out...na mtu yeyote ambaye anaendelea kuikumbatia CCM kwa sababu zozote zile za ovyo kama eti chama kujivua gamba au kupiga vita ufisadi ndani ya CCM, ni mlafi, mnafiki na adui mkubwa wa taifa. Tuko hapa tulipo kwa sababu ya CCM, si Chadema...ni CCM na serikali yake, ni CCM na sera zake, ni CCM na ufisadi wake, ni CCM na uongozi wake, ni CCM na ahadi zake, ni CCM na udanganyifu wake, ni CCM na...Watanzania tumekuwa mateka ndani ya taifa letu, tuko jela na wengine kama mazuzu wanashangilia, OMG!
Big like
 
Wazee na vipofu kwenye sanduku la kura sasa hivi wanasema ,nitikie hapo pekundu zamani ilikuwa kijani
 
Back
Top Bottom