Mwenyekiti wa CCM kata ya Msagati ahamia CHADEMA huko Ifakara katika operesheni ya m4c

cjilo

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
884
444
M4C huko Morogoro wilaya ya kilombero kata ya masagati imeanza tena kuiaibisha CCM, Mwenyekiti huyo pamoja na waliokuwa wana ccm zaidi ya 170 nao wamfuata,wahamia CHADEMA.
Mytake:
CCM Pamoja na single yao ya CHADEMA ipo Arusha tu kutouza wakawa wanailazimisha isikilizwe tu, Walisema chama cha wachaga na WanaMorogoro leo wameamua kuudhihirishia umma kuwa CHADEMA ni chama cha Wananchi wote

source itv
 
Upepo wa mabadiliko ya kweli nchini kamwe hauzuiliki hata kwa kutumia mlima Kilimamanjaro.

Wana-Ifakara wote fuateni mfano wa mwenyekiti wenu aliyefanikiwa kuona mwanga wa mabadiliko hadi hivi sasa.
 
[h=2]Mwenyekiti wa CCM kata ya msagati ahamia CHADEMA : Ni kata ya Masagati[/h]
 
Viva wana Kilombero...viva Morogoro, mnawaonyesha njia wengine, mnawaambia watawala kuwa mmechoka na mambo yao.
 
M4C mpaka ifike 2014-15 mpaka JK atarudisha kadi ya CCM na Nina amini Nyerere angekuweko angekuwa asharudisha kadi ya magamba viva movement for change it's just the beginning bado mapichapicha hayajaanza...
 
Na diwani wa kata ya Mlimba Bw Gubuka lazima avue gamba safari hii.
M4C huko Morogoro wilaya ya kilombero kata ya msagati imeanza tena kuiaibisha CCM, Mwenyekiti huyo pamoja na waliokuwa wana ccm zaidi ya 170 nao wamfuata,wahamia CHADEMA.
Mytake:
CCM Pamoja na single yao ya CHADEMA ipo Arusha tu kutouza wakawa wanailazimisha isikilizwe tu, Walisema chama cha wachaga na WanaMorogoro leo wameamua kuudhihirishia umma kuwa CHADEMA ni chama cha Wananchi wote

source itv
 
Ni jambo la kihistoria sana tu kuona mlalahoi mwenzetu KACHANGIA YAI LA KUCHEMSHA kutokana na upenzi wake wa dhati kwa chama; People's powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
CDM wanapaswa kutengeneza kadi nyingi sana maana before 2014 inaweza kupata wanachama wapya 10 milioni. He!kweli huu mziki mnene
 
Ni jambo la kihistoria sana tu kuona mlalahoi mwenzetu KACHANGIA YAI LA KUCHEMSHA kutokana na upenzi wake wa dhati kwa chama; People's powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!
Uwezo Tunao,kama watu wanachangia hata yai basi hata ruzuku ikifutwa basi Uwezo Tunao wa kuendesha chama
 
Mwenyekiti wa CCM kata ya msagati ahamia CHADEMA : Ni kata ya Masagati

Huo ndio nauita ushujaa...wako wengi ambao hawana ujasiri wa kufanya maamuzi magumu kama hayo lakini taratibu M4C inaanza kuwajengea ujasiri kwa kuwatoa hofu. Wananchi wengi, kwa woga wa kulinda maslahi binafsi, husita kuchukua maamuzi sahihi kwa swali la je, upande ambako wamejikuta kwa sababu moja ama nyingine ndiko upande ambako kwa kweli wangependa wawepo? Nina imani kuwa hadi tunafika mwaka 2015 jibu la swali la kwa nini kuna watu wanaendelea kubaki walipo litakuwa dhahiri hata kwa kipofu.

Kwamba hadi dakika hii kuna watu ambao, bila hata chembe cha aibu, wanao uthubutu wa kusimama mbele ya jamii na kuitetea CCM, ni jambo linalofedhehesha kwa kweli. Inakuwaje mtu huyo huyo analalamikia hali ngumu ya maisha, analalamikia rushwa na ufisadi uliokubuhu, analalamikia utawala dhaifu usiowajibika, analalamikia sheria zisizozingatia haki na usawa na mengine mengi tu...halafu bila haya wala soni anatetea uongozi wa chama tawala na serikali huku akibeza juhudi zozote zile za kupambana na hali hiyo!

Time is running out...na mtu yeyote ambaye anaendelea kuikumbatia CCM kwa sababu zozote zile za ovyo kama eti chama kujivua gamba au kupiga vita ufisadi ndani ya CCM, ni mlafi, mnafiki na adui mkubwa wa taifa. Tuko hapa tulipo kwa sababu ya CCM, si Chadema...ni CCM na serikali yake, ni CCM na sera zake, ni CCM na ufisadi wake, ni CCM na uongozi wake, ni CCM na ahadi zake, ni CCM na udanganyifu wake, ni CCM na...Watanzania tumekuwa mateka ndani ya taifa letu, tuko jela na wengine kama mazuzu wanashangilia, OMG!
 
Back
Top Bottom