Mwenyekiti wa CCM ajiuzulu kwa kuhudhuria sherehe ya CHADEMA (Chanzo HabariLeo)

Kama ni yanaukweli basi Demokrasia bado sana... Collins Powell alisema kwenye television kuwa atampigia kura OBAMA na chamachake hawakumfanya chochote....hiyo ndio Demokrasia...sasa siasa hatuiwezi yani uchukiane na MAMA kisa Siasa ya U CCM na U Chadema!!!shame!!!:embarrassed:
 
Mwanamme lijar hayumbishwi na mtu kwan ccm n baba na mama yako?acha ikafie mbele kwann upate plessure ya moyo
 
Mwanamme lijar hayumbishwi na mtu kwan ccm n baba na mama yako?acha ikafie mbele kwann upate plessure ya moyo
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Makanyagio wilayani Mpanda mkoani Katavi, Chifu Mlela Mallac, amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kwamba amekuwa akizongwa mara kwa mara na wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho akituhumiwa kukisaliti.

Mallac anatuhumiwa kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani hapa mapema mwezi huu.

Mwenyekiti huyo anatoka kwenye familia ya wanasiasa kwani baba yake, John Mallac ni Mwanyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi, wakati mama yake, Anna Mallac ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema.

Mwanasiasa huyo pamoja na kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makanyagio na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda, lakini pia ni Chifu wa eneo la Mpembe lililopo Tarafa ya Mwese ambako alitawazwa kijadi kuwa mtemi wa eneo hilo mwaka jana.

Katika mazungumzo yake ya simu na kisha akiwa dukani kwake maeneo ya barabara mbili mjini hapa, Mallac alikiri kujiuzulu nafasi hiyo, akisema kuwa kama mtemi ni mtu wa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, na pia kama mtoto alikuwa na haki ya kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoani hapa mapema mwezi huu.

Lakini alisema sababu kubwa iliyomfanya ajiuzulu nafasi hiyo ya kisiasa, ni kutokana na maadili mabaya kutoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kutoka ngazi ya Kata hadi Wilaya ambapo anawatuhumu kuwa hawana siri wala uwajibikaji unaotakiwa.

Akifafanua, alisema hali hiyo ilijitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Mbunge wa Mpanda Mjini ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wilayani, alidai walikisaliti chama tawala kwa kumuunga mkono mgombea wa jimbo hilo kupitia Chadema.

Katika uchaguzi huo, Said Arfi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa alishinda tena kiti hicho kwa miaka mitano ijayo; huku CCM wakishutumiana wenyewe kwa wenyewe wakimtafuta mchawi.

“Viongozi na baadhi ya wanachama wa CCM wamegawanyika baada ya kushindwa kulirejesha jimbo hali iliyojenga chuki miongoni mwetu kusema kweli.

Baadhi ya viongozi na wanaCCM wenyewe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa nafasi ya ubunge tulidhani tuko pamoja kumbe baadhi ya viongozi wenzetu walikuwa wanafiki...Walitusaliti kwa kumuunga mkono mgombea wa Chadema,” alidai Mallac.

Katika barua yake kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, Mallac alisema anajiuzulu ili kutoharibu jina na sifa yake kwa jamii inayomwamini na kumfanya awe Chifu wao.


BADO MWENGINE
CCM wanafanya siasa za uhasama na chuki na wanadhani wao tu ndio wanatakiwa kushinda kila uchaguzi. Ni ustaarabu kabisa kumpongeza mshindi ikizingatiwa kuwa Mallac alihudhuria sherehe za kumpongeza mama yake mzazi sasa walitaka asihudhurie? Ni upuuzi huo, siasa hazitakiwi kututenganisha na wazazi, ndugu, jamaa na jamii kwa ujumla!! AMECHUKUA UAMUZI MZURI!!
 
Back
Top Bottom