Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,349
- 6,476
Wana Jf.Taarifa nilizozipata hivi leo ni kuwa Mwenyekiti Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Lewis Makame amestaafu kushikilia wadhifa huo.Mwenyekiti huyo amestaafu rasmi tangu tar 14/6 lakini kwa sasa bado haijatangazwa in public kwa kuwa anasubiri kukabidhi ofisi rasmi mara tu bada ya mtu mwengine kuteuliwa kushika wadhifa huo.Taarifa zinasema mwenyekiti huyo ilikua astaafu tangu mwaka nov 2004 lakini aliombwa na aliyekuwa Rais Ben Mkapa aendelee kushikilia nafasi hiyo kwa sababu kulikua na uchaguzi mkuu mwaka unaofuata jimbo ambalo lilihitaji mtu mwenye uzoefu.Mwaka 2009 alitaka kuachia ngazi tena akidai uzee umeshamchukua lakini Rais Kikwete alimuomba tena mzee huyu abaki Nec ili kusimamia uchaguzi mkuu uliopita mwaka jana ambao Rais Kikwete alishinda kwa mbinde.Mzee huyu ni mwenyekiti wa kwanza wa tume ya uchaguzi Tanzania jambo linalomfanya atumike sana kwa ushauri katika uchaguz wa nchi jirani kama Congo, Zimbabwe n.ksource: Chanzo Makini
Ukisoma katiba ya JMT kifungu 74 (4) unaona kuwa Ben Mkapa na Jakaya Mrisho wamevunja katiba ambayo waliapa kuifuata, kuilinda na kuitetea. Kipindi cha mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni miaka mitano tu, na wala hakuna kifungu kinachosema kuna kuongeza. Pili uzee wa huyo jamaa ndio umetufikisha hapa tulipo. Je, Augustino Ramadhani anaweza kutusaidia? Kiboko ya njia ni Robert Kissanga!!!