Mwenyekiti Halmashauri ya Uyui auwawa

Kwa jinsi mnavyokisimulia kifo hicho basi huenda marehemu aliwafanyia kitu kibaya wenzake ndo maana wakaamua wachukue maamuzi magumu. Na hayo mauwaji sio kama nayafurahia lakini huenda yakaongezeka kutokana na ugumu wa maisha unavyozidi hivi sasa, rejea miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini, kimsingi kwa sasa Tabora hari yake ni mbaya mmno vijana wengi wako kitaani wanacheza bao na drafti tu kiwanda kilichokuwepo cha nyuzi kule mwanza road kimefungwa, reli kapewa mhindi, Unaweza kumkuta kijana toka azaliwe hajatoka nnje ya mji yaani yeye ni kanyenye, kiloleni, isevya, ipuli, tambukaleli nk

My take
Serikari waliangalie kwa makini suala la ajira kwa vijana wa mkoa wa Tabora ili kuondoa gap kati ya masikini na tajiri
 
mkuu unachozungumza kuhusu tabora nisahihi! nimeishi pale! kulikuwa na viwanda walau vijana walipata pesa na mzunguko wapesa ulikuwa mzuri! siku hizi hakuna viwanda wala nini! make nakumbuka kulikuwa nakiwanda cha nyuki,kiwanda cha nyuzi nakiwanda cha maziwa! siku hizi vimekufa vyote! halafu mji ulikuwa kama umefungwa hivi hakuna barabara nzuri yakuingia mkoani! labda sasa wakimaliza huu ujenzi wa hii yakutoka Nzega na ile ya kwenda Mbeya na Itigi kuja Dodoma! wazawa nao hawako tayari kuja kupigania mkoa wao! wasomi niwengi tu Tabora!
rudini mkapiganie maendeleo yamkoa wenu!
 
WanaJF,
Usiku wa kuamkia leo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora (Mh. Mashaka) ameuawa kikatili kwa risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Ipuli nje kidogo ya mji. Ameuwawa akiwa na familia yake ambapo inasemekana ni wezi, iko hivi...
  • Nyumba yake imepigwa jiwe kubwa mlangoni maarufu kama 'fatuma' na kuweza kuingia ndani.
  • Amemiminiwa risasi 7 mkono wa kulia.
  • Risasi 8 upande wa mkono wa kushoto.
  • Amekatwa panga utosini na fuvu kuchanika.
  • Alikuwa na familia yake nyumbani.
  • Mazishi yatafanyika siku ya jumapili katika kijiji cha Utyatya-Sikonge.
  • Alikuwa ni diwani wa kata ya Iyenze.
  • Ameuwawa kati ya saa saba usiku na saa nane usiku.
  • Ameuwawa akiwa ndie mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Uyui.
  • Taarifa za kiintelijensia bado hazijatolewa na chombo kinachohusika.
  • Wauaji nao bado hawajapatikana.
Hili ni tukio baya kabisa likiwa ni la pili ndani ya miaka 5 kuhusisha madiwani/wenyeviti wa Uyui Districts na huwa hakuna taarifa kubaini wauaji zaidi ya kuzungushwa.
Mwaka 2008 tarehe 19 saa tatu usiku aliuawa diwani ambaye alikuwa ni babu yangu aitwae Salum Said Mgeleka wa kata ya Ibiri ambapo hadi tuongeavyo hakuna taarifa zozote za kiintelijensia zilizobaini wauaji zaidi ya porojo. Mzee Mgeleka aliuawa kwa kupigwa risasi tatu pajani na kutelekezwa jirani ya mtaro ambapo bleeding ilisababisha kifo chake. Huyu pia alikuwa jirani kabisa na nyumbani kwake. Inaogofya.

MY TAKE: Tabora inatisha sana kwa mauaji ya aina hii, serikali zote kuu zipo lakini sijui tatizo ni nini. Kuna harufu mbaya sana. Wale wanaowania nafasi fulani za Tabora wawe chonjo na aina hii ya mauaji.

Source: Madiwani 2 wa Uyui, kunijuza kwa kunipigia simu.

Mkuu usisahau na lile tukio la kuuawa kwa mume wa mkurugenzi wa uyui mwaka 2005. Katika tukio hilo mkurugenzi wa uyui ambaye yupo hadi sasa alijeruhiwa vibaya kwa mapanga.
 
Tabora sometimes ni kama lawless vile. Kuna miaka ya nyuma Tabora ilikuwa ni tishio hasa, kulikuwa na watu kama Issa Kandege, Kassim Mchemba, Kashilombo et al. Hawa walikuwa kutoa roho ya mtu ni kama vile kuchinja kuku kwao.

Kumewahi kutokea matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na mauji ya kulipiza visasi kwa kudhulumiana. Mfano miaka hiyo mi nikiwa pale kulikuwa na Mama mmoja akijulikana kama Biti Slim, huyu alikuwa ni storekeeper wa majambazi na ikafikia mahali akawadhulumu wakaja kumuua tena yeye walichofanya walikatakata na sehemu za viungo vya mwili wake kana kwamba wanapeleka buchani.

Mauaji mengine yanayohusiana na dhuluma ni kama yale ya Kanali wa Jeshi Shimanyi, kuua familia ya mtu aliyekuwa ana mdai na jamaa kumzunguusha sana siku aliyopania kwenda kummaliza jamaa alichomokea dirishani na kuacha familia exposed hivyo kumfanya kanali wa jeshi kumalizia hasira zake hapo. Huyu alihukumiwa kunyongwa ila mpaka leo haijulikani kama adhabu hiyo ilitekelezwa.

Ukija katika suala la raia kuuwawa kwa nondo na wezi ilikuwa ni kama normal vile. Kuokota miili imelazwa kwenye reli au machakani ni normal. Kwa ujumla Tabora si mahala salama sana hasa kama unaingilia masilahi ya wahuni wachache.

Ukija wizi wa kwenye treni. Ukifika Tabora ilikuwa mnajiandaa kabisa maana ni headqurter, sijui miaka hii ishirini na nane niliyo nje ya mkoa huo kama kuna kilichobadilika pale.
 
Kwa jinsi mnavyokisimulia kifo hicho basi huenda marehemu aliwafanyia kitu kibaya wenzake ndo maana wakaamua wachukue maamuzi magumu. Na hayo mauwaji sio kama nayafurahia lakini huenda yakaongezeka kutokana na ugumu wa maisha unavyozidi hivi sasa, rejea miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini, kimsingi kwa sasa Tabora hari yake ni mbaya mmno vijana wengi wako kitaani wanacheza bao na drafti tu kiwanda kilichokuwepo cha nyuzi kule mwanza road kimefungwa, reli kapewa mhindi, Unaweza kumkuta kijana toka azaliwe hajatoka nnje ya mji yaani yeye ni kanyenye, kiloleni, isevya, ipuli, tambukaleli nk

My take
Serikari waliangalie kwa makini suala la ajira kwa vijana wa mkoa wa Tabora ili kuondoa gap kati ya masikini na tajiri

Hapa Tabora ni kwamba kuna siasa za makundi ambapo ndizo zaathiri yote, na wakubwa zaidi hususan wale majemedari wa mkoa/wilaya na halmashauri ndio vinara wa mipango (deals). Hivyo itokeapo jamboa lao ama likazuiwa au likakawizwa...basi yule anayekawiza hutoweka kabisa duniani na si kutoweka ktk ramani ya siasa. Nadhani sasa kwa tukio hili huenda (labda) Manumba na akina Chagonja wanaweza kuamua kutilia mkazo, otherwise zitakuwa ni siasa za visasi tu. Nakumbuka vilivyo aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo-hiyo mzee Mgeleka alivyotandikwa risasi kwa same issues hususan ukiegemea upande wa jamii...unapotezwa.
 
... Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
Hivi Bwana hawezi kutwaa peacefully, mpaka akupigishe risasi umelala nyumbani na watoto na mkeo? Huyo Mungu ka Alkaida? Mtu kauawa, jina lake lihimidiwe... kwa lipi?

Anyhow, naona Tabora inaongelewa kana kwamba haya hutokea Tabora tu, yapo haya hata Samora Avenue mchana kweupe. Polisi wamelala tu.
 
Mkuu usisahau na lile tukio la kuuawa kwa mume wa mkurugenzi wa uyui mwaka 2005. Katika tukio hilo mkurugenzi wa uyui ambaye yupo hadi sasa alijeruhiwa vibaya kwa mapanga.

Daahh....tulimzika huyu mzee mkewe akiwa ICU Muhimbili.
RIP mzee Kimwela!
 
Back
Top Bottom