Mwenyekiti Halmashauri ya Uyui auwawa

Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,581
6,675
Diwani wa kata ya MIYENZE NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA UYUI AMEUWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO NYUMBANI KWAKE IPULI MJINI TABORA.

Nimepokoa kwa maskitiko makubwa taarifa ya msiba huu mzito na mkubwa kwa wanauyui wote hasa wapenda maendeleo.Kwani Mh.alikuwa mtu wa watu,mpenda maendeleo.Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
 
poleni wafiwa.. Sisi sote ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea.. Hakuna aijua siku saa wala dakika ya kuondoka hapa duniani..
 
Kama hakuna wizi uliofanyika ni mkono wa mtu..keshawabania watu mlo wao....Tanzania sometimes inatisha sana
 
poleni sn wana uyui pamoja na familia ya mlehemu.mkuu waweza kuelezea mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo kabla ya kukubwa na umauti,jinsi watu walivyopokea msiba na kauliya polisi.
 
nakumbuka kuna diwani wa tabora,kanyenye alivyolambwa risasi kwake,siku moja kabla ya kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mkurungenzi (mama khalfan na genge lake wakina munde tambwe)walivyokuwa wakitafuna pesa za halmashauri.isije ikawa ndio yaliomkuta huyo diwani.tabora huwa ni shamba la bibi.ni sehemu pa kuchumia mihela.
 
ccm ukiwa mzuri hawakutaki na ukikomaa watakuuwa reference Mbeya(mbunge mawaziri), geita (diwani) etc
 
nakumbuka kuna diwani wa tabora,kanyenye alivyolambwa risasi kwake,siku moja kabla ya kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mkurungenzi (mama khalfan na genge lake wakina munde tambwe)walivyokuwa wakitafuna pesa za halmashauri.isije ikawa ndio yaliomkuta huyo diwani.tabora huwa ni shamba la bibi.ni sehemu pa kuchumia mihela.
Hivi ile kesi ya Mkurugenzi Mama Khalfani ilikwisha isha?
 
R.I.P. Diwani.
Habari nilizo zipata hivi punde nikwamba alikua anamendea nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoa na alikua anakubarika kwani nikambi ya rostam hivyo kuondoa upinzani wameamua kumpeleka mbele ya haki kabla ya siku yake.
 
WanaJF,
Usiku wa kuamkia leo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora (Mh. Mashaka) ameuawa kikatili kwa risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Ipuli nje kidogo ya mji. Ameuwawa akiwa na familia yake ambapo inasemekana ni wezi, iko hivi...
  • Nyumba yake imepigwa jiwe kubwa mlangoni maarufu kama 'fatuma' na kuweza kuingia ndani.
  • Amemiminiwa risasi 7 mkono wa kulia.
  • Risasi 8 upande wa mkono wa kushoto.
  • Amekatwa panga utosini na fuvu kuchanika.
  • Alikuwa na familia yake nyumbani.
  • Mazishi yatafanyika siku ya jumapili katika kijiji cha Utyatya-Sikonge.
  • Alikuwa ni diwani wa kata ya Iyenze.
  • Ameuwawa kati ya saa saba usiku na saa nane usiku.
  • Ameuwawa akiwa ndie mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Uyui.
  • Taarifa za kiintelijensia bado hazijatolewa na chombo kinachohusika.
  • Wauaji nao bado hawajapatikana.
Hili ni tukio baya kabisa likiwa ni la pili ndani ya miaka 5 kuhusisha madiwani/wenyeviti wa Uyui Districts na huwa hakuna taarifa kubaini wauaji zaidi ya kuzungushwa.
Mwaka 2008 tarehe 19 saa tatu usiku aliuawa diwani ambaye alikuwa ni babu yangu aitwae Salum Said Mgeleka wa kata ya Ibiri ambapo hadi tuongeavyo hakuna taarifa zozote za kiintelijensia zilizobaini wauaji zaidi ya porojo. Mzee Mgeleka aliuawa kwa kupigwa risasi tatu pajani na kutelekezwa jirani ya mtaro ambapo bleeding ilisababisha kifo chake. Huyu pia alikuwa jirani kabisa na nyumbani kwake. Inaogofya.

MY TAKE: Tabora inatisha sana kwa mauaji ya aina hii, serikali zote kuu zipo lakini sijui tatizo ni nini. Kuna harufu mbaya sana. Wale wanaowania nafasi fulani za Tabora wawe chonjo na aina hii ya mauaji.

Source: Madiwani 2 wa Uyui, kunijuza kwa kunipigia simu.
 
Tukio baya kabisa hili sababu ya mauaji hayo ya kikatili ni nini?
 
Back
Top Bottom