Elections 2010 Mwenyekiti CCM K'njaro naye aanguka jukwaani

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
SIKU tatu baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kuishiwa nguvu wakati akizindua kampeni za Uchaguzi Mkuu wa chama hicho akiwa jukwaani, jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vick Siro Swai, naye aliishiwa nguvu jukwaani na kuelekea kuanguka kabla ya kuokolewa na wasaidizi wake wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani katika Jimbo la Hai.

Tukio hilo lilitokea kwenye uwanja wa CCM eneo la Bomang’ombe muda mfupi baada ya mwenyekiti huyo kuanza kuwanadi wagombea udiwani.
Baada ya kukutana na kadhia hiyo ya kiafya, mwenyekiti huyo alipumzishwa kwa muda wa dakika 30 na baadaye kupewa maji ya kunywa kabla ya kurejea tena.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku tatu baada ya Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kuishiwa nguvu wakati akizindua kampeni za chama hicho kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, kabla ya kusaidiwa na wasaidizi wake.

Aliporejea kuhutubia jukwaani alisema alipatwa na tatizo hilo kutokana na kushikwa kiu na baadaye aliendelea kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Fuya Kimbita, ambaye anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mama Swai alisema CCM inategemea kuendesha kampeni za amani na utulivu na haitarajii kusukumwa kwa ajili ya kuchukua hatua za kujihami endapo watafanyiwa vurugu.
 
Mwaka huu wale wote watakaosimama kwenye majukwaa ya kampeni kuomba kura, huku wakiwa ni mawakala wa kuzimu, watapata aibu ya kukata na shoka.
 
Aisee, kusimama jukwaani huku unahofu ya kuona utakayo kuyasema ni ya uongo mtupu, ni lazima uishiwe nguvu kwa vile hata dhamira ina kusuta
 
Kwani nae kafunga?
Baadae itakuwa ndo style ya kukonga nyoyo za watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom