Mwenyekiti BAVICHA wa Wilaya ashikiliwa na Polisi kwa Wizi

Ngarenaro

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
308
45
Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya, ndugu Emmanuel Mlak, ambaye ni muasisi wa CHADEMA, Tawi la Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, awekwa ndani kwa siku mbili baada ya kuiba vitu akishirikiana na wenzake wa eneo la Semtema amabo ni wezi.

Kiongozi mmoja wa CHADEMA Taifa ambaye ni Mbunge, kamtoa sasa polisi kwa gharama ya Sh. 350000, ili kesi ifutwe na wamekabidhiwa walioibiwa.

Vitu alivyoiba ni pamoja na radio, mabegi 2, nguo za kike na suti 2, kibaya zaidi ni kwamba anamiliki funguo bandia kufungulia hostels za wanafunzi na nyumba za watu jirani. Pia bwana Mlaki anaendelea kutuhumiwa kutumia mihuri ya Mkuu wa Chuo, Dean of students na mhasibu wa chuo kujipatia fedha toka kwa wahisani wa CHADEMA na viongozi wa juu wa CDM.

Serikali ya wanafunzi imeonelea swala hilo liende uso wa sheria za Chuo ili kulinda Image ya Chuo.
Mlaki amemtumia mbunge wa Iringa Mjini ili amsaidie kuongea na Mkuu wa Chuo juu ya jambo hilo.
Twasubiri hatua za Mbunge huyo katika jitihada za Kumnasua M/kiti huyo wa BAVICHA.
Hawa ndio viongozi wa kesho wa CHADEMA

Naomba kuwasilisha.
 
Kama kweli kafanya hivyo, itabidi achukuliwe hatua kali za kisheria na pia asimamishwe uongozi wa chadema katika hiyo sehemu.

Hiyo ni kwa sababu anachafua image ya chama na chuo kwa ujumla. Tabia kama hizo ni vizuri zisivumiliwe ndani ya chama ili kujitofautisha na CCM ambayo wizi kwao sio kosa.
 
Kwanza umeleta kimajungu majungu BUT pia ujue kuwa MLAKI WALA DR SLAA SIO NDO CHADEMA..nao wanaweza kukosea
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya CCm na Chadema. Chadema hatulindi wala kutetea wezi. Huyo aingie chama cha magamba.
 
Tabia kama hiyo si nzuri ata kidogo,huyu bado hajapewa madaraka makubwa ndani yua chama na serikali kafanya hivyo je tukimpa madaraka itakuwaje?siyo huyo tu ata Lema ilishawahi semwa ni jambazi na Zombe alishawahi kutamka hadharani hivyo,Dr slaa ksiba mke wa mtu,Mbowe alituhumiwa kukwepa deni la nssf na ata chama chenyewe kilikuwa kinakwepa kodi TRA , hiyo ndiyo chadema inayotaka tuikabidhi madaraka ya kuongoza taifa,hawa watu uliwatafakari kwa makini wanataka madaraka kwa fujo na vurugu lengo lao kuu ni kuiba na kufilisi rasirimali za taifa letu ,Ewe mtanzania amka kataa chadema illi kulinda rasirimali za Tanzania!
 
Kawachukulieni hatua wakina Chenge na Lowassa na wengine wengi ndani ya CCM hili suala Dogo la CDM tuachie wenyewe

Kwahiyo Pro Chadema kwenu ni sawa viongozi wenu wakiiba eti kwasababu viongozi mmoja mmoja wa chama kingine nao wanaiba?

Shame on you
 
Kwako hizo ndo habari nzuri, Hivi nani alimuua Baba wa Taifa, Alimteka olimboka na kuwaua wanachama wa chadema
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya CCm na Chadema. Chadema hatulindi wala kutetea wezi. Huyo aingie chama cha magamba.

Ina maana umegundua leo kwamba kiongozi wenu ni mwizi wakati mlikua mnamfuga wenyewe mpaka leo ameiva?
 
Tabia kama hiyo si nzuri ata kidogo,huyu bado hajapewa madaraka makubwa ndani yua chama na serikali kafanya hivyo je tukimpa madaraka itakuwaje?siyo huyo tu ata Lema ilishawahi semwa ni jambazi na Zombe alishawahi kutamka hadharani hivyo,Dr slaa ksiba mke wa mtu,Mbowe alituhumiwa kukwepa deni la nssf na ata chama chenyewe kilikuwa kinakwepa kodi TRA , hiyo ndiyo chadema inayotaka tuikabidhi madaraka ya kuongoza taifa,hawa watu uliwatafakari kwa makini wanataka madaraka kwa fujo na vurugu lengo lao kuu ni kuiba na kufilisi rasirimali za taifa letu ,Ewe mtanzania amka kataa chadema illi kulinda rasirimali za Tanzania!
Huko kwenu CCM ni kusafi sana ndio maana unaona kwa Chadema?
 
Kwako hizo ndo habari nzuri, Hivi nani alimuua Baba wa Taifa, Alimteka olimboka na kuwaua wanachama wa chadema

Baba wa Taifa alikufa kwa Kansa ya Damu yaaani Leukemia. Siwezi kulisemea zaidi kwani ni Kazi ya Mungu.

Ulimboka waliomteka wameanza kukamatwa na bado uchunguzi unaendelea

Hata hivyo huwezi kuhalalisha uovu unaoufanya kwasababu wengine nao walifanya, wewe utakua ni kiumbe wa ajabu kutokea dunia hii. Sababu utachukuliwa hatua kwa kosa ulilolitenda wewe binafsi kwa mujibu wa sheria zilizopo
 
Kama mwizi kweli anyongwe tu hamna mjadala.Hawa waizi wadogowadogo ni wakuwadhibiti mapema kabla hawajaanza kunogewa
 
Kawachukulieni hatua wakina Chenge na Lowassa na wengine wengi ndani ya CCM hili suala Dogo la CDM tuachie wenyewe

Si vizuri kupindisha maada Suala la chenge na Lowasa haliusiani hapa,tumjadili huyu mwizi mimi nafikiri waliomkamata wangemchoma moto kama tuchomavyo vibaka wengine huyu kibaka akiachiwa ataendelea kuiba kwani tabia yake ya uwizi iko kwenye damu alafu mbunge eti anaenda kumtoa na kutaka kulimaliza suala kimya kimya yani nae anatetea uwizi,wahusika huko mlipo Iringa tunaomba mumchukulie atua kali za kisheria huyo BAVICHA!
 
hta chadema ni wanadamu sio manyani sasasikiliza hukumu yake utajua kwamba cdm sio ccm waulize madiwani wa arusha
akithibitika ni mwizi atakwisha
 
Back
Top Bottom