Mwenyekiti BAVICHA Taifa ndani ya Same

Wapendwa wana JF Habari za uhakika ni kwamba Kilio Cha Wananchi Wilaya ya Same kwa uongozi wa CHADEMA Taifa kimesikika na Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA Anatarajiwa kuanza Ziara yake ya Siku 4 Same. VUA Gamba Vaa Gwanda Kuanzia tar 10/05/2012. Mkutano wa ufunguzi wa Ziara hiyo utafunguliwa Standi kuu ya mabasi Same Alhamis tar 10 saa 7 mchana na Ratiba za ufunguz Rasmi wa ofisi za CHADEMA kata zote utaendelea kwa siku zote hizo. Karibuni wote Kadi na vifaa vingine vitakuwepo. Waandishi wahabari wote mnakaribishwa kurusha matukio ili Wa Tz waone jinsi wana nchi wa Same walivyo ichoka CCM na Wabunge wake. Mwisho Shukrani ziwafikie viongozi Wa CHADEMA TAIFA WOTE

Eti Chama cha msimu! Kwa heri kilango
 
kumbukeni kufanya kazi, mikutano isiyoisha itawaletea njaa na umasikini. Kazi kwanza.

Kwa hiyo kutokana na ubongo wako....Harakati za ukombozi na utoaji elimu ya uraia na utambuzi si Kazi.? Kwako wewe kazi ni kukata utepe tu..?Anyway sikushangai maana hata hapa Dar zamani kulikuwa na usemi kwamba "UNA KAZI KWANI WEWE NI M....?"
 
kumbukeni kufanya kazi, mikutano isiyoisha itawaletea njaa na umasikini. Kazi kwanza.

Unamwambia nani hapa....kwa sababu hao wanachama wa CHADEMA wanafanya mikutano ambayo ndio kazi yao...kwani hao wameajiriwa na chama.
Mikutano wanafanya jioni muda ambao watu wengi wametoka makazini...na sijaona sehemu wanayohamasisha watu kuacha kazi.
Kuna watu wanatazama mpira kila siku jioni ligi mbalimbali ina maana hawafanyi kazi?
Think as a human being!
 
Sawa SJ piten kila uchochoro msake hao nyoka wenyewe magamba goigoi ili wasiwepo tena kwenye majimbo walokuwepo, juhumu zako zisambae TZ yote.
 
Simon nimeupenda sana uzalendo wako kwa wilaya ya same.Mimi ni mdau mkubwa wa siasa za same na nafahamu vema kwamba maeneo mengi ya miliman ndiyo yaliyobaki ktk harakati za ukombozi.mpeleke bw Heche maeneo yote ya miliman mtapata ushindi mkubwa kamanda.
 
Sante kwa ushauri
Simon nimeupenda sana uzalendo wako kwa wilaya ya same.Mimi ni mdau mkubwa wa siasa za same na nafahamu vema kwamba maeneo mengi ya miliman ndiyo yaliyobaki ktk harakati za ukombozi.mpeleke bw Heche maeneo yote ya miliman mtapata ushindi mkubwa kamanda.
 
Mpeleke bw Heche mamba,bombo,lugulu,bwambo,kirangare,vunta,vugwama,suji,mbaga,vudee,chome,gavao na sehemu nyingine kwa sababu maeneo ya tambarare kazi imeisha.big up!
 
Mh! Ukiona hadi kiongozi wa ka-jumuiya ndani ya chama cha siasa ziara zake zinakuwa na mwitikio mkubwa hadi huko vijijini kweli tumefika patamu. Hivi Beno na Shigela vipi?
 
Mkuu Simon James,
Heshima kwako kamanda, kweli umepigania kuhakikisha vita ya ukombozi inafika Same, na juhudi zako tumeziona.
Hongera sana, endeleeni kuwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano.

Mungu Ibariki Same
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania

kwenye mikutano ya cdm watu huwa wanapewa taarifa tu. Hamasa wanayo mioyoni mwao.
 
Back
Top Bottom