Mwenyeketi wilaya CDM anunuliwa na CCM, aanza kuhujumu cdm

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Ndugu wa JF

Naomba mnisaidie kufikisha taarifa hizi kwa viongozi wa Taifa CDM (MBowe na Slaa) kuwa kuna Kaimu mwenyekiti wa wilaya Tarime anahujumu CDM kwa masilahi ya CCM kwa kuzuia mikutano ya kujenga CDM kufanyika .

Ilikuwa mwenyekiti wa BAVICHA HECHE afanye mikutano katika wilaya ya tarime akazuiliwa na POLICE kwa maelezo kwamba wamepewa barua na mwkt wa CDM kuwa mikutano ya Heche ina agenda binafsi au hajui Heche anataka kufanya mikutano kwa masilahi ya nani? (attached barua), kwa taarifa niliyoipata Heche alikuwa ameandaa mikutano iliyoombewa kibali na katibu wa CDM wilaya (attached) ,Heche alifanikiwa kufanya mkutano mmoja maeneo ya SIRARI Baada ya mabishano makali ya POLICE wilayani humo

Inasemekana mwenyekitu huwa anafanya kazi ya CCM ya kuua chama jimboni humo alioianza kabla ya uchaguzi mkuu 2010 na anaendelea na kwa kuhakikisha CDM hairejeshi halmashauri na jimbo.

Alivyohojiwa mwkt wa wiliya Tarime alisema kuwa HECHE amekuja tarime kwa mapumziko haruhusiwi kufanya mikutano (Je hili ni sahihi kumzuia Mheshimiwa kufanya kazi ya kujenga chama? alitaka Heche akacheze disco ndo arizike?)

Nimeambatanisha barua za kibali cha kufanya mikutano na barua ya mwkt wilaya cha kuzuia mikutano hiyo
 
Kwa hiyo jf kumbe kuna watoa taarifa sahihi kwa viongozi wa juu chadema? Mbona heche mwenyewe ni mjumbe wa kamati kuu anao uwezo wa kumshugulikia kaimu mkt wa wilaya,haya ni majungu ya kikie.
 
Kwa hiyo jf kumbe kuna watoa taarifa sahihi kwa viongozi wa juu chadema? Mbona heche mwenyewe ni mjumbe wa kamati kuu anao uwezo wa kumshugulikia kaimu mkt wa wilaya,haya ni majungu ya kikie.

ukiwa na ubongo ambao upo uchi kuna madhara makubwa ya kimawazo kama haya uliyonayo ww mwndawazimu.
 
kwa hiyo jf kumbe kuna watoa taarifa sahihi kwa viongozi wa juu chadema? Mbona heche mwenyewe ni mjumbe wa kamati kuu anao uwezo wa kumshugulikia kaimu mkt wa wilaya,haya ni majungu ya kikie.
yangekuwa majungu asingeweka viambatanisho vya barua, angeishia kutoa hisia zake.haya yapo katika siasa mchezo mchafu upo hasa kwenye majimbo ambayo cdm anaweza kuyachukua.tuliona nccr kwenda pemba kushindania majimbo wakati haikuwa hata na shina moja.inajulikana hilo jimbo lilichukuliwa kwa hila za ccm, hivyo wanataka kuendelea kulimiliki, kwa ktumia mbinu kama hizi .huyo mdau aliyefichua ni mkereketwa wa kwli wa chama cha cdm.chama hujengwa na wanachama wote na si viongozi kama ilivyo kwa xaxa kwa chama cha ccm, kinakufa huku wanaona ati kuna safu ya viongozi wasiokuwa na dhamira maridhwa na kujenga chama wala uchungu na chama.mdau aliyeleta thread hii apongezwe
 
Huyu ni wa kumtimua arudi ccm ndiko anakostahiri kuwa...lakini pia cdm inaonekana kua virusi vingi sana vya kuscan kama huyu ni mmoja wao...naamini hili ni muendelezo wa vit ya makundi iliyosababisha jimbo kubwa kama Tarime kuongozwa na mtu mwenye upeo mdogo kama Mbunge wa sasa,,,ni aibu
 
attachment.php
 
Mkono wa Wassira unaonekana Live bila chenga. Ndio mpango mkakati huo aliousema kuwa cdm itakufa kabla ya uchaguzi wa 2015. Naona ameamua kuanzia na kwao.
BAHATI MBAYA HATAWEZA, WATADHALILIKA NA MTU WAKE.
 
KUMBE KAMPENI ZIMEANZA au labda kuna kaUchaguzi kadogo ka kuziba nafasi, au ni Operation za kawaida mpaka 2016 na hta mpaka 2020
Kwani Mwenyekiti hajui ni nini kinachotakiwa? bora alivyofanya Zitto kule Kigoma lakini kumkuta M/kiti na kutomuarifu huenda ni sawa kwa baadhi ya Vyama
 
ile barua ya kusitisha mkutano naomba muisome vizuri kwa umakini, nahisi kuna vitu vinamiss na imefanywa makusudi. hii mihuli mbona sio genuine. anyway ngoja tusubirie wataalam wa forensic investgations.
 
Kumbe viongozi wa CHADEMA nao wananunulika! Nimekuwa nikisoma hapa kuwa CHADEMA ikipewa nchi hakutakuwa na ufisadi, maneno hayo na ninachokiona ni tofauti!!!
 
lakini isije kuwa ni vita vilevile ndani ya wanachadema vilivyosababisha jimbo kuchukuliwa na CCM 2010, maana walikuwapo Heche, Mwita Mwikabe Waitara na kwa mbali kambi ya Mwera, sasa isijekuwa huyo jamaa hamtaki heche anawalinda hao wengine, na kama mnakumbuka iliwahi kuwepo thread hapa kuhusu kwa nini chadema ilishindwa tarime, na ikaonekana hawa watu watatu mgawanyiko wao ndio uliochangia kushindwa!!

it is just a thought!! mnapofanya uchunguzi broaden your possibilities kwa jicho la tatu!!
 
huyu hatekelzi ile slogan ya "HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE".

Hata kama Henche amekwenda likizo, kufanyakazi za Chama kwa manufaa ya watanzania ni halali. Huyo mwenyekiti anataka Henche alale ili kisieleweke-aonyeshwe mlango wa kutokea aende Magambani!
 
Kumbe viongozi wa CHADEMA nao wananunulika! Nimekuwa nikisoma hapa kuwa CHADEMA ikipewa nchi hakutakuwa na ufisadi, maneno hayo na ninachokiona ni tofauti!!!

Mkuu viongozi wa Chadema si malaika, ni wanadamu na ni watz kama wengine. Tofauti ya Chadema na CCM ni kwamba ikithibitika kuwa xyz ni fisadi, tunachukulia hatua za kinidhamu badala ya kufunika kama ccm. That is the main difference mkuu wangu.

 
Pengine ugomvi umeanzia hapa:

Heche kugombea ubunge Tarime



na Sitta Tumma, Tarime


amka2.gif

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana (Bavicha) Taifa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Tarime mkoani Mara, mwaka 2015.
Heche alisema kuwa, iwapo dhamira yake hiyo itapewa baraka na chama chake, kwa kupitisha jina lake, atahakikisha anapigania maendeleo makubwa ya wananchi wa Tarime, ikiwa ni pamoja na kuwanusuru na umasikini uliokithiri.
Kada huyo aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika viwanja vya sokoni, Sirari, ambapo pamoja na mambo mengine, aliirushia kombora Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa imehindwa kutumia vizuri rasilimali za nchi kuleta maendeleo.
Alisema, msukumo wa kutaka kugombea ubunge unatokana na uchungu alio nao wa kutaka kuweka chemichemi kubwa ya mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo, pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha wakazi wa Tarime na Watanzania wote.
"Huu ni wakati wa ukombozi wa nchi hii. Maana Serikali hii ya CCM imeshindwa kabisa kuwasaidia wananchi wake!. Rasilimali za kila aina, zipo hapa Tanzania, lakini zinawanufaisha watu wa nje ya nchi.
"Kwa maana hiyo, mwaka 2015 kama Mungu ataniweka hai nitagombea ubunge Tarime. Kama chama changu kitanipitisha, nimejipanga vizuri kuhakikisha ninaleta mabadiliko ya kimaendeleo hapa," alisema Heche.
Kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, mwenyekiti huyo alimshutumu Rais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kujenga uchumi wa ndani ya nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo, badala yake rasilimali hizo zinayanufaisha wageni.
Alisema, licha ya kuwepo kwa madini ya almasi, dhahabu, makaa ya mawe, nyuklia, gesi na madini yanayotengeneza ndege na kompyuta, maziwa, bahari, mbuga za wanyama na milima mikubwa, watanznaia wanazidi kuteseka kwa umasikini wa kutupwa.
"Tanzania ina kila aina ya madini, lakini umasikini ndiyo unazidi kuota mizizi na kuwatesa Watanzania. CHADEMA hatukubaliani na hali hii, tujiandaeni tuiondoe CCM kupitia sanduku la kura mwaka 2015," alisema Heche.
Source: Heche kugombea ubunge Tarime


 
Wanachadema wanafahamu malengo ya mikutano inayoendelea nchi nzima kuwa ni kutoa elimu kwa umma. Sasa huyu BUNJU asiyejua nini kinaendelea ametokea wapi kwenye hiyo nafasi. Yawezekana ndiyo chanzo cha Cdm kushindwa ubunge 2010 huko Tarime.
 
Back
Top Bottom